Katibu mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay (katikati) akiwa na balozi wa Canada nchini Tanzania Robert Orr (kushoto) na Mshauri msaidizi anayeshughulikia zoezi la uhamasishaji wa kupiga kura kutoka ubalozi wa Ujerumani Bw. Hans Koeppel (kulia) kwa pamoja wakionyesha nembo kumi ambazo zinapigiwa kura na mataifa mbalimbali kupitia mtandao wa www.humanrightslogo.net ambapo nembo itakayopata kura nyingi itawasilishwa tarehe 23 mwezi huu kwenye mkutano wa Umoja.
Katibu mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay (katikati) akijadili jambo na balozi wa Canada nchini Tanzania Bw. Robert Orr (kushoto) na Mshauri msaidizi anayeshughulikia zoezi la uhamasishaji wa kupiga kura kutoka ubalozi wa Ujerumani Bw. Hans Koeppel (kulia) leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wa uhamasishaji wa watanzania kushiriki zoezi la kupiga kura ya Nembo ya Haki za binadamu.
Katibu mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu zoezi la upigaji wa kura linaloendelea duniani kote kwa ajili ya kupata Nembo rasmi ya Haki za binadamu itakayotumika duniani, Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zilizoridhia mkataba wa wa kimataifa wa Haki za Binadamu inashiriki zoezi hilo kwa wananchi kupiga kura kuchagua nembo inayofaa kati ya kumi zilizopendekezwa kupitia mtandao wa www.humanrightslogo.net kabla ya tarehe 17 mwezi huu.
Balozi wa Canada nchini Tanzania Robert Orr akizungumza na waandishi wa habari na wajumbe mbalimbali waliohudhuria mkutano wa uhamasishaji wa Tanzania (watanzania) kushiriki zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kupata nembo rasmi itakayotumika kimataifa kwa ajili ya shughuli za Haki za Binadamu leo jijini Dar es salaam. Pamoja na mambo mengine balozi huyo amesema watanzania wanaomchango mkubwa katika kupiga kura ili ipatikane nembo moja kati ya kumi zilizopendekezwa na washindi wa tuzo za Amani na wanaharakati mashuhuri wa Haki za Binadamu duniani.Picha na Aron Msigwa – MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...