Timu ya wanawake ya Taifa ya Tanzania (Twiga Stars) imepoteza mechi yake ya kwanza ya michezo ya All Africa Games (AAG) baada ya leo kufungwa mabao 2-1 na Ghana katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Machava, jijini Maputo.
Kwa mujibu wa Meneja wa Twiga Stars, Furaha Francis hadi mapumziko timu hiyo ilikuwa nyuma kwa bao 1-0. Mwanahamisi Shuruwa aliisawazishia Twiga Stars dakika ya 85, lakini Ghana ikapata bao la pili dakika tatu kabla ya filimbi ya mwisho.
Twiga Stars itacheza mechi yake ya pili Septemba 8 mwaka huu dhidi Afrika Kusini. Mechi ya mwisho katika hatua hiyo ya makundi itakuwa Septemba 11 mwaka huu dhidi ya Zimbabwe.
Unaweza kuwasiliana na Meneja wa Twiga Stars kwa nambari +258 840207262
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Good try Twiga Stars. We still are proud of you. Mtashinda mechi zilizobakiGood try Twiga Stars. We still are proud of you. Mtashinda mechi zilizobaki
ReplyDeleteI don't care what people said about Twiga Stars lakini muda waliokaa kambini it's only one month and yet wamewaonyesha kazi Waghana moja ya timu ngumu barani Africa (Black Princess) keep it up ladies.
ReplyDelete