Hi kaka Michuzi,
Mie nimekuwa mdau kwa kitambo kirefu na nilizia sana kuwa wa Milioni kumi lakini bahati haikuwa yangu na katu sikuweza kuilalia mlango wazi bahati ya mwenzangu.

Pia leo ni siku yangu ya kuzaliwa kaka 17th December hapo jijini Dar ila kwa sasa ninaishi Apeldoorn, the Netherlands. So si vibaya nami niking'aa kwenye ukurasa wa Michuzi maana nimefuatilia msiba wa Dr. Remmy Ongalla kama nipo Dar es Salaam maana nilikuwa naishi pale kwa Sinza kwa Remmy, mtaa wa Muungano, Block No. 673.

Ahsante sana kaka na nakutakia kazi njema katika kutupasha habari za nyumbani maana kwaa hakika nakubali sana kazi zako na latest pics za VIOTA vipya vya Dar kaka!!

Thanks in advance kaka Michuzi a.k.a Mzee wa Libeneke.

Says
Tully, Rudewa Jr

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hongera kaka naona umri unakwenda na kama kawaida train hilo linakupeleka kupiga box safi sana halafu hela yenyewe inaishia kwenye rent,kodi ,bills na savings kidogo ndio maisha hayo ndugu yangu bongo hali ni mbaya zaidi piga moyo konde na upweke wako usijali

    ReplyDelete
  2. Kwanza Hepi Basidei ya kuzaliwa kwako. Pia tumekuona uko ulaya ya uholanzi, ila kumbuka siku hizi hawataki wageni tena, hawana kazi wenyewe na kila mgeni kwao sasa ni nuksi. Angalia maisha yako na asikuchuje mtu urudi bongo, hamna umeme wala maji mpaka leo.

    ReplyDelete
  3. Kazana sana kijana kuangalia taarifa za habari za Tanzania, kweli Tully Remmy mwenyewe alikuwa anakujua sana pole sana kwa msiba. vipi the netherlands wanasemaje naona unawaka bongo jua kali, mishahara iko juu sana sasa laki moja kwa mwezi rudi nyumbani kaka uchaguzi umeisha.

    ReplyDelete
  4. happy birhday tully si mbaya kuuza sura mara mojamoja hasa siku special kama hii,
    nakutakia upigaji mzuri wa boksi na usisahau kusaidia wazazi angalau vicent vya kubadili mboga.

    ReplyDelete
  5. Duh hizi comments noma

    ReplyDelete
  6. watu mna visa umu!!kama JF vile
    aya dogo adabu tu heshimu walinazo na wasionazo

    ReplyDelete
  7. Kweli ubinadamu kazi, naona umeamua kuuza sura kwa kisingizio cha birthday, hapo kaka unawahi shift ya asubuhi Mac Donald. Trash work njema kaka Tully

    ReplyDelete
  8. Duh, yaani wadau wa hapa kweli nuksi. Nimecheka sana na maoni ya mdau kuhusu ishu ya Trash work ya McDonald's. Jamaa sasa anafikiri kwa nini kauza sura bei nafuu.

    ReplyDelete
  9. TULLY

    Hongera kwa kusogeza mwaka mwengine. Ila inabidi utambue kuwa miaka yako duniani (umri) ndio inapungua. sasa pamoja na kushereheka, inapaswa kuzingatia kuwa na kifo/mauti nacho kimejisogeza kwa mwaka moja.

    Kiufupi, ni furaha endapo umefanya unayopaswa kufanya; na ukitazama nyuma; mwaka uliopita umefanya mambo unayoweza kujinadi nayo.

    La si hivyo, ni huzuni na inabidi itawale kutokana na kwamba amali za kujivunia hazikuchukua nafasi kubwa mwaka uliokwisha.

    ALAMSIKI

    ReplyDelete
  10. bosco wa magomeni mapipaDecember 17, 2010

    HONGERA SANA TULLY
    ila jiangalie sana kwani wenzako hapa dar wako na maendeleo sana nchi imebadilika kimaendeleo alonacho anacho hapa......na njia ziko hapa zakutafuta hasa ukishakaa ulaya, kama uko sawa kidogo tu basi rudi na nitafute mimi niko pale pale magomeni kijiweni, ninakula raha zangu kila jioni ...kwani sikujuwa mimi hama uko beach hilo kavu lisilona hata mchanga ....ningekupigia nilipita hapo mwezi uliopita nuksi tupu hapo hupigiwi simu mpaka uwe na LYCA.....HAHAHAHAHA.....AMA KWELI ULAYA HIYO ULIYO WEWE INGENISHINDA .....ila nipigie tuongee kaka

    ReplyDelete
  11. HAPPY BIRTHDAY DOGO.ZEEKEA HUKOHUKO
    NASIKU ISHIRINI SIJA WASHA LUNINGA.
    NAOGA MAJI YA KISIMA.NATEMA SANA KWENYE FOLENI.

    ReplyDelete
  12. DUHH WATOA COMMENT WANA HASİRA UTAFİKİRİ WANACHAMA WA CUF HEHE , KAAZİ KWELİ KWELİ , TUPUNGUZE JAZBA NDUGU WATANZANİ

    ReplyDelete
  13. Happy Birthday Kaka, kumbe na wewe unamindisha hayo magazeti ya bure eeh, hilo gazeti tunatumia zaidi sie masikini tunaokaa ulaya kwa maana ni la bure kila mpita njia anapewa, kila sehemu limewekwa unaweza jichukulia,,halafu limezagaa sana Europe, sijui nchi gani huku ambao hawana hilo nadhani zipo chache ambao hawalitumii.Kazana kaka, yote maisha, boksi, umeneja,mradi mkono unaenda kinywani, mradi hauvunji sheria...Mdau uliyesema sikuhizi hawataki wageni, wala haujakosea na haya mambo ya ugaidi yanaanza kujitokeza hadi Sweden, kweli tukae tu kwa watu na amani, tusivunje sheria, tutafikishwa pabaya.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...