Justin Kasusura akitoka katika chumba cha Mahakama huku akisindikizwa na askari magereza baada ya rufaa yake ya kupinga kifungo cha miaka 35 jela kutupwa na Mahakama Kuu Dar es Salaam.

Kasusura alihukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwezi Machi 2007 kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha na wizi wa dola milioni mbili za kimarekani.

Mahakama Kuu imetupilia mbali rufaa hiyo ya Justin Kasusura ya kupinga adhabu ya kifungo cha miaka 35 jela kutokana na kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha na wizi wa dola milioni mbili za Kimarekani.

Jaji mstaafu Thomas Mihayo katika hukumu yake alisema kuwa hukumu iliyotolewa na mahakama ya Kisutu ilikuwa sahihi na rufani iliyokatwa na mrufani aina sababu za msingi za kutengua hukumu hiyo na hivyo mshitakiwa ataendelea kutumikia adhabu yake kama ilivyotolewa na Mahakama ya Kisutu Machi 27 mwaka 2007 na hakimu, Sivangilwa Mwangesi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2010

    huyu mtu hata kama aliiba kwakweli does not deserve to be sent to prison for 35 years. hizi courts za tanzania mbona judjements zao nyingi ni za uonevu. mimi simjui huyu mtu lakini i hope and pray one of these days atasamehewa na raisi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 23, 2010

    DUUU!!NILIKUWA NIMESHASAHAU KESI YA HUYU JAMAA,KUMBE WALIMFUNGA..NA WALE WAKINA URASA JE WA UKONGA WAO PIA WAMEFUNGWA?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 23, 2010

    Mbona huyu jamaa haonekani kama anatokea magereza. Maanake kavaa vizuri na kupendeza sio kawaida. Anaonekana pia alikuwa mwana fasion pimp fulani hivi

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 24, 2010

    bongo kweli shwain yani kesi ya kuiba ndio afungwe miaka 35 nimeamini kweli bongo wanatoa hukumu kwa kuangalia mshitaki

    huyo jamaa kafungwa miaka 35 kwa sababu hela alizoiba ni za ubalozi wa marekani sasa wanatoa adhabu kali kwa kuwaogopa wamarekani ili waonekane wametoa adhabu kali

    huku nilipo mimi naishi hapa nchi yenye mahakama kuu ya dunia nchi hii hata ufanye kosa gani adhabu ya mwisho ni jela miaka 5

    kwanza mihela yenyewe sio yao ni ya marekani nchi bilionea si wamuachie tu ajenge nchi yake na hiyo mihela

    mdau wa mahakama kuu ya dunia nawakilisha

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 24, 2010

    huyu jamaa ni fala sana mi hata simuonei huruka wewe mtu mzima utaibaje kipumbavu hivyo!!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 24, 2010

    mbona wa bilioni na ushee kafungwa miaka miwili? kwani tofauti ni nini? gap kubwa sana

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 24, 2010

    Hivi kumbe majambazi wako kama sisi??

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 24, 2010

    Maskini Kasusura~ Hivi mihela yote hiyo uliiharibu bure kwenye gesti na vimwana. Sasa ona kesi ilivyokushinda. Hizo hela ungewapa hawa wasingekufunga. Kesi ya pesa haimshindi mtu bwana. Pole sana. Sijui hiyo miaka itakukuta? maana naona imefika saa 10 jioni.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 24, 2010

    Nyinyi wapambe wa Kasusura. Mpende au msipende, wizi wa kutumia silaha ya moto ni very serious na adhabu yake inajulikana. Ushahidi uliotolewa ulikuwa bayana. Kama hamjafaidi kitita hicho mfuateni magereza anaweza kuwaeleza amezificha wapi...LOL.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 24, 2010

    KASUSURA UMEKOSEA MAHESABU WEWE UNGEONESHA NIA YA KUTAKA KUGOMBEA KUPITIA CHAMA CHA MAPINDUZI UNGETOKA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 24, 2010

    Ingekuwa Uchina, ungekuwa umekula shaba!

    ReplyDelete
  12. maskini kasusura,miaka 35 na rufaa imeonekana kupigwa chini!

    mdau.

    ReplyDelete
  13. Wale wote mliomegewa mgao na kasusura mnaombea tu aendelee kubaki ndani ili asije kuwanyang'anya chake. Familia yake inataabika, mkewe alifariki kwa ugonjwa malaria baada ya kukosa msaada. Huko majamaa yanakamua kama kawaida.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...