Jokate Mwegelo msemaji wa Kampuni ya DT Dobie Tanzania akijaribu gari mpya aina ya Mercedes Benz E Class, Sehemu mapato ya mauzo ya gari hilo yatatumika katika kusaidia vituo mblalimbali vinavyohudumia watoto yatima ambao wazazi wao wamefariki kwa madhara ya UKIMWI. Kulia ni Meneja Biashara wa kampuni hiyo Bw. Wayne Mcintosh na katikati ni Bw. Marco Kahabi ambaye ni Meneja wa Tenda wa kampuni hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. sasa hapo mmeongea, ningependa kuona MASHANGINGI YA WABUNGE NA MAWAZIRI pia nayo yanapigwa mnada kusaidia wananchi kuondosha shida zao mbalimbali kama kuboresha huduma za afya badala ya kusubiri WAHISANI waje.

    ReplyDelete
  2. Mtume, bad luck sina pochi. Hii ni dream come true: una pose na watoto yatima unasaidia.. vi keep left tu ndio taabu.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  3. ilo gari zuri sana. jee bei ni vipi.

    ReplyDelete
  4. KWELI NYIE NDIO HAMJUAGI KULA NA VIPOFU AISEE,UBAYA WA MAFISADI HAWANA ROHO YA KUSAIDIA AU HURUMA KWA JAMII NA KWA BONGO MWENGINE ATAKUWA NI NANI MWENYE UWEZO WA KULINUNUA HILO KAMA SIO HAOHAO TU??MI NINGEWASHAURI MBADILISHE TANGAZO KAMA KWELI MMEDHAMIRIA MLIUZE MUWASAIDIE MAYATIMA,MNGESEMA HIVI""PESA ITAKAYOPATIKANA ITAPELEKWA KWENYE MAMBO YA U-MISS"" UNGEWAONA SASA WANGEPIGANA VIKUMBO HAPO NA HATA BEI WANGELIPA EXTRA WAPATE UJIKO TU KISHA BAADAE PESA MNAIPELEKA KWA YATIMA .AAAAAHH PAPAA JACK PEMBA WAPI OMARI TOLI AU PEDESHEE NDAMA MUTOTO YA NGÒMBE.UZURI WA BONGO HUHESHIMIWI BILA KUWA NA PESA HATA UWE MUUNGWANA KUWAZIDI MANABII NI KAZI BURE TU NA WANACHOKIJALI WAO NI PESA HAIJALISHI PESA HIO UNAIPATAJEPATAJE.CRIMINAL LAND BONGO I LOVE YOU

    ReplyDelete
  5. Haaaa!!!! masikini wee huyu mtoto Jokate ndo nishamkosa hivyo! mtoto nlikuwa nampigia mahesabu huyu!! dah basi tena kama keshaangukia midomoni mwa hawa jamaa wakampa na usemaji wa kampuni yao mh ndo basi tena sina changu hapo. hii mizungu na yenyewe si ingekuwa inakuja na wa kwao badala ya kutolea mimacho vibinti vyetu vizuri kisha inajifanya kuwapa vyeo kwenye makampuni yao wizi mtupu!!

    ReplyDelete
  6. from berlin or frankfult,pleeeeeeeeeeeese wekeni bei kabisa nimechoka na skini hedi wa moscow waliaribu gari yangu mpya aina ya infinity nakuja bongo nataka nijue bei kabisa nijipange wekeni bei,ERASTO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...