Na Woinde Shizza,Arusha
MUASISI na mwanzilishi wa tawi la chama cha mapinduzi(CCM) katika chuo kikuu cha Arusha Rehema Mroso (pichani) ametawataka wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali nchini hususani wanawake kujitokeza kwa wingi katika kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye kinyang”anyiro cha uchaguzi mwaka huu.
Mroso ambaye pia ni mgombea wa nafasi ya ubunge wa viti maalumu mkoani Arusha alitoa kauli hiyo mkoani hapa wakati wa hafla ya kuwakabidhi na kuwatunuku vyeti mbalimbali waanzilishi wa tawi la CCM katika chuo kikuu cha Arusha.
Alisema ya kuwa kwa jamii ya sasa hususani wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali nchini hawana budi kujitokeza kwa wingi katika kuwania nafasi hizo kwa malengo ya kuwapa kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi nchini.
“Ninatoa wito kwa wanawake hususani wahitimu wa vyuo vikuu mbalimbali nchini kujitokeza kwa wingi nchini kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi wa mwaka huu”alisema Mroso
Alisema ya kuwa kwa hali ya sasa bunge la jamhuri ya muungano ya Tanzania linahitaji wasomi ambao wanaweza kubadili hali ya maisha ya watanzania kupitia elimu yao .
Awali akikabidhi vyeti mbalimbali vya heshima kwa waanzilishi wa tawi la CCM katika chuo hicho,mgeni rasmi katika hafla hiyo ambaye pia ni mwanasheria wa CCM kutoka makao makuu,Glorius Luoga aliwataka vijana wa jumuiya ya CCM nchini kutotumika kama madaraja kwa viongozi wakubwa katika kufanikisha malengo yao.
Mwanasheria huyo aliwataka vijana hao kutotumika kama migongo ya baadhi ya wakubwa katika kufanikisha malengo yao hususani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
“vijana safari hii wataonekana wanafaa sana lakini wamekuwa wakitumika kama migongo ya wakubwa kufanikisha malengo yao katika chaguzi mbalimbali ,mimi nawaasa vijana kuwa waaminifu wasiwachague Viongozi wanaotoa fedha kuwahonga”alisema Luoga
Katika hatua nyingine Luoga alichangia kiasi cha sh,700,000 kama mchango wa ujenzi wa ofisi ya tawi la CCM katika Chuo hicho sanjari na kuwakabidhi kadi wanachuo 150 walioamua kujiunga na chama cha CCM katika chuo hicho kwa hiyari yao.

sasa anti kama kila mtu akipiga siasa taifa litajengwa na nani?
ReplyDelete(US Blogger)
This is serious!! Wewe ni mwanafunzi wa chuo halafu ukagombee ubunge!!. Ukichaguliwa kuwa mbunge utasoma lini na utawawakilisha waliokuchagua lini? Hii sasa inatisha. Taifa linaangamia. Mimi nilidhani mambo ya siasa hasa katika level ya kugombea uongozi kama ubunge, udiwani, urais, n.k. ni pale unapomaliza chuo. Jamani hebu tuwe serious, mshika mbili moja lazima imponyoke. Wanachuo wenzangu hebu achaneni na siasa tusome ili tupate ujuzi wa kuja kuendeleza nchi yetu.
ReplyDeleteMdau,
Mwanfunzi wa SUA,
MOROGORO
MwanafunzI sUA usihofu.acha wagombee tu kwani kule kuna kazi? kazi zilikuwepo enzi za mwalimu. Sasa hivi kila mtu anaweza kuitwa mbunge. Si cheo tu? na masomo kama kazi. Si wewe mwenyewe huwa unaangalia luninga kipindi cha bunge! kuna ambao hata huwa hawajui bunge limemalizika saa ngapi. Wao huuchapa usingizi from day one mpaka mwisho. Hatujawahi kusikia neno kutoka baadhi ya wabunge.
ReplyDeleteShule ipo mtasoma na ubunge hapo hapo. Wabunge siku hizi wanawakilisha familia zao si wananchi. Nyie gombeeni muwakilishe familia, ni pamoja na kununuliwa magari ya kifahari kila mwanafamilia, kusoma na kutibiwa ulaya, kupiga mkorogo mpaka basi. Jamani wewe mchuo unataka wenzio wakose hayo? Ukisoma kama wewe si wa ukoo wa ubunge hata kazi hupati.
HABARI NDIO HIYO
Ahaa Kweli huyu mama lazima ahamasishe wavyuo kugombea. Siasa ni mchezo tu kila mtu anaweza , alimradi uwe kwenye system yaani uwe ndugu wa mbunge au waziri hapo mambo safi.
ReplyDeleteNadhani baadhi ya wachangia mada labda wamekurupuka au neno wahitimu kwao ni msamiati mgumu.
ReplyDeleteJapo sishabikii wasomi kuingia kwenye siasa, huyu dada amewahimiza WAHITIMU ( hao ni wale waliomaliza masomo tayari) kuingia kwenye siasa. Ujumbe wake hauwahusu wale walioko shule bado.