Ofisa Sheria wa Tume Shadrack Makongoro (kulia) akimkabidhi Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Evarist Mbaga baadhi ya nyaraka zilizofanyiwa kazi na tume.
Ofisa Sheria wa Tume Shadrack Makongoro akionesha msisitizo wakati akitoa ufafanuzi kwa wazee, viongozi wa dini, watawala wa jadi na washauri wa baraza wakati wa kupitiwa kwa rasimu ya sheria za mila zinazofuata mkondo wa mama.
Baadhi ya Wazee wa wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro wakimsikiliza kwa makini Ofisa Sheria wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania,Shadrack Makongoro (hayupo) pichani wakati wa kujadili rasimu ya Sheria za Mila zinazofuata mkondo wa ukoo wa mama wilayani humo. Wazee hao wamesifu jitihada zinazofanywa na Tume hiyo katika kuzifanyia marekebisho sheria mbalimbali ambapo Tume hiyo imekuwa ikiwashirikisha wadau kwa kuwafuata mahali walipo kama ilivyofanya katika sheria hii ya mila ambapo tayari imeshawatembelea wadau wa mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara na sasa iko katika mkoa wa Morogoro ambapo huko imeanza kwa kuwatembelea wadau wa wilaya za Ulanga na Kilombero na sasa imeelekea Kilosa na baadaye Mvomero.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. sheria za tanzania hazieleweki. katiba ya nchi haiweki wazi. wenye sheria ni ccm na wanaweza kuibadilisha wanavyotaka. hivi vitu ni lazima viwekwe wazi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...