JK akiwa na Ruge Mutahaba wakati wa shoo ya THT jijini Dar karibuni
SWALI: Ruge mutahaba ni nani?

RUGE: Nimezaliwa Brooklyn New York Marekani mwaka 1970, Primary School nimesoma Arusha School standard 1 hadi 6, kisha nikahamia Mlimani Primary School maeneo ya Chuo Kikuu Dar es Salaam na ndipo nilipomaliza darasa la saba. Kisha nikasoma Forodhani Secondary School form 1 – 4, baadae Pugu High School 5 na 6. baada ya hapo nikarudi Marekani ambako nikaenda kusoma San Jose University California ambako nikachukua BA in Marketing na pia nikawa nakachukua BA in Finance, kozi zote nilisoma ndani ya miaka 5, kind of 2 courses at the same time. Baada ya hapo nikarudi tena Tanzania.

SWALI: Nini kilichotokea hadi ukajikuta uko cloudz FM.

RUGE: Wakati nipo Marekani, Joseph Kusaga alikuwa na disco, Clouds Disco, mimi nikawa supplier wake wa vifaa mbalimbali vya music, then hapo tuka-build good friendship. Sasa, niliporudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yangu, Joseph Kusaga akanishawishi sana nibaki kutokana na opportunity zilizokuwepo za kuanzisha Radio na kuipeleka katika level nyingine kabisa, ndipo nilipojikuta nipo Clouds Entertainment.

SWALI: Tuambie kuhusu THT.
RUGE: Kama Clouds Entertainment tuliamua kuanzisha kampuni ya management ya wasanii ambayo tuliita Smooth Vibes ambayo ndiyo kampuni iliyowatoa wanamuziki kama Lady Jay Dee, Ray C na wengineo. Unajua utakuta kati ya wasanii watano, only mmoja au wawili wana-survive na suddenly utakuta msanii alikuwepo then kapotea. Hii inatokana na kutokuwa na foundation nzuri. Hivyo nikaona ni bora nianzishe House of Talents ambayo sasa kupitia hiyo, tukawa tunawafundisha wasanii misingi ya muziki, kumfundisha msanii how to Manage Industry, Vocal Coaching, Music Business, Music Instrumentation, Dance Classes na kadhalika.
Nikagundua kuwa unakuta msanii anaenda kwenye show lakini performance inakuwa mbovu na pia ili msanii aweze ku-last longer kwenye game anatakiwa ajue dancing. Ndio maana THT tukawa na dance classes. THT imewatoa wasanii wengi kama Maunda Zorro, Mwasiti, Marlaw, Barnaba na wengineo. THT hadi sasa ina miaka minne.

Kupata intavyuu nzima



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. bla bla blaaa....utawa-coach vp watu mziki wakati wee mwenyewe hujasomea mziki??

    ReplyDelete
  2. mjomba siuchague lugha moja aaah lkn sawa jina lake ni Ruge mutahaba

    kamugisha,senior staff/coventry

    ReplyDelete
  3. sawa kabisa ila hapo uko na jk kwenye picha koti la suti kuubwa lol

    ReplyDelete
  4. Vijamaa kama hivi ndivyo vinavyostahili post za uwaziri jameni

    ReplyDelete
  5. Papaa Ruge mbona hutaji Mazengo bwana wakati tumekula wote bondo pale ukiwa form five kabla ya kuhamia Pugu ?

    Huyu jamaa soka pia lipo sana mguuni basi tu ubraza...!!

    ReplyDelete
  6. Good interview! Well done Ruge; we are proud of you. Keep up the good work
    Mdau, DC

    ReplyDelete
  7. Ruge is a role model. Licha ya mafanikio na kufuatwa sana na mademu wanaotaka msaada, bado hajaingia kwenye kashfa. Hata Zeutamu haikuwahi kumwandika chocote. Big up mjasiliamali, waonyeshe wote wanao wakandia Wahaya kuwa vijana wa Kihaya wana tabia worth being role models. Big up Rugemalira.

    Mdau, BK

    ReplyDelete
  8. mdau bk umekuja lini mjoni? , uliza uambiwe. ruge form six tu lakini zamani tayari ana ...

    ReplyDelete
  9. Ruge mimi nakupongeza sana kwa juhudi zako.


    (US Blogger)

    ReplyDelete
  10. Are u Single RUGE?natafuta mchumba

    ReplyDelete
  11. KUOA LINI BEST ??

    ReplyDelete
  12. atera 2 positions at the same time. Mwenu this guy is fantastic

    ReplyDelete
  13. kalembee

    nilitaka kushangaa MUHAYA asiongee/kuandika ivo apo juu

    shomile waitu,,,

    ReplyDelete
  14. Jitahidi THT iwe na mfumo imara wa kujiendesha ili iwe endelevuuu..

    Ni juhudi nzuri, BIG UP.

    ReplyDelete
  15. Jitahidi THT iwe na mfumo imara wa kujiendesha ili iwe endelevuuu..

    Ni juhudi nzuri, BIG UP.

    ReplyDelete
  16. Watanzania inabidi tubadilike, kama anafanya vizuri katika game apewe sifa yake, hayo mengine ni maisha yake binafsi hayakuhusu wewe wala mimi, mambo ya kuwa toka form six tayari .. yanatoka wapi au ni wivu tu??? Keep up Bro achana na haters hawana mpango.

    ReplyDelete
  17. Kama umezaliwa Marekani unapewa uraia wao moja kwa moja, yaani automatic. Je, ameukana uraia wa Tanzania au wa Marekani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...