Wakurugenzi wa Vodafone na Vodacom wakienda kuzindua rasmi mradi wa mifugo wenye thamani ya Sh Milioni 12 kwa ajili ya kusaidia huduma za watoto yatima wa kituo cha Yatima Trust Fund cha chamanzi mbagala.
Mkuu wa Mfuko wa kusaidia Jamii wa Vodacom,Vodacom Foundation Mwamvita Makamba akiwaongoza wakurugenzi wa Vodafone na Vodacom kwenda kuzindua rasmi mradi wa mifugo wenye thamani ya Sh Milioni 12 kwa ajili ya kusaidia huduma za watoto yatima wa kituo cha Yatima Trust Fund cha chamanzi mbagala.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodafone barani Ulaya na Africa Morten Lundal (katikati) akimwelekeza kuandika mmoja wa watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Yatima Group Trust Fund Izack Lubanza(kushoto)wakati walipoenda kuzindua mradi wa mifugo wenye thamani ya Sh Milioni 12 kwa ajili ya kusaidia huduma za watoto yatima wa kituo hicho.(kulia) Mkurugenzi wa mahusiano wa mambo ya nje wa Vodafone Matthew Kirk
Mlezi wa kituo cha Yatima Group Trust Fund Winfreda Rubanje(kushoto)akiwaelekeza mazingira ya kituo hicho Afisa Mkuu wa mahusiano ya kibiashara wa Vodacom group Bob Collymore(katikati) Mkurugenzi wa mahusiano wa mambo ya nje wa Vodafone Matthew Kirk(kulia)Walipoenda kuzindua mradi wa mifugo wenye thamani wa Sh Milioni 12 kwa ajili ya kusaidia huduma za watoto yatima wa kituo hicho.
Mkurugenzi mahusiano wa mambo ya nje wa Vodafone Matthew Kirk akipata maelekezo kutoka kwa Meneja wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule kuhusiana na Mradi wa Mifugo wenye thamani ya shilingi Milioni 12 kwa ajili ya kusaidia kituo cha Yatima Group Trust Fund chamanzi mbagala.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. dont send these kids to a mine field please!

    ReplyDelete
  2. huyo mzungu ukimwambia huo ni mlima kilimanjaro atakupa ela ya kuupanda

    ReplyDelete
  3. vodacom imekuwa ikiisaidia jamii kila mara. Kuna uwezekano makapuni mengine yanafanya hivi ila hatupati taarifa, lakini kwa kweli vodacom imekuwa mstari wa mbele. Hawa ndio wawekezaji wanaoijali jamii yao maana jamii ndio wateja. Wawekezaji wa nyanja zingine kama madini wanatakiwa kuiga mfano huu!

    Go voda go!!

    Mdau wa Juu

    ReplyDelete
  4. humo uchochoroni waangalie wasijelipuliwa na mabomu yaliojificha!

    ReplyDelete
  5. I would like to congratulate Vodacom Foundation for the huge humanitarian effort they're contributing to Tanzania as a whole. They have managed to diversify their humanitarian portfolio to cover all areas of the community that really do need a helping hand. It seems like everywhere you turn, if help is needed, vodacom are there with a helping hand. Congratulations Mwamvita Makamba on the exceptional work that you are doing. Congrats to vodacome for giving back to the community, people will say you ahve ulterior motives, but atleast the people who really need help, get it.

    Mdau T-Dot

    ReplyDelete
  6. kaka michuzi natoka nje ya mada. kuna hii habari nimeisoma kwenye blog ya TMZ kuwa Jessica Biel na Isabel Lucas wataenda kupanda mlima Kilimanjaro mwezi wa kwanza mwakani. naweka hii link yenye maelezo zaidi..sijui kama wizara yetu ya utalii ina hizi habari..
    http://www.tmz.com/2009/09/24/broadback-mountain-biel-to-mount-kilimanjaro

    ReplyDelete
  7. Swali la kimbeya and apology - is Mwamvita Makamba the daughter of Lt Col Makamba?

    ReplyDelete
  8. hivi ni kwa nini hata kama hoja ni ya muhimu sana kina mashaka huwa hawachangiagi maoni?? lakini wao hutoa hoja zao ndeeefu na wadau tunachangia kwa wingi au mnajiona nyie ni watu flani bora sana acheni hizo kama ni hivyo msiwe mnatoa hoja zenu humu then msubiri wadau watoe maoni

    ReplyDelete
  9. Mifugo gani wametolewa?

    ReplyDelete
  10. mdau wala hilo sio swali la kimbea ni kutaka kufahamu tu ni kweli kabisaa mwamvita makamba ni binti wa luteni yusuph makamba na wanafanana pia

    ReplyDelete
  11. MWAMVITA WEYE MBONA WAPIGA PICHA MBALI ATI, MIE NTAKA KUJUA KAMA UMEOLEWA AU BADO YAKHE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...