mama wa mitindo asia idarous-khamsin akikata keki wakati wa sherehe za besdei ya 50 ya kuzaliwa kwake akisaidiwa na mustafa hassanali na kushangiliwa na shemeji zake na waalikwa kwengine usiku wa kuamkia leo hoteli ya regency jijini dar
ally rhemtullah akimtuza asia shada la maua asia akiwa na kikosi kazi chake cha fabak fashions
asia akipozi na baadhi ya waalikwa
asia na marafiki wakila pozi
asia akimkabidhi hadija mwanamboka zawadi kwa ajili ya watoto yatika
asia akitoa zawadi ya nguo za shule 100 kwa ajili ya wasichana wanaosaidiwa na taasisi ya somesha mtoto wa kike
asia akipokea zawadi toka kwa mumewe bw. khamsin aliyeko marekani

mapema asia na ankal walipeleka misaada ya nguo
kwa watoto yatima katika kituo chao sehemu za kigogo jijini dar
asia na ankal wakigawa nguo kwa watoto yatima kigogo ikiwa ni mojawapo ya maadhimisho ya miaka 50 ya kuzaliwa kwa mama huyo wa mitindo.
Picha zingine

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Uncle hao watoto yatima ni WAISLAM tu au kuna WAKRISTO pia ila waliamua kuvaa hizo hijab tu!.
    Sisemi kwa swala la udini ila mi nilidhani uyatima wa watoto hauchagui dini wala kabila, au hicho ktuo nicha taasisi ya dini ya kiislam.
    Waosha vinya karibuni.
    Mjumbe.

    ReplyDelete
  2. mikristo bana,kitu kidogo tu wataanza zao,hivi mbona waislam wa nchi hawa jamaa wanatuzidi akili hivi,cia fact zinaonesha waislam wamewazidi wakiristo nchi hii kwa asilimia 7 lakini bado wanataka waifanye nchi yao wenyewe,mbona jana magufuli katoa samaki kwa vituo vya yatima vya kanisa peke yake lakini waislam tumechukulia poa tu,hatujapiga kelele,maana tunaamini hii ni nchi yetu sote,lakini nyie kitu kidogo kelele,kuna vyeo nchi hii tangu tz ipate uhuru waislam hawajawahi kuvishika,kama jaji mkuu,mkuu wa majeshi na vyengine vingi lakini hatulii,nyie kitu kidogo kelele,2010 tunataka nusu kwa nusu,kama mawaziri 30,basi 15 kwa kila dini,maana tumeshaanza kuchoka sasa.mmezidi na mkimuamsha alolala mtalala nyie.

    ReplyDelete
  3. Kwa miaka 50,bado Asia anadai.

    ReplyDelete
  4. mdau hapo juu acha jazba,mjibu tu vizuri huyo mtu utakuwa umemsaidia kuondoa udini

    ReplyDelete
  5. Happy Birthday Asia! Dada unaonekana bado kijana sana like years old. Tueleze nini siri ya kuonekana that young wakati unagonga 50!

    ReplyDelete
  6. anon fri dec25,12:39:00pm jaribu kuwa na utafiti kidogo sio kuropoka tu,mfano hao samaki wamegawiwa kwa taasisi nyingi tu ikiwemo jeshi,polisi,muhimbili,udsm na vituo vya yatima bila kujali dini, ila taasisi nyingi zimekataa kwa kukosa sehemu ya kuhifadhi kwani wamepewa tons sio kilo mbili,imagine hiki kituo tunachokiona kina freezer ya kuhifadhi ton mbili??hakuna udini mdau kauliza tu,na jibu ni ndio hicho kituo ni cha kiislm tu kama ambavyo vingine ni vya kikristo tu,ambavyo havina dini vinamilikiwa na serikali au ngos.

    ReplyDelete
  7. Fri Dec 25, 12:39:00 PM taifa lina mzigo mzito sana, anon wa kwanza umeuliza swali lenye akili sana na Fri Dec 25, 02:41:00 PM umejibu vizuri sana hata mimi nilikuwa sifahamu

    ReplyDelete
  8. Naomba kuuliza huyo mdau aliye sema waislamu wamewazidi wakristo kwa 7% hiyo sensa aimeifanyia wapi na lini? naomba anieleza Tanzania waislamu, wakristo na wasio na dini ni asilimia ngapi kila kundi?

    ReplyDelete
  9. Mtowa maoni wa kwanza na wapili hapa nina wasiwasi kama kweli mnaujuwa huo ukiristo kwani ndani ya Bible imesema kuwa mwamke afunike kichwa chake na kama hataki kufanya hivyo zikatwe nenda kaisome Bible ulikuta hilo.

    from Jabiri Muhidin

    ReplyDelete
  10. "HEPI BETHIDEI BI ASIA KHAMSINI"

    Hongera shemeji kwa kutimiza miaka 50 nimefurahishwa kwa umri wako ukiwa bado unapendeza,mfano mzuri kwa wabunifu,wanamitindo wa kizazi kipya kufuatilizia nyayo zako katika fani ya mitindo na moyo mzito wa kusaidia wasiojiweza kwa kiwango cha hali ya juu bila ya kujali rangi au madhehebu ya dini zao.
    Natukutakia kila la kheri
    Mickey Jones-Denmark

    ReplyDelete
  11. wewe mtuma maoni wa kwanza kama unaone hicho ni kituo cha taasisi ya kiislam, kwani si kueka chako cha kikafiri tu.

    ReplyDelete
  12. Nitaendelea kuwa Anonymous,niliuliza swali mwanzo kabisa kuhusu uncle wa globu ya JAMII kuonekana akitoa misaada kwenye kituo cha watoto yatima wa KIISLAM.Sio siri kwamba kila mwenyedini yake anahisia zake lakini ukionekana kupendelea upande mmmoja hasa katika JAMII nikuionyesha JAMII kwamba kunaupande usioujali. Sasa uncle ni kweli kwamba haujali yatima wa-KIKRISTO?.Nadhani ingependeza kama mgegawa nusu ya zawadi hizo ili kuonyesha usawa katika JAMII.Au nawewe umeamua kuonyesha hisia zako uncle?
    Ungemtafuta Mwavita Makamba akuonyeshe zilipo na MADRASA anakotoa zawadi za majuzuu kila kukicha kupitia Vodacom-foundation,ili tujue msimamo wako kidini bila kutuzuga na jina zuuri eti BLOG YA JAMII.
    JAMII inaweza isiwe na watu wanaoelewa tu kama wewe na huyo mwenye sensa za CIA,JAMII inawatu kama sisi tusioelewa au kujua kubalance mambo, inaweza ikawa ni waislam au wakristo au wasioamini mungu lakini tukaendelea kubalance mambo na tukaishi au kuona kama JAMII.Itikadi za makundi bila kujali udugu, ukabila, jinsia, utaifa,ama udini ndizo zinaweza kutufanya tuishi kwa kujiita wana-JAMII si wana-JAMII.Ndio tunaweza kuwa wana-JAMII tukiwa na tofauti zetu lakini bila kuzionyesha mbele ya yale makundi tunayoyatumikia yenye itikadi tofauti. kwaneno moja tunaita UBAGUZI.
    USHAURI-Unapoamua kuitumikia JAMII ama kwa ihari au kwa ulazima wake unatakiwa kutojihusisha na itikadi ya kibaguzi. ukiweza kutoa misaada ya juzuu na mitandio wakati wa sikukuu za kiislam, basi ikifika za kikristo fanya hivyo pia,lakini usionyeshe adhara kwamba una upande unaouzidi mwingine katiak misaada yako,tulidani wakati wa sikukuzile za kiislam ilikuwa ni season yake lakini tunapitiliza sasa,ukichukizwa na hili ama Acha kabisa au jirekebishe au sema adharani pia JAMII ijue hilo pia, nikatika kubalance mambo. ni mtizamo tu na tusitafutane kama anavyosema Ney wa Mitego katika wimbo wake unaweza kuupata kupitia YOUTUBE. unaitwa ITAFAHAMIKA.
    Waosha vinywa karibuni ila sasa hivi tungeomba na data za FBI, au hata za hapa kwetu toka kwa ,SAID MWEMA,MANUMBA,Chikawe,AG na HATA waziri MASHA.
    Asanteni.

    ReplyDelete
  13. We Da Asia...mbona umeninyima mwenzio hiyo keki..... Haya bwana..
    Anyways Happy Birthday Bi dada!!! InshaAllah ufike mara mbili ya hamsini au 'Khamsini' -My hazbendi wako!...but mind you upendeze hivyo hivyo... much love, Belinda.
    Huyo MC..kaanza lini hiyo kazi? mwambie anipigie na mmiss sana ..namba anyo..dadie belinda,

    ReplyDelete
  14. Anonymous wa kwanza naona baada ya kupewa data za idadi ya Waislamu na Wakristo ukaamua u-guugo sio kupata uhakika...Kwa taarifa yako hizo data ulizoziona za CIA ndizo zinatambulika kimataifa na hata hao uliosema waulizwe wanatumia hizo hizo... Hapa hakuna ubaguzi, leo wanatoa miasaada huko kesho wanatoa kule... ASANTENI.

    ReplyDelete
  15. Wacheni kumsakama Michuzi, Michuzi si yeye aliyetoa zawadi hizo, yeye kakaribishwa tu na Bi Asia, na Bi Asia kwa kuwa ni Muislamu, mapenzi yake yamemtuma kutoa zawadi katika kituo cha yatima cha kiislamu! Tatizo liko wapi mdau wa kwanza??? Mbona waleta Udini tena katika 'globu' ya jamii??? Ankal yuko huru kwenda popote wadau wakimualika kwenda, mara ngapi ameripoti habari tena akiwa ndani ya kanisa??? Acheni hizo.
    Wasalamu.
    Mdau Uholanzi.

    ReplyDelete
  16. acheni kuita wenzenu makafiri kila mtu na imani yake kafiri ni wewe na ukoo wako! tena ukome

    ReplyDelete
  17. KAZI KWELI KWELI Watu wanacomment utadhani wako Mirembe....WAAMBIENI HAO WAKRISTO NA WAO WAKITOA MISAADA WAMUALIKE ANKO ISSA MICHUZI HALAFU ISSA AKIKATAA NDO MJE MUONGEE HIZO PUMBA....Kwahiyo maelezo yenu ni kwamba akialikwa kwenye shughuli ya kidini asiende?? au asilete habari?? nyie ni watu wa ajabu.....ANKO ISSA MIE NATAKA HIZO CONTACT ZA HICHO KITUO NAOMBA USINIANGUSHE KWA HILI...AU KAMA KUNA MDAU PIA ANAEJUA CONTACT ZAO AANDIKE HAPO CHINI....

    ReplyDelete
  18. dohooo anatishaa jamani fide si mchezo mwambieni walokaribu nae.maaana balaa tupu yaaani

    mdau den haag

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...