Habari yako kaka michuzi.
mimi ni Sakina. Shida yangu ni kiwanja maeneo ya kitunda au kigamboni, chenye gharama ya shilingi milioni 2 na nusu. Awali nilikuwa nawasiliana na mwenyeji wangu wa huko Dar akawa ananiambia viwanja kwa sasa ni kuanzia mil.5. Lakini nilipata tetesi kuwa sehem nilizozitaja naweza pata kwa bei nafuu kidogo.

Tafadhali wadau, yeyote mwenye kuweza
kunisaidia awasiliane na mimi kwa email yangu;
sakinaabd@yahoo.com
natanguliza shukrani zangu za dhati!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. milioni 2 na nusu ungeanzia biashara ya mkaa baba

    ReplyDelete
  2. Kwani biashara ya mkaa siyo biashara? Mtaji wa biashara ndogo ndogo ni kati ya $2000 na $4000. Kwahiyo, sh milioni mbili na nusu ni karibia na $2000. siyo pesa ndogo.

    ReplyDelete
  3. MBONA SIJAWAHI KUMSIKIA ALIKIBA AKIONGE AKIINGELEZA? KAMA KWELI YEYE NI SUPA STAA, INABIDI AFUATE NYAZO YA MR. BRUE

    ReplyDelete
  4. te te te millioni mbili na nusu???? Unatania wewe, kwanini usifungue bihashara ya kuuza dagaa??

    ReplyDelete
  5. anaemshauri huyo dada kuwa hiyo pesa yake akaanzie biashara ya mkaa sio fresh.yeye hakuomba ushauri wa biashara,anchotaka ni kiwanja..so kama hujui jinsi ya kumsaidia kaa kimya.isitoshe huyo anaeshauri hivyo bado anaishi nyumba ya kupanga,hadi lini?big up dada kwa mawazo endelevu soon najua utajenga.
    ninachoweza kumsaidia huyu dada ni kwamba kwa pesa uliyonayo kiwanja unapata but sio town.nenda maeneo ya pugu au g/mboto kunaitwa ulongoni.kama unataka kitunda,ongeza pesa ifike mil.3 nitakusaidia.

    ReplyDelete
  6. mwanzo mgumu utafika.

    ReplyDelete
  7. Usijisumbue dada yangu na kupoteza mda bure. 2.5m huwezi kupata. bei za kununua kwa wallio navyo ndio kama hiyo 5m, tena hapo umepata cha kujenga kibanda tu sio nyumba. Pole

    ReplyDelete
  8. DADA YANGU USISIKIE WATU WAMEJENGA NA WEWE UKAFURUKUTA TU NA KIMILIONI MBILI CHAKO.WEWE TANGU LINI UKASIKIA MJINI WANAUZA VIWANJA KWA BEI HIYO.HATA BUSTANI UPATI KWA PESA HIYO.MIMI NAKUSHAURI ENDELEA KUPANGA TU SI LAZIMA WOTE TUJENGE.TUKIJENGA WOTE SI HITAKUWA BALAA

    ReplyDelete
  9. Jamani wadau huko nyumbani na kwingineko tunapouliza mambo hapa barazani muwe mnajibu kile tulichouliza kwani huo ndio msaada tulioomba. Lakimo hii habari ya mtu anauliza bei ya kitu nyie mnaanza kuzungumzia kafanye sijui biashara ya mkaa, sijui dagaa mara visepe hata haileti picha nzuri. Cha kushangaza unakuta mtu kalipia internet café halafu anaishia kuleta michango ya mawazo ambayo ni michango mfu, jamani heshima hainunuliwi.
    Binafsi naumizwa na sana hii tabia. Unakuta mtu unaulizia kama nnchi au eneo Fulani kuna mtanzania mwenzako walau upate company hata kama hutamtegemea kwa chochote watu wanaanza kwanza huko unakokwenda hakula dili ili iweje? Mie ninayekqwenda si ninajua ninachofuata?
    Tuelimike jamani…tutakalia politiki tu wakati wenzetu wanachanja mbuga!
    Mdau ughaibuni!

    ReplyDelete
  10. KWANZA KUWA MWANGALIFU.KIGAMBONI ISHAUZWA KWA BUSH HAKIKISHA UNAUZIWA KIWANJA KILICHOPIMWA TU ZAIDI YA HAPO TAFUTA ENEO JINGINE USIJEINGIZWA MJINI.

    ReplyDelete
  11. DADA SAKINA KWA HIYO PESA YAKO USUBIRI VIWAJA VYA MRADI AU VYA SERIKALI AMBAVYO HUWA VINAGOMBEWA KAMA KITU GANI SIJUI. NAVYO HAVIUZWI SOKONI, UNASUBIRI WATANGAZE WAKISHAVIPIMA, KISHA UNACHUKUA FOMU, HALAFU UNASUBIRI SADAKA LAWE KUPATA AU KUKOSA, WATU WANA LOBBY KUNUNUA HIVYO VIWANJA KAMA ASSETS ILI WAUZE KWANI SIKU HIZI SHERIA INARUHUSU KUUZA VIWANJA.

    HUYO JAMAA YAKO AMEKWAMBIA UKWELI, TATIZO NYIE MLIO NJE YA NCHI MUDA WOTE MUNAONA MNAIBIWA TU HAMUAMINI WATU, KWELI WENGINE SIO WAADILIFU, TENA HIYO BEI ALIYOSEMA JAMAA YAKO YA 5M UTAPATA KIWANJA KILICHOPIMWA LAKINI KUANZIA HIGH DENSITY UKIBAHATIKA MEDIUM DENSITY. ILA HUWEZI KUPATA LOW DENSITY KWA HIYO PESA. HEBU MWENYEWE FIKIRIA HIYO 2.5M NI SAWA NA DOLA AU PAUNI NGAPI?

    TATU UAWEZA KUPATA KIWANJA CHA HIYO BEI MPAKA CHINI YA HAPO LAKINI HAKIJAPIMWA NA KITAKUWA NDANI SANA NA KUTOKA BARABARANI ILA SIO HUKO KIGAMBONI, ITAKUWA MAENEO YA MBALI KIDOGO KAMA TUANGOMA, MIKWAMBE, KISARAWE, KIBUGUMO, NACHO PIA SIO KIKUBWA NA HAKIJAPIMWA KAMA NILIVYOSEMA.

    SASA KAMA KWELI UNATAKA KIWANJA TAFUTA HIYO 5M, MWAMBIE JAMAA YAKO AKUTAFUTIE KABISA KIWANJA AANZE PROCESS, KISHA TAFUTA NAULI NENDA MWENYEWE DAR, KANUNUE MUANDIKISHANE MKATABA KWA WAKILI, UJAZE TRANSFER DOCS KABISA KISHA PELEKA DOCS ZAKO PAMOJA NA HATI/OFFER YA KIWANJA KWA TRANSFER KABISA KABLA HUJAONDOKA, INABAKI JAMAA ZAKO WANAFUATILIA TU HUKU NYUMA. HAPO UNAWEZA KUSEMA UMENUNUA KIWANJA NA SI VINGINEVYO.

    mswahli

    ReplyDelete
  12. wasikukatishe tamaa dada mil 2.5 si pesa ndogo kabisa,sure you can do it!

    ReplyDelete
  13. FUATA USHAURI WA MCHANGIAJI WA 5 HAPO JUU

    ReplyDelete
  14. we Sakina!!!yaani kukaa kote nje unaongelea ishu ya 2.5m?? hii ni aibu kubwa kwa wabeba box...sasa nyumba utajengaje???....ndiyo maana mimi simaindi kwenda kubeba box kabisa...ongeza kama hiyo nikuuzie 800sqm beach plot iko 45km from dsm ferry...UNDER SERIOUS NOTE:NINA PLOTS NYINGI
    Mnyau

    ReplyDelete
  15. mama fillipaFebruary 01, 2010

    dada yangu sakina viwanja vya bei hiyo vipo,ninamaana unanunua shamba eka ni laki 300,000.wewe unaenda ardhi iliwakupimie naupate makaratasi ya kiwanja chako. ila ukitaka kiwanja kabisa ambacho kimepimwa ni bei mbaya sana.mimi mwenyewe niko ughaibuni nimejenga kigamboni.namwaka jana nilikuwa nyumbani nimenunua shamba tena kigamboni heka 5 kwa shilingi 1m.nikaenda ardhi wamekuja kupima kila kitu kiko sawa.kwahiyo hizo sehemu viwanja vipo sana.ila ni ndanindani sana.waambie ndugu zako waende kigamboni wakaulizie kwa wenyeji.na kabla ya kununua muende ardhi kuhakikisha kwamba mradi wa viwanja haupiti hapo asante.

    ReplyDelete
  16. Viwanja vya bei hiyo vinapatikana tena kwa wingi. Ila sio kigamboni ya karibu, ukienda about 18 km unapata. Kuna maeneo yanaitwa mwembemtegu, watu kibao tumenunua huko,...na tumeanza kujenga.

    usikatishwe tamaa.

    ReplyDelete
  17. Hello mama fillipa na Dada Wa Kiwanja,
    Mama filipa naomba namba yako or email ili niwe jirani yako,pia mama natafuta eneo la ukubwa kama lako kigamboni,so mimi plus huyu dada tutakuwa wote majirani.
    Kwa Bei hiyo 2.5mill huwezi kupata kiwanja kilichopimwa kwa mtu,kwani serikali wanauza kuanzina 1.5mil,hivyo ukiongeza udalali inafika millioni5-6 hivi,nimesikia kuwa maeneo ya kibada imeshafika mil 10.

    email yangu mama filipa ni
    taifasystems@gmail.com

    ReplyDelete
  18. watu wengine bwana mtu kauliza swali nyie mnajibu vitu vingine ,jibuni swali bwana, mdau uk

    ReplyDelete
  19. Mie nimenunua Mbezi Beach kwa Milion 2.5 miaka 5 iliyopita, wanga wengi haswa unapotaka kufanya jambo la maendeleo!!!, Katika suala hilo kama uko nje ya nchi ni ngumu sana kushughulikia suala hilo ni lazima upate mtu akuhangaikie otherwise ukiwepo "to the ground" ni jambo rahisi na hizo ni nyingi!

    ReplyDelete
  20. WATANZANIA TUNAONGEA SANA HALAFU KUONGGEA KWETU NI KUKATISHANA TAMAA,PONGEZI KWA WALE WOTE MLIMPATIA USHAURI MZURI SAKINA.YEYE ANA PESA YA KUNUNULIA KIWANJA NA SI KUJENGA JAMANI KWANZA MUELEWE.MM NILINUNUA KIWANJA KITUNDA KULE KIBEBERU EKA 3 KIZURI TU.NA TEYARI NIMEMALIZA PROCESS ZOTE ZA ARDHI,NIKAKIACHA,THEN NIKAJA KUBEBA BOKSI HUKU,NA NILINUNUA KWA LAKI 700,000.SASA WEWE UNA 2MILION YAANI UTAPATA KIKUBWA NA CHA KUTOSHA KABISA.KAMA UKO SERIEOUS TUWASILINE MNOGAJR@HOTMAIL.COM THEN NIKUUNGANISHE KWA MWENYE HIVYO VIWANJA.ACHANA NA HAO WACHONGA NGENGA NA WALA USICHOKE NA JITAHADA ZAKO.CC WATANZANIA TUNA CHOYO SANA HASA KATIKA KUSAIDIANA KATIKA MAMBO YA KIMAENDELEO.

    ReplyDelete
  21. AHSANTENI SANA WADAU MLIOCHANGIA HAPO.KWA KWELI NASHUKURU SANA KWA MICHANGO YENU MIZURI.NIMEFANIKIWA KUPATA MAWASILIANO NA MMOJA WA WACHANGIAJI TUMEPATANA NIJE HUKO DAR JUMATANO NIKAANGALIE VIWANJA MAENEO MATATU TOFAUTI KISHA NICHAGUE BEI MAELEWANO KULINGANA NA FEDHA NILIYONAYO NAWEZA KUONGEZA KIDOGO KAMA NITARIDHIKA NA ENEO.
    SHUKRANI ZA PEKEE ZIMUENDEE KAKA MICHUZI,MUNGU AWABARIKI WOTE.
    MIMI NI SAKINA WA TABORA.

    ReplyDelete
  22. sio mbaya sana sema kwa kweli maisha yamepanda sana milioni 2 na nusu naona kama unatafuta kutapeliwa tu kwa msaada wangu endelea kumake kidogo walau ifike 5m au nitafute nikusaidie nipe hizo 2unusu nitaziingiza kwenye biashara zangu alafu kila mwezi nakuongezea kidogo just kupigana tafu maana maisha ni safari ndefu.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 15, 2010

    WATANZANIA WENGINE BWANA?HEBU ACHENI ROHO MBAYA,HUYO DADA KAOMBA USHAURI YA NN KUMKATISHA TAMAA JAMANI?ACHENI WIVU MNACHAFUA BLOG ZA WATU OVYO,NYIE MLIOCHANGIA UJINGA UTAKUTA MAWAZO YENU NI STAREHE TU MWENZETU KAOMBA USHAURI YA NN KUMZODOA!OOVYOOOOOOOOOOOOOOO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...