Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Pius Msekwa akiwahutubia vijana jana mjini Dodoma leo juu ya umuhimu wa kushikamana na kujenga umoja wakati wanaelekea katika Uchaguzi Mkuu, mara baada ya kuwasimika Makamanda wa UVCCM wa wilaya zote za Dodoma na Mkoa katika Sherehe zilizofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Taifa mjini Dodoma.
Makamanda wa CCM wa wilaya na Mkoa wa Dodoma. Toka kulia kwenda shoto ni Mh. Hezekiah Chibunje,huyo ni Kamanda wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, anyefuata ni Mh. Zabein Mhita yeye ni Kamanda wa UVCCM Kondoa Kaskazini, Mh. Job Ndugai, Kamanda wa UVCCM Kongwa na Mh. Laurent Hoya yeye anakuwa Kamanda wa UVCCM Chamwino.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. HUU NI UKAMANDA WA KITU GANI? JAMANI WATU BADO WANA ZILE MENTALITY ZA ZAMA ZA CHAMA KIMOJA..JE KUWA KAMANDA INA UMUHIMU GANI KWA WATANZANIA?

    ReplyDelete
  2. Hivi kwa nini kila mara unapokuwa ni mwaka wa uchaguzi, UVCCM huteua makamanda wao tena ambao ni wabunge waliopo au wale wanaoutafuta ubunge. Jambo hili huwa linaleta mtafaruku ndani ya CCM kuliko. Hivi ina maana mtu unaechaguliwa kuwa Kamanda ni automatic utapigiwa kura ya maoni ya kuwa mgombea kwa niaba ya CCM? Tumeshuhudia juzi juzi wakati mbunge wa Arumeru Magharibi Mhe Elisa Mollel alipoachwa kuchaguliwa kuwa Kamanda alivyosababisha vaga kwa vile aliyechaguliwa Ndugu Mideye kaonyesha nia ya kugombea ubunge.Nini hii

    ReplyDelete
  3. sasa huu ukamanda tena wa kazi gani jamani
    mbona mnataka kutuua njaa tu .kiru na mashisha!!! mimi nazani tanzania tupo hivi kwa sababu wote si ni wageni tumechanga nyika changanyika wazawa awakusoma adi leo wanacheza ngoma.humu ndani kuna wa south , wakongo, wanalawi ,wakenya, WA ZENCHI,WAKAMEROONI ,WAPOPO,.CHUKUA TAPIA ZA WATU WOTE AWA NDO SISI WA BONGO .HIYO NDO ROOTS ZA WAZEE WETU

    ReplyDelete
  4. Nawapongeza na ninawatakia heri viongozi na wanachama wote wa CCM. CCM ndiyo chama pekee Tanzania kinachotuunganisha watu wa makabila, rangi na dini zote TZ. Lakini lazima tuwe more serious katika kuitekeleza ilani yetu. Wapinzani wana haki ya kujieleza, lakini wameshindwa kupendekeza programu yako ya ujenzi; badala yake, kazi yao kutukana, uongo kujenga chuki na ku"whine and ramble". Mungu ibariki CCM. Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...