PAMBANO la watani wa jadi Simba na Yanga linatarajiwa kuchezwa Oktoba 16 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Pambano hilo ambalo litakuwa ni la mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania bara iliyoanza kutimua vumbi Agosti 21 ikiwa ni siku mbili baada ya vigogo hao kuvunja utepe katika mchezo wa kuwania ngao ya hisani iliyochezwa Agosti 18 na timu ya Yanga kuibuka kidedea kwa kuinyuka Simba mabao 3-1, Mchezo huo utachezwa Kirumba baada ya uwanja wa Uhuru kufungwa kutokana na shughuli za kitaifa na hivyo klabu za Ligi Kuu za jijini kutakiwa kusaka viwanja nje ya Dar es Salaam.

Kufuatia hali hiyo Yanga ilipeleka maombi Wizarani kuomba kutumia uwanja wa taifa hali kadhalika kwa Simba.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa Yanga wameruhusiwa kutumia uwanja huo kwa kukatwa asilimia 10 ya mapato ya mlangoni kama garama ya uwanja pia itakatwa shilingi milioni tatu za usafi iwapo watacheza na timu kubwa ambayo italazimika kutumia mageti yote ya uwanja na iwapo itatumia
mageti machache itakatwa shilingi milioni 1.8.

Hata hivyo kuna taarifa kuwa Simba ambao awali walitangaza kutumia uwanja wa CCM Kirumba waligeuka na kupeleka barua wizarani kuomba nao waruhusiwe kutumia uwanja huo kitu ambacho kiliiwia vigumu serikali ambao walidai haiwezekani kutumia uwanja huo kwa mechi
mfululizo.

Kaimu katibu mkuu wa TFF, Sunday Kayuni amesema leo kuwa "Baada ya mazungumzo ya muda mrefu Wizara ilikubali ichezwe michezo miwili kwa Simba na Yanga lakini kwa taratibu zetu haiwezekani kuwa na viwanja viwili vya nyumbani nje ya mkoa wake hivyo tuliviachia vilabu vikubaliane kuachiana jambo ambalo halikuwa rahisi."alisema Kayuni.

"Maamuzi ya mwisho Simba watatumia uwanja wa CCM Kirumba na tunaitaka Yanga itufahamishe uwanja watakaotumia ifikapo saa kumi na moja jioni hii, Simba pia wametuarifu pambano lao na Yanga litachezwa Kirumba kwa kuwa wao ndio wenyeji wa mchezo."alisema Kayuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. sawa hilo liwanja la neshno limegeuzwa kuwa museum?kweli hii nchi tutafika kweli?mnataka kukuza vipaji vya wachezaji lkn zana za kuwapa wachezaji mnazibania kwa sababu ya ubinafsi na siasa pumbavu mbili!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...