Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami akiwa katika mazungumzo na kiongozi wa kundi la wafanyabiashara kutoka Japan waliomtembelea ofisini kwake jijini dsm leo. Wafanyabiashara hao wameonesha nia ya kuwekeza katika maeneo mbali mbali nchini.

Kutoka kulia waliosimama ni Balozi wa Japan hapa nchini Bw Hiroshi Nakagawa na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami wakiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji kutoka Japan na Viongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami, amekutana na kundi la wafanyabiashara kutoka nchini Japan liitwalo Maruben lenye nia ya kuwekeza katika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Ujumbe huo umeongozwa na mwenjeji wao, Balozi wa Japan hapa nchini Bw Hiroshi Nakagawa aliyewahakikishia wafanyabiashara hao kuwa, Tanzania ni nchi nzuri, yenye amani, utulivu na watu wenye nia thabiti ya kujiletea maendeleo.

Akizungumza na ujumbe huo, Waziri Chami amesema, Tanzania inaona furaha kuendelea kushirikiana na Japan katika maeneo mbalimbali kutokana na uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya nchi hizi mbili.

Aidha,Dkt Chami amawakarisha wawekezaji hao kuja nchini na kushirikiana na watanzania katika kutumia vyema rasimali zilizopo kwa faida ya pande zote. Maeneo ambayo wawekezaji hao wameonesha nia ya kuwekeza ni pamoja na Nishati, Miundombinu na miradi ya kiuchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2011

    tunaomba hawa wawekezaji wawekezeee kwenye mradi wa kutengeneza umeme na kusambaza maji vijijini na mjini siooo waje huku kariakoo kuja kuuza bidhaaa zao za kichina yaani baada ya kuwekeza katika kuzalisha bidhaa hapa na kupeleka nje sisi tunawekeza katika kuletewa vyoo,maua na kubeba mizigo kuuza yeboyebo au viatu vya sandals na kadhalika dahhhhh..harafu jamaa wakiwekeza kwenye kampuni unakuta mtanzania hakuna hata mmoja kwenye senior level zaidi ya waooo tuuuuu ambayo inakuwa inazidi idadi ya wafanyakazi wanahoitajika katika kampuni!ivii jamani uhamiaji wanajua ni wageni wangapi wanafanya kazi tanzania bila vibali mhhhhh mhhhh jamani workpermit wenzetu upati nje au china bila kuwa skills lobaour hapa dahhhhh harafu tunataka chumi upandeee tutaweza kweli wakati idadi ya watu wasioo kuwa na ajira inaongezeka kila siku na ndioo sehemu mojawapo ambayooo inaonyesha kama nchi inakuwa kiuchumi jamani!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...