TAIFA STARS IMESHAFUNGWA BAO 3-0 KATIKA KIPINDI CHA KWANZA AMBAPO MLINZI HAROUB NADIR 'CANAVARO' KAJIFUNGA MWENYEWE BAO LA TATU WAKATI MAWILI YA MWANZO YAMEFUNGWA NDANI YA DAKIKA 10 ZA AWALI ZA MCHEZO KATIKA UWANJA WA JIJINI CAIRO. HIVI SASA NI MAPUMZIKO...

MPIRA UMEANZA TENA NA MISRI IMEPATA BAO LA 4

OHOOOOO..... LA TANO HILO!
HADI SASA MISRI INAONGOZA 5-0

RASHID GUMBO ANAPATA BAO KWA TAIFA STARS DAKIKA YA 36 KIPINDI CHA PILI. HIVYO HADI SASA MISRI INAONGOZA 5-1

NA MPIRA UMEKWISHA NA MABAO NI YALE YALE
MISRI 5 TAIFA STARS 1

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. kuna dalili hata 8 yanaweza kufika. sisi tunacheza mpira magazetini, sio viwanjani

    ReplyDelete
  2. Siku zote nikisikia timu yoyote kutoka bongo yaja misiri huwa sina raha.Kwa sabau yajulikana sie ni watu wa kufungwa siku zote tena si goli moja!!! Na kinacho umiza zaidi ni kejeli kutoka kwa wamisiri,mpaka mtu watamani laiti wangekuwa hawakujui kuwa wewe ni mbongo.Kwa kweli ni lazima tubadilike kwa nini sie siku zote ni wakufungwa tuu na wamisiri au wawo kila mmoja ana miguu minne ???!!!

    ReplyDelete
  3. Usilalamike sana kuhusu kufungwa na Misri.Misri wako mbali sana kisoka na kuna mambo mengi sana nje ya uwanja wanatushinda.
    Tatizo letu sisi ni kuwa tunataka kwenda peponi bila ya kufa kitu ambacho hakiwezekani.
    Kwanza kabisa Misri wameizidi Tanzania kiuchumi,Ukiangalia utakuta kuwa klabu za Misri ni tajiri kuliko za Tanzania.Kwa maana hiyo basi klabu zao zinawaandaa wachezaji toka wakiwa watoto.Je vilabu vyote vya Tanzania vina pesa ya kuwa na timu za vijana?.
    Misri wana ligi za watoto na ligi za vijana katika mji wa Cairo na kitaifa.Je Tanzania kuna ligi ya vijana kimkoa,kikanda au kitaifa.?
    Wachezaji wa Misri wengi wanaanzia mpira utotoni wakitoka katika shule za soka.Je wachezaji wa Tanzania wanaanzia mpira katika shule za soka au mtaani tu ambapo mtu akiona maisha magumu anaanza kucheza soka?
    Misri wana league daraja la pili inayoitwa 'The Egyptian Premier League B'.Je Tanzania kuna madaraja mangapi ya ligi,tujiulize kwa nini hatuna daraja la pili? kutokuwa na daraja la pili kunachangia wachezaji wasiostahili kuingia daraja la kwanza na kuondoa ushindani katika ligi.

    Misri ina ligi kuu yenye timu 16 ambapo kwa msimu timu moja inacheza michezo 30.Tanzania ina ligi kuu ya timu 12 ambapo kwa msimu timu inacheza michezo 22.Kwa hiyo wachezaji hawapati mechi nyingi na kwa mujibu wa FIFA ni kwamba mchezaji kwa msimu inabidi acheze mechi 40.Je wachezaji wa Tanzania hucheza mechi ngapi kwa msimu?

    Kwa hiyo wenye jukumu la kukuza soka ya Tanzania ni vilabu vya soka na T.F.F

    ReplyDelete
  4. wewe Tarehe Wed Jan 05, 10:33:00 PM,

    usituletee politics zako za uchimi kwenye mpira , as long tanzania tunaweza kujimudu kwa vifaa basic vya mchezo huo hatuna sababu ya kujitete eti tuna fungwa kwa sababu blah blah blah blah ! nyie ndo mnakubali utumwa eti kwa babu ............

    taifa stars na kama nchi tanzania hina weza ku compete na nchi yoyote
    . sema tu viongozi wetu na wachezaji wetu ni VILAZA FULL STOP .


    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  5. Kwenye msimamo wa FIFA timu za mpira wa miguu wanaume, Misri iko top 10,iko nafasi ya 9.
    Tanzania ya ngapi vile.. 100+
    Hivyo bila nia dhabiti, kuwafunga Misri bado

    ReplyDelete
  6. Jamani ndugu zangu hebu tuwe wa kweli hizi siasa za misri wanapesa sijui nin tuziache maana ukweli utabaki pale pale timu yetu haiandaliwi kuwa timu ya muda mrefu bali ni timu ya msimu angalia wenzetu hao nimeanza kumuona Aboutreka karibu muda sasa na wengine wengi haya sisi hiyo timu ikirudi itavunjwa na kuchukuliwa wapya kabisaaa na hivi kuchanganyana kwa mabeki na kipa ni kukosa pesa pia wadau???halafu TFF siwaelewi hivi muda alipokuwepo maximo kwanini wasipeleke makocha wazawa hata watatu chuoni wangekuwa wameishamaliza haya amekuja Poulsen wangekuwa hata wasaidizi akitoka huyu wangeshika mikoba ila tff mmmh kazi tunayo

    ReplyDelete
  7. Naungana mkono na Phiri na Papic kutotaka wachezaji wao waende huko.
    Acha waende hawa wengineo..wapate exposure..

    ReplyDelete
  8. Tatizo kubwa ni viongozi TFF sio wabunifu, vilabu huwa vinafuata maelekezo yao. TFF ndio iliyovunja ligi daraja la kwanza. ligi hii ilikuwa nzuri ya kuchuja wachezaji wanaotoka ligi za chini kabla hawajaenda premier ligi.

    hatuna ligi inayotambulika ya vijana zaidi ya kucheza kikanda mechi chache za copa coca cola.

    Kusomesha makocha ingekuwa ni priority mojawapo, lkn angalia mtu kama Kayuni ambacho ndio mshauri wa ufundi anashauri nini kama haya ya kawaida hayaoni?

    Tenga na Ndolanga wanatofautiana kidogo sana, kipindi cha Ndolanga migogoro ilikuwa mingi tofauti na sasa. lkn wote sio creative.

    mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali angefanya ukaguzi sahihi kwenye zile sh millioni 4 za FIFA zitolewazo kila mwaka kuendeleza ligi za wanawake na vijana tuone matumizi yake yakoje

    ReplyDelete
  9. Siku zote mtoto yake nepi,sikio halizidi kichwa mkubwa mkubwa tu,Mimi sishangai kufungwa 5 na Misri hata hivyo tumeulumiwa kufungwa 5,Kocha sasa imefika wakati mpango wa kubadilisha timu kila leo nalonitatizo, timu ilitakiwa kuwa ile ile ya Chalengi, ila yeye anachukua wachezaji wengine kila siku itakuwa hivi hivi Tenga na Wenzako kazi munayo kurekebisha soka la bongo.

    ReplyDelete
  10. Lakini sio vibaya hiyo ni zawadi kwa katibu mkuu mpya na msemaji mpya wa TFF,wamekaribishwa vizuri kwa 4 o'clock.

    ReplyDelete
  11. Jamani kuna mdau hapo kasema ligi daraja la kwanza imevunjwa!, hii ni kweli? Mimi sina habari na sitaki kuamini TFF inaweza kufanya ujinga huo!!!!! Hivi ni kweli Ligi daraja la kwanza imevunjwa??? Sababu inaweza ikawa ni nini?????

    Mimi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...