wapiganaji wa Arusha wakiwa katika ziara
ya kutembelea Kisiwa cha Saa Nane, Mwanza

Wapiganaji wakirejea Mwanza mjini baada
ya kutembelea Kisiwa cha Saa Nane

Mmoja wa wanyama kibao katika kisiwa cha Saa Nane


Na Woinde Shizza,Mwanza

SERIKALI kwa kushirikiana na shirika la hifadhi ya taifa (TANAPA) ipo katika mchakato wa mwisho wa kukipandisha hadhi kisiwa cha Saa nane kilichopo katika mkoa wa Mwanza kuwa hifadhi ya taifa.

Rai hiyo ilitolewa na kaimu mkurugenzi mkuu wa kisiwa hicho Donats Kayona wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kisiwa hicho ili kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika visiwa hivyo

Kwa mujibu wa Kayona, tafiti mbalimbali zimeshafanyika ili kuweza kubaini ni wanyama wa aina gani ambao wataaweza kuishi katika kisiwa hicho kwa kuzingatia mahitaji ya kiikolojia

“Wataalamu kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam wameshafika katika kisiwa hiki na kufanya utafiti wa hali ya juu wa wanyama ambao wataweza kuishi katika kisiwa hiki ili kuongeza vivutio vya utalii na serikali ipo kati mchakato wa mwisho kabisa wa kukipandisha hadhi kisiwa hiki kuwa hifadhi ya taifa” alisema Kayona

Kayona alisema kwa sasa kisiwa hicho kina vivutio mbalimbali vya utalii kama vile mapango makubwa ya kuvutia yaliyozingirwa na miamba Swala, Mijusi ya aina mbalimbali,Kobe,Paka Mwitu, Nyoka Mamba na aina mbalimbali za ndege

Aliwataja wanyama watakaoongezwa mara baada ya kisiwa hicho kuwa hifadhi ya taifa ni pamoja na pundamilia,mbuzi mawe,Swala granti Dikidiki,Kobe na kwamba itachangia kwa kiasi kikubwa kukidhi mahitaji ya watalii wa ndani na nje

Mbali na mafanikio hayo Kayomba alisema kuwa kisiwa hicho kinakabiliwa na changamaoto kadha wa kadha. “Tunakabiliwa na changamoto ya usafiri katika kisiwa hiki kwani watalii wengi hawpendi kutumia boti ndogo jambo ambalo limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kutopata wageni wakutosha kwa kuzingatia kuwa hii ni hifadhi pekee hapa nchini kati ya hifadhi 15 iliyopo ndani ya maispaa ya mji wa Mwanza

Kisiwa cha Saa nane kina ukubwa wa kilimita 0.7 za mraba na kwamba miaka 1964 kilikuwa pori la akiba na ilipofika mwaka 2008 kilikabidhiwa rasmi kwa shirika la hifadhi ya wanyama pori(TANAPA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Sikuwahi kufahamu ya kuwa kisiwa hiki kina Mountain Gorilla

    http://tembeatz.blogspot.com/

    ReplyDelete
  2. Mwandishi, kuwa makini. Huyo bwana ni kaimu mkuu mhifadhi mkuu na sio kaimu mkurugenzi- mbuga za wanyama zina mkurugenzi mmoja tu ambaye yupo makao makuu Arusha. Pia, jina lake siyo hilo, umekosea nadhani anaitwa Bayona.

    ReplyDelete
  3. Hapi besdei mdogo wangu tully usijali maneno ya wabongo kwani kukandiana kuoneana wivu kulogana na kuuwana ndio sifa yao hata kanumba ameshangaa juzi alipo pokewa kama rais nchini rwanda waka nchi kwake kila siku wana mkandia na kumzarau. nakutakia maisha marefu ndugu yangu.
    James

    ReplyDelete
  4. Michuzi nimekutumie issue ya Tanzania Airport Authority umeiweka kapuni na kuwataambia warekebishe website yao. Sio mbaya kuwafahamisha ila ulitakiwa uiweke kwenye mtandao sio kuwapigia simu!!!Kumbe ndio ulivyo.....

    ReplyDelete
  5. Napenda kunukuu huu usemi kuwa "watalii wengi hawapendi kutumia boti ndogo jambo ambalo limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kutopata wageni wa kutosha."

    Mimi ni mtafiti katika masuala ya tabia za watu zinazotokana na tamaduni zao. Suala linalotajwa hapo juu linahusika moja kwa moja na yale ninayotafiti. Ninaangalia, kwa mfano, kwa nini waSwahili hawaogopi kutumia hizi boti, kama inavyoonekana hapa kwenye picha.

    Huku ughaibuni, watu wana ari ya kusikiliza maoni na mawaidha yangu, na ushahidi uko tele huko mitandaoni. Lakini kwa upande wa Tanzania, mwamko wa kutafuta elimu ya aina hii ni kidogo sana, hata miongoni mwa taasisi na watu wanaohusika na hiyo sekta. Nasema hivi kwa sababu nimejaribu kwa miaka mitatu kuendesha warsha kwenye miji kama Dar es Salaam, Tanga na Arusha.

    Matokeo yake, watu wanaendelea kushangaa kwa nini watalii hawafanyi hiki au kile, na hatimaye tutashagaa iwapo watalii hao wataenda kwenye nchi ambazo zinajizatiti kielimu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...