Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, amevunja Kamati Kuu pamoja na sekretarieti ya chama hicho inayoongozwa na Katibu Mkuu, Yusuf Makamba.

Hatua hiyo imechukuliwa usiku huu na Mwenyekiti wa chama hicho,Rais Jakaya Kikwete kutokana na hali ya chama hicho kuwa mbaya katika swala zima la utendaji.

Hali bado ni tete mjini Dodoma ambako ndiko kunakoendelea kufanyika vikao vya chama hicho vilivyotanguliwa na sekretarieti na baadae Kamati Kuu.

Uamuzi huo mzito uliotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho,Rais Jakaya Kikwete usiku huu kutokana na kufanyika kwa mambo ambayo hayakinufaishi chama zaidi zaidi yanakididimiza chama.

Hivyo ili kuhakikisha chama kinatakiwa kusimama imara na kuwa na watendaji wazuri katika chama hicho,imebidi Mwenyekiti wa chama achukue uamuzi huo ili kuhakikisha mambo yanakwenda kama yanavyostahiki kwenda.

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa chama hicho,Yussuf Makamba hakutaka kuzungumzia lolote zaidi ya kusema kwamba "Huu ni wakati wa kulala na si wa kuzungumzia swala lolote".

Hivyo Globu ya Jamii inaendelea kutega sikio lake huko Dodoma na itaendelea kukujuza kila kitakachokuwa kinajiri toka mkoani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hayo ndio mambo. Mkiendelea hivyo tutarudisha imani kwa ccm na tutaachana na chadema na CUF. Bado mafisadi tu ndio mmewaonea haya.
    Yona, Mramba na Mgonja wametolewa kafara tu lakini wapo wengine wengi mlowaacha. Wakamateni muwafikishe kotini muwafunge. Hapo tutaamini mbadilika.

    ReplyDelete
  2. Jamani, Mwenyekiti wa CCM hana madaraka ya Kikatiba ya kuvunja Kamati Kuu au Sekretariati ya CCM. Ni NEC na Mkutano Mkuu tu wenye uwezo huo. Kwa vile tunajua kuwa hakuna Mkutano Mkuu wa CCM umeitishwa ni wazi chochote kilichotokea ni kazi ya NEC na si ya mtu mmoja - Mwenyekiti. Hii hata hivyo haiondoi uwezekano kuwa Mwenyekiti ambaye ni Rais alitoa "shinikizo" kwa NEC kutaka wachukue hatua fulani.

    Hata hivyo NEC hiyo hiyo itatakiwa kuunda upya na wakipenda wanaweza kurudisha watu wale wale. Kwa hiyo tunachosubiria kuelewa zaidi ni kina nani wataingizwa kwenye vyombo hivyo. Tuvute pumzi.

    ReplyDelete
  3. Ninahisi amechelewa sana kuchukua hatua hii muhimu. Alitakiwa aichukue hatua hii zamani sana. Uovu umezidi sana na kwa kweli hali ni mbaya. Ingawa amechelewa sana lakini nampongeza.

    Kaka Gee.

    ReplyDelete
  4. WOTE MNAKARIBISHWA CHADEMA::KARIBUNI

    ReplyDelete
  5. This is a good news for Tanzania. Lets rebuild our the party we love. No Makamba please, at least we should praise JK for being bold this time around. May God Bless Tanzania.

    ReplyDelete
  6. Good!

    Well done Mr President.. it's about time people took responsibility for their actions.

    Eti huu ni wakati wa kulala.. So typical of our African leaders. Wakati viongozi wa mataifa mengine wanakesha kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi wao, yeye anawaza kulala?! Wakati wanajamii wanahitaji feedback na hali halisi ya status quo yeye ni "kulala" tu hadi anadiriki kutoa such a blunt response?! Akumbuke kwamba walipa kodi ndio waliomweka hapo na anapaswa kuwatumikia na si kuwadharau. I wish viongozi wetu wangeika mfano kwa mataifa yaliyoendelea ambako transparency (ukweli na uwazi) ndio msingi wa maendeleo.

    Let's take a lesson at how the Democrats and Republicans in the US worked with the public and the media and managed to avert an impending government shutdown in the recent budget saga.. which (ironically) took nearly a whole night to resolve!

    Sijui politics zetu zitaimprove lini tu kwakweli! It's almost 60 years now since we gained our independence from the British and the system is twice as much almost worsening.. uvivu umekithiri, kutokuwajibika kumejaa na corruption ndio kwanza inapamba moto.

    We need to wake up!

    Mzalendo - UK

    ReplyDelete
  7. Good!

    Well done Mr President.. it's about time people took responsibility for their actions.

    Eti huu ni wakati wa kulala.. So typical of our African leaders. Wakati viongozi wa mataifa mengine wanakesha kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya wananchi wao, yeye anawaza kulala?! Wakati wanajamii wanahitaji feedback na hali halisi ya status quo yeye ni "kulala" tu hadi anadiriki kutoa such a blunt response?! Akumbuke kwamba walipa kodi ndio waliomweka hapo na anapaswa kuwatumikia na si kuwadharau. I wish viongozi wetu wangeika mfano kwa mataifa yaliyoendelea ambako transparency (ukweli na uwazi) ndio msingi wa maendeleo.

    Let's take a lesson at how the Democrats and Republicans in the US worked with the public and the media and managed to avert an impending government shutdown in the recent budget saga.. which (ironically) took nearly a whole night to resolve!

    Sijui politics zetu zitaimprove lini tu kwakweli! It's almost 60 years now since we gained our independence from the British and the system is twice as much almost worsening.. uvivu umekithiri, kutokuwajibika kumejaa na corruption ndio kwanza inapamba moto.

    We need to wake up!

    Mzalendo - Buckinghamshire

    PS. Michuzi, naomba uwatahadharishe vijana wako wasiibanie hii please. Otherwise we're going to have a "word" when I come over!

    ReplyDelete
  8. Thats real sound good to everyone who like our Tanzania. But pamoja na hayo siamini ng'o CCM na serikali na mfumo wake. Eti tunajitahidi kutuma gari au mizigo kutoka huku Ughaibuni na ni maendeleo ya nchi huo uongozi wa bandari na TRA wanatuzungusha kisa kuna tajiri kapenda hilo gari na hawa viongozi wanakusumbua ili wawauzie matajiri oh utaambiwa boss anayehusika kaenda kula njoo kesho, kesho ukienda unaambiwa ooh yupo kwenye kikao njoo baada ya 2days siku zinaenda na ushuru unanogezeke. Cha kuchekesha zaidi ndani ya gari umetilia begi lenye nguo za zamani wana pigia hesabu ya milioni na cha aibu kubwa eti hawafuati bei ulionunulia wana yakwao hata kama unarisiti na aliyekuuzia wamemtumia email kuhakiisha bei bado hawaaini. Yaani nina hasira nao maana wanarudisha maendeleo nyuma au wanatufanya tutumie nchi za jirani wao wafadike na si Tanzania halafu wanasema hela ya serikali sasa sijui hizi hela zinafanya nini kwa nchi yetu ikiwa yatima na wajane serikali haiwasaidie barabara zenyewe na bandari ovyo.Uonevu umejaa kwa serikali na ndo maana viongozi wengi hata wakiwa na mali hazdumu maana zina unajisi hata watoto wao hawafiki mbali vile mnawalisha fedha za uonevu. Biblia inasema apandacho mtu ndicho avunacho but mind yoursef mavuno siku zote ni mengi kuliko mbegu.

    ReplyDelete
  9. Welldone, Bado UVCCM, na Mafisadi!

    ReplyDelete
  10. Ni hatua muhimu. Ila bado kabisa. Mhe anatakiwa aende mbele ya kubadili uongozi. Nchi hii inahitaji ujasiri wa kuondoa mafisadi wote na kuwashitaki. Kila mtu ale kwa jasho halisi na ndipo maendeleo tutapata. Mhe hao marafiki watose please. Tanzania kwanza, urafiki baadae. Lets put the first things first.

    ReplyDelete
  11. kingangitiApril 11, 2011

    Asee ankal amenifurahisha sana Makamba alipojibu kwamba ni wakati wa kulala sio wa kuongea lolote.Makamba wengi tunamjua na chati yake ilikuwa nzuri tu alipokuwa RC wa Dar na hata ukatibu wenyewe wa CCM amejikaza pamoja na wakati mgumu chama kilimojizamisha.Anyway wengine wangekatasimu kabisa lakini hili la kujibu tu Tulale mwajameni safi...!
    Na Vitabu vyote vya Mungu yuko mahili sana kunukuu hasa Biblia.let Try again CCM...On the max..go!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...