Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na baadhi ya marais wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika AU akimpongeza Rais mstaafu wa Brazil Lula Da Silva kwa hotuba yake aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 17 wa Wakuu wa nchi za AU uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Sipopo,jijini Malabo,Equatorial Guinea leo. Hotuba hiyo ya kusisimua ilitilia mkazo kwa nchi za Afrika kushirikiana ili kujiletea maendeleo na kuepuka misaada yenye masharti inayolididimiza bara la Afrika katika lindi la umaskini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2011

    Please tuwekeeni iyo hotuba hapa jamvini ili nasi tuipitie.Maneno matupu hapana.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 30, 2011

    Ati misaada ya masharti. Sasa Africa usipowapa masharti na hiyo misaada si watazimaliza hizo pesa zote kwa kununua magari (ushamba) na kujenga majumba makubwa (Tamaa) na kuwa na nyumba ndogo kila kona (Upungufu wa mawazo) na kuzaa hovyo (kukosa hekima)? Mdau-USA

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 30, 2011

    WEE UNAE JITA MDAU WA USA ACHA USHAMBA NENDA SHULE KWANZA INAONYESHA WEWE HAPO ULIPO UMELETWA NA EXHIBITION KUFUMBA NA KUFUMBUA UKO US,MASHARTI YANAYO ZUNGUMZIWA NA KICHWA HICHO SIO UNAYO FIKIRIA WEWE HAMNAZO,IMF MASHARTI YAKE NDIO YAILIOTUFIKISHA HAPO TULIPO TUMELAZIMISHWA KUUZA MASHIRIKA NA VIWANDA VYETU HATA VILE VILIVYO KUWA VINAFANYA VIZURI,BRAZIL,VENEZUELA NA NCHI ZA FAR EAST ZIMENDELEA BILA IMF NA MASHARTI YAO.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 30, 2011

    We Anon wa Jun 30,06:31 umenena kweli kweli.... Eti unaelewa mtoto wako ni mlevi na anachelewaga kurudi nyumbani unampa gari unamwambia nenda ufanye unavyotaka. My analog could be harsh, but as a whole Africa has failed to demontrate on the international stage that it can get out of poverty cycle, corruption, infighting etc.

    Kwahiyo masharti yako justfied...otherwise tusiombe mikopo na tujitegemee

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 01, 2011

    Mi nafikiri we anon uliyeandika kwa capital letters ndo unahitaji kwenda shule, well niseme unahitaji kuelimika kwasababu Bongo shule tunaenda tunapata A tupu lakini bado we we act kama vile hatukwenda.

    Mi nakubaliana na mdau USA, kwasababu swala ni kwamba hatukuhitaji kuchukua mikopo in the first place. Na kama hatuwezi kutumia hiyo mikopo inavyotumika, basi itabidi tukubaliane na masharti yake. Ni sawa na anon aliyesema unajua mtoto wako ni mlevi na mchelewaji jioni unampa gari lako unamwambia nenda tu mwanangu..

    C'mon tumezidi sisi na kuomba omba, kulalamika, na kutafuta visingizio its about time we stand on our two feet..

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 01, 2011

    Humu duniani kweli wajinga haweshi.Hawa wanaosema huwezipewa misaada bila mashart sijui wanaishi dunia gani.Swali dogo tu hivi mnamjua Lula ni nani? Kwa taarifa zenu tu IMF ni wezi wakubwa na mashart ya misaada yao ndo kikwazo.Mifano mingi ipo ila kwa uchache angalieni nchi kama Uturuki na Malaysia zimeendelea mara baada yakujitoa IMF nakukataa mikopo yao.Mfano uturuki ilikua inadaiwa dola km 24m.na hao IMF mpaka mwaka2001 ulizeni tangu walipojitoa nakuanza kulipa deni limebaki kiasi gani na hali yao kiuchumi ikoje?Msiwe watumwa wafikra mkaona kila cha mzungu mali mtakula mavi ya mzungu pia.Hao ndo wanyang'anyi wakubwa kama hamjui msiibuke tu nacomment zenu zakipuuuzi na si kila anaejua kutumia pc basi aandie comment.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 01, 2011

    sasa nimeamini nyerere alikuwa na matatizo yake katika kuiongoza Tanzania lakini hili shirika la fedha la dunia alilishtukia muda mrefu na kukwaruzana nao na alipoona nchi inakwenda ovyo akahiari nchi ampe Mzee ruhsa awakaribishe hao wezi lakini yeye hayumo.

    mdau.
    myanmar.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 02, 2011

    Hizo IMF na World Bank ni mikonga mikubwa ya wakubwa. Kiongozi mwenye walinzi wa kike au Bwana Pamba aliwagutukia pia miaka mingi. Hilo kosa wanamchukia sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...