Na Mohammed Mhina
Serikali imesema inafanya mazungumzo na muungano wa Shule za binafsi hapa nchini (TAMOSO) ili kuangalia upya viwango vya ada vinavyotozwa kwa wazazi na walezi wenye watoto wanaosoma katika shule za msingi na sekondari.
Akizungumza wakati wa mahafali ya saba ya wahitimu wa elimu ya msingi kwenye shule ya St. Theresa Ukonga Jijini Dar es Salaam, Afisa Elimu Mkuu, Idara ya Elimu ya Msingi nchini Bw. Clarence Mwinuka, amesema hatua hiyo itasaidia kuweka uwiano sawa wa viwango vya ada ili kuwapa unafuu wazazi na walezi wenye watoto wanaosoma kwenye shule hizo.
Bw. Mwinuka alikuwa akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Mh. Philip Malugo, wakati wa mahojiano maalum na Mwandishi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi nchini ambaye pia ni Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina.
Amesema kuwa kutokana na kutofautiana kwa ada kati ya Shule moja na nyingine, Serikali inaendelea na mazungumzo na muungano wa shule hizo ingawa amekiri kuwa shule za binafsi zimekuwa msaada mkubwa kwa serikali katika kukuza kiwango cha elimu kwa Watanzania.
Amesemesa pamoja na msaada huo, lakini bado wananchi hasa wazazi na walezi hasa wale wa kipato cha chini wameonekana kubeba mzigo mkubwa zaidi katika kuchangia elimu kwa watoto waliopo kwenye shule hizo za binafsi hapa nchini.
Amesema  majadiliano hayo yatakapokamilika Serikali inaweza kuweka viwango sawa vya ada kwa shule binafsi za msingi na za Sekondari ili kila mzazi aweze na  fursa na kupeleka motto wake katika shule anayoipenda.
Hata hivyo Bw. Mwinuka amesema kuwa Serikali inaendelea na mikakati yake yakuziboresha shule zake za Msingi na Sekondari kwa kukuza viwango vya taaluma ya walimu na kuboresha mahitaji na miundombinu muhimu katika shule zake ili kusiwe na tofauti ya elimu unayotolewa katika shule binafsi na zile za Serikali.
Awali Mkuu wa Shule hiyo Sr. Amelbberga Rwezahura na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Bw. Wilfred Kipondya, walisema kuwa shule hiyo ina malengo ya kuhikia hatua ya juu ya utoaji wa elimu ya msingi hapa nchini kwa kuboresha miundombinu na kuhakikisha kuwa wanajenga mabweni kwa watoto wote ili kuondoa gharama za nauli na usumbufu kwa watoto kusafiri masafa marefu kwa madaladala.
Shule ya St. Theresa iliyoanza na idadi ya wanafunzi 20 wa darasa la awali, mwaka 1998 imefikia hatua hiyo baada ya mawazo na fikra za aliyekuwa Mwalimu Mkuu mwanzilishi Sr. Pepetua Mhana, za kuindeleza shule hiyo.
Sr. Mhana ndiye aliyeanzisha ujenzi wa jengo la shule hiyo yenye ghorofa mbili ambazo zinavyumba vya madarasa, ofisi za walimu na vyumba vya maabara ya sayansi.
Hivi sasa shule hiyo ina watoto 638 na imekuwa ikifaulisha kwa aslimia 100 ya watoto wote wanaosoma na kufanya mitihani ya kuingia darasa la nne na kidato cha kwanza.
Naye mmoja wa wanafunzi wanaohitimu mwaka huu darasa la saba shuleni hapo, Batuli Mhina, amesema matarajio yake atakapokuwa Sekondari atasoma kwa bidii hadi kufikia elimu ya chuo kikuu na lengo lake kubwa ni kuja kuwa Mwandhishi wa Habari.
Amesema anatamani sana kazi ya uandishi wa habari ili aje aielimishe jamii na kuwa sauti ya watoto wanaoishi mitaani kwa maisha ya kuombaomba ili nao waweze kupatiwa elimu na wajipangie malengo yao maishani.
Amesema kama wanawake wakiwezeshwa wanaweza ni vipi watoto hasa wanaoishi mitaani nao wasiwezeshwe ili waweze kupata elimu bora? Kwani amesema watoto ni Taifa la leo na wazazi wa kesho na hivyo kama mama zao wanawezeshwa nao bila kuwawezesha hawatajiweza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. HAO WANAOALIKWA KWENYE HIZO MAHAFALI ZA SHULE BINAFSI KWENDA KUTIA RUBBER STAMP KAMA HUWA WANAKOSAGA CHA KUONGEA WAKAE KIMYA, SIO KUTULETEA UNAFIKI WAO. Nitatoa mfano mdogo tu, serikali imepiga marufuku wazazi kutozwa michango kwenye mashule. Lakini cha ajabu shule za binafsi zinaongoza kwa michango isiyo na kichwa wala miguu. Utakuta mbali na kulipa mamilioni ya pesa kwa ada bado mzazi unatakiwa utoe mchango wa jengo tena malaki, mara mchango wa madawati, mara sijui mchango wa genereta na mafuta yake. Basi michango kila kukicha, mwisho wa mwaka michango inalingana na ada uliyotoa. Ndio maana watu siku hizi wanahangaika kupeleka watoto kusoma shule Zimbabwe, Botwsana na South Afrika, Kenya na Uganda kukimbia michango yenu isiyokwisha. Nchi ya michango lol!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...