Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Liberia anaeondoka madarakani,Bi Elizabeth Mlangwa akimkabidhi bendera ya Taifa Afande John Minja ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya watanzania nchini Liberia.
Baadhi ya wanajumuiya wakipitia taarifa ya fedha ya kipindi cha mwaka wa uongozi uliopita.
Baadhi ya watanzania waishio na kufanya kazi nchini Liberia katika picha ya pamoja na viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibuni.

Na Meshack Mfugale wa Globu ya Jamii,
Monrovia - Liberia

Watanzania waishio na kufanya kazi nchini Liberia wamepata viongozi wapya katika uchaguzi ulifanyika hivi karibuni katika eneo la Coconut Plantation jijini Monrovia, Liberia.

Katika uchaguzi huo uliojumuisha watanzania wanaofanya kazi katika taasisi/mashirika mbali mbali ya kimataifa nchini Liberia, Bw. John Minja kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza jijini Dar es Salaam ambaye kwa sasa anafanya kazi na Umoja wa Mataifa jijini Monrovia alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania nchini Liberia, nafasi iliyokuwa ikishirikiwa na Bi. Elizabeth Mlangwa.

Dk. Bwire alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa jumuiya, nafasi iliyokuwa ikishirikiwa na Bw. Deusdedith John Kitambi.

Nafasi ya ukatibu mkuu wa jumuiya ilichukuliwa na Bi. Judith Mshiu. Awali nafasi hiyo ilikuwa ikishikiriwa na Bw. Salumeza Kanuti.

Bw. Athman Sharif alichaguliwa kuwa Mweka hazina wa jumuiya.

Viongozi wapya watakuwa madaraka kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Juni 2010 hadi Juni 2011.

Shughuli ya kuchagua viongozi wapya ilienda sambamba na kuwakaribisha watanzania waliowasili nchini Liberia siku za karibuni pamoja na kuwaaga watanzania wanaotarajia kuondoka nchini Liberia hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 24, 2010

    Ankal hivi kuna nchi ambayo wabongo wanakosekana hapa duniani kweli?Naomba upost na umoja wa wabongo wanaoishi Afghanistan najua wapo wengi tu huko.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 24, 2010

    Safi sana !

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2010

    Asante Ankal kwa kutuhabarisha. Poa kweli, Wabongo wamezagaa kila kona ya duniani !

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2010

    Haya ndiyo mambo yanayotakiwa,siyo wale walioshindwa maisha wanafungua matawi ya CCM.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...