JB akipika chapati kwenye moja ya scene katika filmu ya SENIOR BACHELOR.
Richie Mtambalike akiwa na production manager Said Barafu

Na timu ya Globu ya Jamii, Tanga
Filamu ya Senior Bachelor imepangwa kufunga pazia la wiki ya maonyesho ya wazi ya filamu yanayoendelea katika viwanja ya Tangamano Mjini Tanga.

Filamu hiyo ambayo itaonyeshwa Jumamosi hii katika Tamasha la Grand Malt la wazi la filamu linaloendelea viwanjani hapo imeongozwa na Single Mtambalike(RICHIE) na  production manager ni Suleiman Said Barafu.

 Akiongea nasi Musa Kissoki Mkurugenzi wa Sofia Production waandaaji wa Tamasha hilo amesema anaamini filamu itasisimua wengi kwenye maonyesho hayo hasa kutokana na uigizaji wake.

"JB ni moja ya waigizaji wenye mbwembwe sana, hivyo hii imetoka kuwa moja ya kazi zake nzuri ambazo tutazionyesha katika tamasha hili la GrandMalt la wazi la filamu Tanzania.

MUIGIZAJI wa filamu hiyo Jacob Stiven maarufu kama JB amejizolea umaarufu kutokana na filamu hiyo hadi kupelekea kupachikwa jina la Erick Ford alilotumia katika muvi hiyo.

Senior Bachelor ni moja ya filamu pendwa kuonyeshwa katika Tamasha hili
JB anatarajiwa kuwepo mjini Tanga kufungua filamu hiyo katika hadhara kwa ajili ya maonyesho yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 30, 2011

    mchomba vipi na kujichokonoa miguu ama ana funza ! LOL
    mdau paris

    ReplyDelete
  2. Kaka, huyo jamaa wa kushoto ni BAUNZA?

    Khaah!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 01, 2011

    wasanii wa nyumbani mambo ya fangazzzzzzzzzz lol

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...