Licha ya kuwa vyombo vya habari vinakemea udhalilishaji wa watoto lakini mama huyu alipatikana akiwa amembebesha ngunia mtoto huyu huku wakitembea masafa marefu,usoni unaweza kumuona mtoto huyu alikuwa akiumia kwa ukubwa wa mzigo huu lakini hakuwa na jinsi ya kuushusha. jee unafikiria Ankal hii ni haki ???kwani nini asibebe yeye mkubwa ??

mdau mpenda haki ya watoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. UNAWEZA KUPIMA UZITO KWA MACHO? NA KWA NINI USIMUULIZE MWENYEWE?

    ReplyDelete
  2. Huyo lazima atakuwa mama wa kambo. Huwezi kumbebesha mtoto ulomzaa mwenyewe kilo 30. Hizo ni lazima ni kilo zisizopungua 30. Haya watetezi wa haki za binadamu mpo. Inabidi itungwe sheria ya kunusuru hawa malaika. Kuna mi mama inawageuza watoto watumwa wao.

    Look at her. She soo innocent. poor kid.

    ReplyDelete
  3. Hiyo sio haki hata kidogo,lakini wewe ulifanya nini kumsaidia huyo mtoto?Zaidi ya kumpiga picha.U should have done something to help her.

    ReplyDelete
  4. NADHANI NINGEKUWA MIE NDO MPIGA PICHA HII BASI NINGETUNDUA MKANDA MMOJA YA HAPO KUSHOTO MWA PICHA HII NA KUMCHARAZA HUYO DADA VIBAYA SANA.

    ReplyDelete
  5. Mzigo mzito mpe mnyamwezi.

    Hata hivyo hatujui ni kilo ngapi amabeba. Unaweza ukute hata kilo tatu haifiki. Tusilaumu kwanza.

    ReplyDelete
  6. Huo sio mzigo mzito jamani, kwa kumtazama mtoto mwenyewe usoni tu waweza tambua yeye yupo poa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...