Anko Michuzi nimekuwa kimya sababu ya kusaka Nondoz huko A-Taun. Tumehitimu juzi na kutunukiwa nondoz katika kitivo cha sayansi za jamii. Chuo Kikuu Cha Tumaini University. Asante mdau Meshack Maganga.

http://magangam.blogspot.com
meshackmaganga@gmail.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. "...chuo kikuu cha tumaini university..." ndio nini, jamani?

    ReplyDelete
  2. Nawapeni hongera kwa kufikia hatua hii. Mimi kama mwalimu napenda kuwakumbusheni kuwa elimu haina mwisho. Chuoni mmepata fununu kuhusu upana wa hii bahari inayoitwa elimu. Sasa kazi yenu ni kuzidisha bidii kujielimisha.

    Kama ni vitabu, muwe makini kuvitafuta na kuvisoma. Mna wajibu wa kuchangia taaluma zenu, na kutoa mchango kwa jamii. Kumbukeni kuwa kuna kusoma na kuna kuelimika. Mtu aliyeelimika hana mbwembwe. Anafahamu kuwa elimu yake ni tone dogo sana katika bahari. Anawaheshimu na kuwasikiliza wengine, wawe wamesoma au hawajasoma, kwani elimu haipatikani shuleni tu. Nawatakieni kila la heri.

    ReplyDelete
  3. Nawapa hongera sana enyi watanzania wenzangu.Kila laheri katikaa kujenga taifa letu.

    Mtunza Kumbukumbu

    ReplyDelete
  4. Kuandika Chuo kikuu cha Tumaini University inaonesha ni jinsi gani watanzania walivyo watumwa wa lugha ya Kingereza.

    Kuandika Chuo kikuu watu wanaona haitoshi mpaka waweke University lol!!

    Tuache huo utumwa jamani ,tuache 'kuchakachua' lugha

    ReplyDelete
  5. Hongereni kwa kufikia hatua hiyo japo ni mwanzo wa safari. Nawatakia safari njema na mfike salama husussan kufikia malengo yenu!

    Napenda kumpongeza mdau aliye toa maoni hapo juu kuhusu utumwa wa lugha. Jamani hakuna lugha iliyo ya maana kuliko nyingine, tuachane na ugonjwa huo. Wa Tanzania ifike mahali ambapo tutmie lugha kwa usahihi zaidi hiyo hutua mojawapo ya kuwa tume elimika. Kusema Chuo Kikuu cha Tumaini University kweli inatia kichefuchefu.

    Najua kuna wakati tunaandika baadhi ya mambo kwa kufurahisha na kwa utani lakini napenda kuwa kumbusha wadau kuwa blog hizi zipewe heshima kama sehemu muhimu ya kubadilishana taarifa na mawazo.

    Unakuta baadhi ya wadau wameandika matusi, huko ni kukosa ustarabu na hekima.

    ReplyDelete
  6. Nilidhani ni mimi pekee ambaye kila siku nakosoa kuhusu kuandika "Chuo Kikuu cha Dodoma University" au "Barabara ya Morogoro Road" kumbe wadau wengi mnaliona tatizo hili. Huu ni uharibifu wa lugha kwani kuandika Chuo Kikuu peke yake au Barabara inatosha sio lazima uandike "University" au "Road".

    ReplyDelete
  7. Nyie mnaokosoa lugha katika globu hii inaonesha ni wageni kabisa katika jukwaa hili. Hio ni burudani tu, wala haina maana kwamba Michuzi hajui afanyacho, poleni sana kwa sababu hamjui mtendalo!
    Kwani hamjaona Michuzi anaandika mara nyingi tu neno ' MDAU AKIWA NA MY WIFE WAKE' au 'MY HUSBAND WAKE'? Hio ni kinogesho cha jukwaa tu.
    Msihofu na hilo.
    Mdau wa Mwenge Kijijini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...