Mkurugenzi wa Kitengo kipya cha Biashara Cha Vodacom (Vodacom Business) Dylan Lennox akizungumza Jijini Dar wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari juu ya uanzishwaji wa kitengo hicho ambacho kitaboresha huduma za mawasiliano za Vodacom Tanzania.waliokaa wa kwanza kushoto ni Afisa Biashara Mkuu wa Vodacom Gideon Hugo, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo kwa makampuni makubwa, George Kivaria na Mkurugenzi wa Mauzo wa Kitengo cha Biashara Cha Vodacom Tanzania Felista Jenssens

Wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo
Juu na chini Maafisa waandamizi wa Vodacom wakbadilishana mawazo
Vodacom yazindua kitengo chake cha biashara

· Huduma za mawasiliano kutolewa kwa pamoja na kwa ubora

Dar es Salaam, Tarehe 08.09.09. Vodacom Tanzania imeanzisha kitengo cha Kibiashara kijulikanacho kama Vodacom Business lengo likiwa kukidhi mahitaji ya wateja ya kibiashara yanayokua kila siku.

Mkurugenzi wa Biashara ya Vodacom, Bw Dylan Lennox amesema kuanzishwa kwa kitengo hiki kunatokana na mahitaji makubwa ya kibiashara ya wateja yanayokua kila kukicha.

“Kitengo hiki ya Kibiashara cha Vodacom kina lenga kuboresha na kurahisisha njia za mawasilaiano za wateja wetu kwa Kutumia teknolojia za kisasa zaidi za mawasiliano ya kiofisi,biashara na kibinafsi kwa kwa kasi na kwa gharama nafuu,”

Bw Lennox amesema “Vodacom Business” ina nia ya kutoa huduma zote ambazo ni zaidi ya ile ya sauti iliyozoeleka na sasa kujumuisha huduma za data na internet,” alisema.

Alifafanua kwamba huduma za data ambazo zitayawezesha makampuni ya hapa nchini na makampuni mama kokote Duniani kuwasiliana kwa kasi ya ajabu.

Huduma nyingine ni pamoja na Wimax na simu za mezani .
Ili kuhakikisha kwamba Vodacom Tanzania inatoa huduma za uhakika imeshirikiana na kampuni ya maarufu ya mawasiliano ya Gateway ambayo inamilikiwa kundi la makapmuni ya Vodacom.

Bw Lennox amesema Vodacom ina mkakati wa kuboresha huduma zake na kuwa za kisasa zaidi ili kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma zote kwa pamoja na kwa wakati.

“Tutahakikisha kwamba Vodacom Tanzania inaendelea kuongoza katika mawasiliano ya mawasiliano,” alisema.

Alisema Vodacom Tanzania ndiyo mkombozi pekee na njia ya kukata kiu ya mawasiliano ya Watanzania na hivyo kuharakisha maendeleo yao.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Papa G naona mambo si mabaya kila la kheri

    ReplyDelete
  2. juu na chini wapi wakibadilishana mawazo? naona juu wakaa na chini wamesimama, picha mbili tofauti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...