Jukwaa la upande wa yanga
upande wa simba
kocha wa yanga kostadi Clinton akiwa kabebwa na mashabiki kwa kuiwezesha timu yao kuwashinda watani wa jadi leo
Timu ya Yanga a.k.a Watoto wa Jangwani imetoa zawadi nono ya Xmass kwa wapenzi wake kwa kumbanjua mtani wake wa jadi Simba kwa bao 2-1 kwenye nusu fainali za kombe la Tusker Cup.Alikuwa ni Jerry Tegete aliyeweka chuma kimiani zikiwa zimebaki dakika tatu kabla ya muda wa dakika 120 kumalizika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. Yule Boban anatuaibisha na ushamba wake wa "TABORA" sasa ndio kafanya nini? tuwache "UNAZI" leo Yanga wametutandazia mpira "REFA" katubeba tumeshindwa kubebeka ila "SIMBA" bado ni "TAIFA KUBWA" hongereni yANGA tunawatakia ushindi mbele. MWANA WA MSIMBAZI.

    ReplyDelete
  2. Ummetufarahisha watoto wa JK au wajangwani au watoto wa manji na bado kwenye ligi tuue tena mnyama YANGA...OYEEEEEEEEEEE X-MASS TUTAILA VIZURI asante clinton wetu na wachezaji wote na viongozi kwa ushindi wa leo.....

    ReplyDelete
  3. angalu yanga mmetupa raha maana hata maji tulikuwa hatumwi leo siku nzima nilikuwa nawaza tu jinsi nitakavyotaniwa

    ReplyDelete
  4. yaaan we hacha tu dalali,kaduguda chali yanga safi sanaaaaaaaaaaaana
    bado hao paka fro nbo.ahsante misoup

    ReplyDelete
  5. Tunashukuru sana vijana kwa kutupa zawadi nzuri ya X-MAS! X-MAS Isingeweza kwenda bila NYAMA sasa kutuchinjia hiyo nyama ya PORINI, hakika tutafurahi sana KESHO!

    Poleni sana watani zetu, mkumbuke huu ndo mpira.
    Mdau wa Jangwani

    ReplyDelete
  6. Asanteni sana vijana wa Jangwani! What a victory?... Absolutely fantastic!!! Christmas njema wana-Simba!

    ReplyDelete
  7. yanga daima na hilo komber linakwenda jangwani

    ReplyDelete
  8. Mzee wa misupu, Unajua xmass zote kitoweo lazima iwe Nyama ya kuku, ng'ombe, mbuzi nakadhalika. Lakini nimefurahi sana kuwa xmass ya safari hii kitoweo ni kipya kabisa kuanzia asubuhi supu, mchana pilatooo na jioni dina la mchana ni nyama ya Simba. Uwindaji wa wana wa jangwani umenifurahisha sana leo hureeeeeeeeeee TEGETE. Ila sina budi kuwakaribisha watani zangu wa jadi pale msimbazi wote karibuni sana. Na pia nawatakia watanzania wote xmass njema na mwaka mpya wenye mafanikio katika maisha yenu na Taifa letu kwa ujumla.

    ReplyDelete
  9. red card ya haruna moshi imeicost timu. jamaa walitawala gemu after the dismissal of that teja.thats why maximo hampangi hamtaki

    ReplyDelete
  10. mkubwa una tisha uko up 2 datE sana dats gud broo nice Holday man,

    ReplyDelete
  11. Haruna Moshi si alikuwa Ulaya,vp tena karudi Bongo?

    ReplyDelete
  12. wajinga hao yaani kila siku wao wakitufunga sawa si tukiwaonja tu kitu tu ni noma.LMAO all the simba sports clubs fans

    ReplyDelete
  13. yanga oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.perfect christmass present

    ReplyDelete
  14. asiyekubali kushindwa si mpinzani,roho inaniuma sana ila ndo mchezo..kila la kheri yanga

    ReplyDelete
  15. katika siku ambazo Yanga mmenifurahisha ni leo, yaani nimepigwa sana na baridi na haya mabarafu ya ughaibuni ila nilipopata simu kuwa mmeibanjua simba 2-1 yaani hata baridi sikuisikia tena nilijikuta nakimbia kama chizi huku niko kifua wazi mpaka niliposhtuka nimelowa kwa mvua na baridi ilikuwa kali mno. yaani hata msipochukua kombe lakini mmenipa usingizi wa xmass maana tangu asubuhi maji yalikuwa na chumvi kama sio siki na limao ila sasa hivi matamu kama asali. yaani kesho nitapika pilau mchele utakuwa wa kuhesabu bali nyama za kumwaga walau nijisikie namla mnyama wa msimbazi. Yanga idumu juu milele. watani poleni sana, hizo ndio dalili kuwa mwaka 2010 mtauanza kwa kufungwa yaani ushindi kwenu utakuwa ndoto

    ReplyDelete
  16. KIPIGO HIKI KIMENIFURAHISHA SANA MPAKA NIKAJIKUTUKA NAKUMBUKA RAFIKI ZANGU WA MOROGORO WAKINA BEDA MSIMBE, CRESTUS MAGORI, FANCIS NG'ATIGWA, MWANANZINGE, MAGODA HAWA WALIKUWA WPENZI WAKUBWA WA SIMBA- NAJUA POPOTE WALIPO DUNIANI WATAKUWA KILIO NA SIMANZI KRISMAS YAO BARIDI KWELI KWELI; POLENI WANZAI WA SIMBA NA RAFIKI ZAO

    ReplyDelete
  17. jamani mimi nadhani nitakuwa na uchungu kuliko wote maana nilihaidi kuwa Yanga akishinda nitakata mkono wangu.uuuwwwi sitaki tena ushabiki

    ReplyDelete
  18. Ehhh Simba koko kauliwa poa sana wanachonga sana hao.Bado ktk ligi. heti Phiri hawezi kufungwa na Yanga yako wapi sasa. Au sio Phiri tena ni Piri? Xmass njema Yanga oyeeeeeee

    ReplyDelete
  19. Basi tena, kombe limeenda Kenya.

    ReplyDelete
  20. Yaani Hawa Leo Wetu Full Hata wangetufunga Tunamlilia Boban Tu Maana Kashasajiliwa Ulaya Habari Tunazo..Yanga Oyeeeeeee

    ReplyDelete
  21. Yaani Yangaa mmenipa furaha na zawadi ya xmas. Tuendeleze goma

    ReplyDelete
  22. chuji + kaseja + boban = Jamaica

    who is wanderin boban to get redcard?

    ReplyDelete
  23. Nliona mechi tangu filimbi ya kwanza hadi ya mwisho Simba haikucheza vizuri kipindi cha kwanza, makosa yalikua mengi sana angalau Phiri alipomtoa Santo na kumuingiza Chombo kiungo kilichangamka,japo Banka hakuwa kiwango. Yanga wangeweza kufunga mapema kipindi cha kwanza kama si kutokua makini kwa foward wake Jerry Tegete na Ngasa ambao mara nyingi walipata nafasi za wazi ndani ya eighteen yards wakashindwa kufunga. Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kuamka na kuanza kusukuma mashambulizi mazito kuelekea lango la yanga hadi kupelekea kuumia kwa kipa wake toka Ghana ambaye aligongana na Mgosi wakigombea mpira wa juu alioupangu kufuatia shuti kali tika kwa Mgosi pembezoni mwa uwanja. Kuumia kwa kipa huyo kulimpa nafasi Obren kuingia na pia kufanya kile alichokia kipa mwenzie lakini kwa mara nyingine tena kutokua makini kwa wachezaji wa Simba kutoa pasi kwa wakati ndani ya box kuliighalimu timu hiyo bao la kuongoza. Presha ya kutafuta goli iliwasahaulisha Simba majukumu yao defensively na hapo Yanga ikaamka na kupiga shambulizi moja la nguvu lililozaa bao la kuongoza. Kufuatia bao hilo Simba ilijipanga na kurudi tena na presha ya kutafuta bao na kufuatia makosa yaliyofanywa na golikipa Obren kupiga fyongo mpira aliodaka na kuishia kwa Simba huku defense ya Yanga ikiwa imesogea kati Simba waliounasa mpira uliopigwa hovyo toka kwa Obren ilipigwa through ball na Echessa pasi iliyoikata defence ya Yanga na mpira kumfikia .... aliyekua udokoa mpira kumpita kipa lakini kipa akamwangusha na refa kuamuru ipigwe penalti( swali ni kwanini kipa hakupata kadi yoyote kwa kosa la kumwangusha mchezaji kwenye box? Ask Mr. Referee).Penalti ilifungwa na Echessa kuisawazishia Simba bao. Simba nusura waandike bao la pili lakini shuti kali la mkenya Barasa lilipanguliwa na Obren. Hadi mwisho Yanga 1-1 Simba. Kwakua ni lazima afungwe mtu zikaongezwa dakika 30. dakika zilizoshuhudia Simba kumpoteza Haruna Moshi kwa kadi nyekundu kutokana na kuhoji kwa nini line man haflag any infringement directed to him by Yanga defenders,kwni mara tatu katika vipindi tofauti alikua akihoji kutolindwa anapomiliki mpira na beki kutaka kuunyanganya kwa kutoka nyuma.,na hadi nyakati fulani alichezewa rafu na Maftah akaacha mpira na kutaka kumwuliza lineman aliyekua hatua tatu toka eneo la tukio lakini refa aliyekua mbali aliona ile faulo na kuamuru ipigwe faulo kuelekea Yanga. Kutoka kwa Boban na kuumia kwa Okwi kuliigharimu Simba kwani sasa Yanga ikawa na numerical advantage na na kidogo iwagharimu kwani walianza kucheza bila umakini na kufurahisha mashabiki kwa pasi za hapa na pale nyingine zisizokua na umuhimu na hapo ndipo Simba walipo "sniff" kama waweza kufunga goli, hivyo walianza kusukuma mashambulizi bila tahadhari kwenye "backline" yao, kwani mpira aliouchukua Yondani toka nyuma alipanda nao mbele upande wakulia alipotaka kumpiga chenga Ngasa,Ngasa akaunasa na kuusogeza hatua tatu mbele. Yondani alipogeuka akamkuta Ngasa kishaanzisha safari! Bwana Yongani sijui ni misuli au kuchoka akajitupa sakafuni na kubariki safari ya Ngasa. Ngasa akasogea apiga low cross iliyomkuta Tegete ndani ya box with time and space.Naye kwa utulivu akapasia nyavu Yanga 2-1 Simba game over Fulaha jangwani msiba Msimbazi
    Hitimisho ni kwamba Chuji, Nsajigwa,Mgosi, Ngasa walistahili kupewa kadi nyekundu mechi ile
    Nsajigwa..ye alimpigwa kiwiko Mgosi na kumtoa nje, alikua overreact kufuatia Mgosi kumpiga kipepsi kipa wa Yanga
    Mgosi ..ye alimpiga kipepsi golikipa wa Yanga
    Ngasa ..aimkwatua Yondani ikiwa ni off the ball incident ambayo kama line man angeiona na kumtaarifu refa basi ilikua ni straight red
    Chuji ..kuwakamia wachezaji wa Simba kwani mara mbili aliwakanyaga Banka na Haruna kwa makusudi na tukio moja la kumkanyaga Haruna lilionekana na refa akampa kadi ya njano Chuji na kuamuru ipigwe faulo.
    Mnamuonea Maximo hawa wachezaji hawajui kujiheshimu ndani ya mchezo ndio maana walimiminiwa kadi kwenye Chalenji ila kwa soka ya bongo kuna kulindana sana.
    Chrismas Njema!

    ReplyDelete
  24. BOra tumefungwa maana hasira za mashabiki wa Yanga kufungwa ni fedheha kwa taifa. Maana hawakawii kukujoa kwenye masinki.

    Tumewapa mfano wa kujifunza kufungwa ni mchezo. Mbona hamna picha za masinki kukujolewa wala mabomba na vitu kuibiwa hapo uwanjani. Ikibidi tuwaachie kila siku ili tusifedheheke.

    ReplyDelete
  25. TANZANIA KWELI KUNA WATU HATARI KAMA ANONY Tarehe Fri Dec 25, 03:35:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous YAANI SIJUI NI MSHAMNBA WA WAPI YEYE YAANI KILA KOSA LA KIPA NI KADI NYEKUNDU! DUUH ACHA UNAZI KAKA. WATU KAMA NINYI NDIO TUNAWATAKA TUNAJUA INAKUUMA SANA KUFUNGWA NA NDIO FURAHA YETU KUKUONA UNATAKA KULIA ETI KADI NYEKUNDU ZOTE HIZO YAANI KAMA TANO? WEWE USIJIFANYE UNAJUA BOBAN KATOLEWA KWA SABABU GANI HAUKUWAPO KARIBU KAMA ALITUKANA JE?
    TENA JAMNA MNGEPIGWA HATA SITA. INASHANGAZA KUONA WACHEZAJI NA VIONGOZI WA SIMBA WAMEKUBALI KIPIGO NA KUISIFU YANGA YEYE ANAKALIA KUPINGA KUWA WALIONEWA. LABDA MWENZETU MACHO YAKO YAKO NYUMA!!! JUA KUWA WEWE MPENZI WA SIMBA UNAPOKUWA HUNA RAHA NDIO FURAHA YETU YANGA.

    ReplyDelete
  26. kama kawaida ya mashabiki wa yanga huyo kocha anvyobebwa kama simu ipo mfuko wa nyuma ndio ivyo tena Manji ajitaarishe kununa nyingine. LOL

    ReplyDelete
  27. Hongereni Yanga.Pia Simba tunashukuru mpira ulikuwa wa upinzani sana.Ingawa tumefungwa lakini kiwango bado kipo palepale.Yaani sisi bado ni taifa kubwa.Ushauri kwa Yanga bakizeni kombe basi lisije kwenda Kenya.
    Bado naipenda Simba kwa moyo wangu wote,hata leo watu walinishangaa sana nilivyokuwa nimevaa jezi ya Okwi hapa Bagamoyo.
    Tunaomba Kombe libaki Tz.
    Ni mimi,
    Shabiki wa kweli wa Simba.

    ReplyDelete
  28. Yanga oyee,na bado tumeshafungulia fuko la gundu, yaani ile pyee na majimaji simba inaloa tena. Ila annoni wa Fri Dec 25, 03:35:00 PM kanifurahisha na kauchambuzi kake jamaa anaonekana live ni shabiki wa Simba lakini kajitahidi sana kuongea ukweli.Tathmini yake ni nzuri nimeipenda. Ni kweli simba tungewafunga mengi lakini Yanga hatukua makini kwenye umaliziaji yaani laiti Ambani angekua kwenye kiwango ingekua balaa.Haruna ili umpunguze kasi we piga buti tu lazima atalizua..hahahaaaaa

    ReplyDelete
  29. We Anon wa frid DEc 25, 03:35:00pm acha kuchambua mpira kinazi we unajua alichotamka Haruna kwa yule mwamuzi?
    Isitoshe nani kakwambia kwamba timu ikipungiwa na mtu ndo inafungwa mbona mechi iliyopita mlishinda mkiwa pungufu,mbona mwaka juzi kwenye mechi yenu na polisi Dodoma mlitoka sare 2-2 wakati polisi walikuwa pungufu wachezaji wawili acha unazi wa mitaani kama wa Clifford Ndimbo eti oooh kundi letu ndilo lilikuwa gumu la mabingwa oooh Yanga wameifunga mafunzo timu dhaifu wakati juzi tu tumeshuhudia Zanzibar heroes wakiifunga Kilimanjaro stars, mpira hauko hivyo ili mradi mko kwenye mashindano mamoja basi tafsiri ni kwamba timu zote zina uwezo sawa waulize wafaransa walifanywa nini na senegal.
    Ukweli wa mambo uko wazi Yanga siku ile ilkuwa kwenye form ukilinganisha na simba

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...