Wana chadema tuliopo jijini Turini nchini Italia Tunaungana na watanzania wenzetu woote kuhudhunika kwa janga/msiba mkubwa ulio likumba taifa letu. Ndugu watanzania ni msiba mzito kwani tumepoteza wazazi weetu naam mama zeetu, baba zeetu, kaka zeetu , dada zeetu na wadogo zeetu Eh Mungu wa Rehema uwarehem milele amina.

Tunatoa pole kwa wale woote walioguswa kwa njia moja au nyingine na hili janga kubwa duniani. Tunatoa pole kwa serikali ya nchi yeetu iliyopo madarakani. watanzania poleni saaana.

Kwa kuzuia majanga ya aina hii kwa mda ujao , tunaiomba serikali kuimarisha ukaguzi wa vyombo vya usafiri sio tu baharini bali pia na nchi kavu na anga ili kupunguza majanga ya aina hii. Mungu ni mwema , tukiweka mikakati madhubuti tutafanikiwa.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WAPE UIMARA NA NGUVU KUPITA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU WALE WOOTE WALIOGUSWA NA MSIBA HUU.

AMEN!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. WanaChadema Turin Italia. mmetoa rambirambi tu hamjasema kama mnachangia akaunti iliyofunguliwa na NBC Zanzibar. Au ndio mnatuonyesha kuwa mpo? hata hivyo wangapi? ngoja na sisi wana CCM Turin tutume rambirambi zetu

    ReplyDelete
  2. Huu ndiyo ubaya wa kuwa na vyama vya kisiasa ughaibuni,badala ya kuwa na hoja za maana na kuzingatia kuwa sasa tupo katika janga la kila mtanzania, unakuta watu wanavutia vyama vyao.CCM /CHADEMA ..etc Naelewa vizuri kuna watu ughaibuni wanatumia nafasi ya vyama ili wajitengenezee ngazi ya kuwa viongozi wa siasa wakirudi Bongo.Watu kama hawa daima hawana nia yoyote ya kusaidia nchi lengo lao ni (.......)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...