bustani mwanana inaremba sehemu za Machinga Com[lex ambayo ni majengo maalumu yaliyoandaliwa kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga ili kuwapa sehemu nzuri ya kufanyia kazi na kuondokana na kero ya kupigwa na jua na mvua barabarani. Mradi huu ambao umebuniwa na JK unatarajiwa kufanyika wilaya zote tatu za jiji la Dar na baadaye mikoani. Hivi sasa wamachinga wameruhusiwa kuingia na kuanza kazi inagwa ufunguzi rasmi bado. Inasemekana wiki ijayo sherehe za ufunguzi rasmi zitafanyika. Jumla ya wamachinga 4,500 wanatarajiwa kufanya biashara zao humo
sehemu ya chini kusini
mafundi wakiwa kazini kujenga ofisi za
Benki ya Wamachinga itayokuwepo hapo pamoja na ATM kibao
sehemu ya ndani katika mojawapo ya ghorofa tano za jengo hilo
wadau wakiingiza fomeka kwa ajili ya kutengenezea segemu zao
mama anaandaa biashara ya khanga. anasema anashukuru kupata maghali rasmi pa kufanyia biashara na kwamba ada ya 2000/- kwa siku
wadau wakijiandaa kuingia kazini kwenye
sehemu iliyotengwa maalumu kwa stationary

mojawapo ya ghorofa katika jengo hilo
wengine tayari wameshaanza kazi
kwa nje











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 30, 2010

    hiyo machinga complex ipo wapi? maana nahisi kama itakuwa china complex, jego zima litachukuliwa na wachina

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2010

    Sawa imeanza kazi, lakini hiyo ni sehemu ya wateja kununua bidhaa au ni gereza?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 30, 2010

    bravo jk,ahadi zako zote umefanyia kazi,japo kuna watu hawapendi kukubali,sema hiyo finishing ya ndani halmashauri ya jiji wameifanya kienyeji sana,maana jengo wamekabidhiwa zuri,wawo walitakiwa kujenga mabanda ya ndani tu,stil wamefanya kulipua.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 30, 2010

    Sana sana na natoa mwaka, halafu mnipe majibu ya hiyo complex yenu. Mtakoma kuringa.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 30, 2010

    Hivi walikosa vifaa vya kufanya 'partition'!!! Mbona inaonekana kama mabanda ya naniiii wale wa kienyeji!!



    Nkyabo - Bongo

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 30, 2010

    Good idea JK lakini mbona iko kama Zoo? Well tunaelewa hapakuwa na njia...ili kuepuka vibaka kuibia wenzao...ndo njia pekee. Pili ni lazima watu waweze kuona bidhaa na vioo kwa wamachinga...Lol inaweza kuleta hatari...ila acheni kukosoa vitu angalau wataondoa kero kule katikati ya mji....

    ReplyDelete
  7. MBONA NI KAMA PARKING GARAGE????.....WACHORA RAMANI WA BONGO MIYEYUSHO KWELI YAANI..HII NI KARNE YA 21 BADO MNACHORA NA KUJENGA VITU VYA AJABU, AU MPAKA WAGENI WATUSAIDIE??...SIDHANI HATA KAMA KUNA AIR CONDITION HAPO

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 30, 2010

    Wazo ni zuri ila vyumba ni vidogo sana ni kama gereza tu

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 30, 2010

    Mtasema natabiri uchuro.
    Tahadhari ya MOTO ipo hapo?
    Sioni tahadhari yoyote ile,maana bidhaa zikijaa hapo jengo laweza kuwaka moto kama kiberiti

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 30, 2010

    Jamani machinga complex iko wapi? Pale manzese? na hilo daraja la kupitia watu ndio lile lililojengwa pale manzese miaka ya 80? mwenye maelezo asaidie

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 30, 2010

    Moto.. waweke matangazo ya kukimbia moto/kupambana na moto na kuwe na njia za kutoka mkuku moto ukitokea... vinginevyo itakuwa hatari

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 30, 2010

    Ushuru kwa siku 2000? macho yangu yamesoma vizuri au? na je analipia pango.Kwa hiyo ushuru kwa mwezi 60,000 na kwa mwaka 720,000 kweli biashara ya Machinga itarudisha?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 30, 2010

    hivi mtu kakaa chini kabisa na kutumia ujuzi na ufundi na pesa kujenga hivyo vyumba vya biashara?
    1.) usalama wa mali ya mfanyabiashara upo wapi?
    2.) kuna suala la privacy (samahani kamusi imegoma) nalo mbona halijazingatiwa?

    ReplyDelete
  14. KionaMbaliJuly 30, 2010

    Sawa Kaka.

    Lakini kuna Paking ya amagari ya uhakika hapo na kuna Walinzi wa magari?

    Au ndo mambo ya kutoka unakuta hakuna SAITI MIRA?

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 30, 2010

    duh hii ni complez kweli maana naona ni gereza tu sijui ujenzi wa nani huu kwa kutaka kubana matumizi.Hii noma na kwa bei waliyopewa

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 30, 2010

    huu mradi ni tembo mweupe, utakuja kuwa kama soko la makumbusho, kwa sababu biashara ya machinga inafuata mteja na si mteja amfuate machinga

    ReplyDelete
  17. Hii imekaa kama fire hazard place tu!

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 30, 2010

    Hao wamachinga wawe wastaarabu sasa jinsi ya kupanga vitu na usafi ama sivyo kutakuwa kama soko la kariakoo..
    Mdau,
    US

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 30, 2010

    Anon wa Fri Jul 30, 01:39:00 PM

    Umeeleza point moja muhimu sana. Kwa jinsi hiyo sehemu ilivyo tutarajie wateja kukabwa kila siku na kuporwa vihela vyao.

    Baada ya kujenga hivi ilitakiwa kuimarisha na ulinzi wa polisi 24 hours, yaani kuwe na kituo cha polisi pamoja na askari wa kuangalia usalama muda wote; ila jiji watakachofanya baada ya uzinduzi wa kukifungua kwa ajilia ya kampeni za uchaguzi ni kukitelekeza.

    Na si ajabu wananchi wakasusia hiyo sehemu kwa usalama wao. Mfano mzuri ni daraja la Manzese ambalo watu wanaliogopa kama ukoma.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 30, 2010

    Nani amedesign hiyo kitu, mbona panatisha? Na hiyo 2000 kwa siku ni nyingi sana kwa watu waliolengwa. Wazo zuri lakini tayari muelekeo wake ni mbovu.

    ReplyDelete
  21. Hatua kwa hatua kuelekea kwenye maendeleo ya kifikra.Je?tunaweza kuzuia wanapenda kujisadia haja hovyo hovyo....kua maji na huduma za kijamii za kutosha kama clinic kama sio hospitali?kuna mbinu mbadala za kuzuia wizi?na uahalifu mwingine?ni wasiwasi kwa jambo hili.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 30, 2010

    hayo mabanda mbona kama ya kuku? madogo mno nafasi ndogo pia kwa wateja kutembea kuangalia vitu.jinsi nafasi zilivyo jibana hapo wizi utaongezeka na hewa itaweza kuwa nzito sana na kuhatarisha afya za watu.

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 30, 2010

    Naona hao wanaoenda kwa stationary section kama sio machinga vile. Mwishowe wa yote machinga kweli watakosa sehemu na wale wenye uwezo wa kurent sehemu zingine huko mjini wachukue hiyo chance ya mlala hoi kweli kweli....

    Watahakikishaje kuwa wote wanaopewa nafasi hapo ni wale walikua wanauza mitaani tu? Bila hivyo complex itachukuliwa na wenye mission zao mjini na machinga wa kweli wabaki mitaani na kutaabika.

    Halafu ninavyojua machinga wa kweli hela ya kuweka bank hana. Akipata hela kwa siku ni kwenda kununua chakula cha familia yake na kulipa mama mwenye nyumba...Hiyo bank ingekaa huko huko mbali wakitaka machinaga wataifwata huko huko. Bank za kwetu wala sio za kuwasaidia watu wasio na hela bali ni kuwafilisi tu zaidi. Bank inacharge interest na fees kubwa kuliko hela iliyo kwenye account si kuengezeana umasikini tu hapo. Mtawamaliza hao machinga...Na mwisho wa yote utasikia lazima uwe na account kwenye hiyo bank ndio upewe sehemu ya kuuzia vitu vyako...

    .

    ReplyDelete
  24. ili jengo mpaka ikifika krismas litakuwa halitamaniki kwa uchafu ndani na nje subiri mtaona

    ReplyDelete
  25. Kaka TrioJuly 31, 2010

    Faya code zimefuatwa? au hadi moto uje utokee uuwe maelfu ndio tustuke? Hizo cage sidhani kama zinaipa nafasi emergency exit doors! Yangu Mecho....

    ReplyDelete
  26. AnonymousJuly 31, 2010

    wewe mdau wa 1.39 pm its better than nothing kumbuka hao wamachinga wanapata tabu ya kuzunguka mji mzima na joto la dar.pia kwa usarama wa moto ni afadhali pawe hivyo wakitenganisha na mbao ni hatari na nadhani wamepunguza joto pia kuliko kuweka tofari

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 31, 2010

    mbona yamekaa kama mabanda ya kuku wa kisutu?

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 31, 2010

    Sijaona fire extinguishers zozote wala vyoo.

    ReplyDelete
  29. AnonymousJuly 31, 2010

    Hongereni wadau kwa chambuzi nyingi za kujenga.Mjengo huu uko Ilala jirani sasa na soko la Mchikichini,kituo cha basi karume.La msingi ni kwamba hatua fulani imepigwa kuboresha hali za hao walengwa -Machinga.Nadhani ukiangalia utaona plani ya kupatition sio mbaya nina imani uwazi uliopo sio wa hatari sana kufanya watu waishiwe hewa.kumbe hilo la viyoyozi litadai tena muundo mzima ubadilike bilashaka.La msingi wahusika wajipange na warekebishe yale ya msingi kama tahadhari ya moto ma usalama wa mali za wateja.azawaisi good start!

    ReplyDelete
  30. AnonymousJuly 31, 2010

    Ni hatua jamani lazima tukubali hali ya bongo na mfumo mzima wa uongozi wake hasa katika karne ya nahihii kila kona, hii wanayofanya tahenkuru.mengine yakichefua si tutaona na kuwapigia kelele.hata kariakoo walau siku hizi inaonekana twende tu tutafika.chonde tusifananishe sana na mashoping mall ya wenzetu au kama mlimani city,kwenye kipupwe hapo gharama ndo itakuwa toba weee!!

    ReplyDelete
  31. AnonymousJuly 31, 2010

    Whow! Penitentiary II no heat in tropical condition, well done.
    Mdau
    Lupango US.

    ReplyDelete
  32. AnonymousJuly 31, 2010

    KULIPIA SH. 2000 KWA SIKU KWA MACHINGA NA BIASHARA KAMA HIYO SIJAJUA NINI ATABAKISHA MFUKONI MWISHONI MWA SIKU.
    HUU NI UNYONYAJI WA WAZI KWA WALALAHOI, KWANI INAONEKANA JENGO HILO NI KITEGAUCHUMI ZAIDI BADALA YA KUONDOA KERO YA MACHINGA KATIKATI YA JIJI NA MAENEO YASIYORUHUSIWA KUFANYA BIASHARA.

    ReplyDelete
  33. Watanzania mmezidi maneno au niseme kulalamika badala ya maoni hapa. NInani duniani anepangisha sehemu ya biashara kwa chini ya $2, mmachinga ni muhimu ajuwe kwamba kuna kulipa kodi, tatizo langu ni kwamba sijui wamechaguwa namna gani ya hao wamchinga kupata hiyo nafasi. Kama ni kwa ajili ya bahati nasibu hiyo ni njia ya uhalali, lakini kamani kujaza form ina maana kuna wala rushwa hapo, na kuna watu ambao wangepata hizo nafasi na wamekosa kwa sababu hawajui mtu. Kuhusu jengo ni safi sana kwa hali ya TZ, Tatizo ni kama hakuna EXIT za kutosha kama kuna moto hapo ni tataizo, kwani kunahitaji uwa na ngazi za nje. Je jengo hili ni la serikali au ni la mtu binafsi?
    Nadhani hakuna kitu kizuri kama vijan kupata ajira, namshukuru sana aliyejenga hili jengo kwani litasaidia familia nyingi sana.Watoto wengi watapata chakula cha usiku na kualal wameshiba sababu ya hii sehemu, watoto wengi watapta kalamu ya kwenda shule kwa sababu ya hili jengo. kuhusu ulinzi nadhani kampuni ya walinzi ya watu binafsi ni nzuri kuliko polisi.

    ReplyDelete
  34. bomu la hiroshima hilo moto hapo ukittokea ni salia mtume. moto moto jamani mbona tunajitengenezea majeneza? ilitakiwa wkubali kuamua mtaa wa uhuru mpaka mnazi ni market area kariakoo inter market kingeeleweka.kama camden town vile. kuia moto na kukwepa moto ingekuwa rahisi

    ReplyDelete
  35. Haya niambieni na hilo jengo la machinga complex, je kama kukitokea dharuara yoyote kuna njia za kujiokoa kwa dharura hiyo?

    Wazo la kuwa na sehemu kama hiyo lilikuwa zuri. Lakini umaliziaji wa hilo jengo umekua ni dhaifu ajabu. Kwanza jengo linaonekana lina mwanga hafifu na sielewi kama likifurika wachuuzi na wanunuzi kama kutakua na good visibility. Labda mnataka kuniambia kwamba lna umeme na zile taa za fluolescent zinawaka mtindo mmoja kugawa mwanga kwa watu watakaokuwepo hapo.

    Je kuna choo? na kama kipo nani atahudumia? Nakubaliana na mtoa maoni hapo juu aliyesema anatoa mwaka mmoja na tutaona patakavyo kuwa pamefujika. Maana sisi watanzania tuna historia ya kutokuwa wasafi wa mazingira.

    Kuhusu kupata eneo, je ni masharti gani? na je itakuwa fea kwa kila mtu? Rushwa jamani!!!

    Hongera Jiji kwa kuwafikiria wamachinga lakini utunzaji ni kitu ambacho mtatakiwa kuúzingatia.

    ReplyDelete
  36. kweli Sun Aug 01, 01:50:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous Anonymous hujui unachoongea, wewe unaongelea dunia ya dola $2 nani kakwambia wanakodisha dola mbili, tunaongelea Tanzania shilingi. Hivi unajua maisha ya Mtanzania anaishi kwa dola ngapi ukitaka kuweka maisha kwa kulinganisha dola. Pili unasema watu hawaishi kulalamika mara unaanza kulalamikia urasmu wa kugawa vyumba. Odoa kibazi kwenye jicho lako kabla ya kuona boriti la kwenye jicho la mwenzio

    ReplyDelete
  37. ni wazo zuri hili ila tunaomba na picha za vyoo,mabafu,kituo cha polisi,clinic,vizima moto

    utupe picha hapa wewe mpiga picha vipi???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...