Kampuni ya mauzo ya nguo, bidhaa za nyumbani na chakula ya Afrika Kusini maarufu kwa jina la Woolworths imeingia ubia na mfanyabishara wa Tanzania Ali Mufuruki na kutangaza mipango ya kupanua mauzo yake nchini Tanzania na Uganda. Bwana Mufuruki aliyekuwa mmiliki wa maduka ya uwakilishi ya Woolworths (franchise stores) nchini Tanzania na Uganda kwa zaidi ya miaka kumi sasa atakuwa mbia kamili wa Woolworths baada ya mktataba wa ubia kupata ruhusa ya tume ya ushindani wa kibiashara nchini - Fair Competition Commission (FCC)

Akizungumza kwenye hafla ya kutia saini mikataba ya ubia iliyohudhuriwa na waandishi wa habari, Mufuruki alisema duka moja jipya litafunguliwa Dar Es Salaam na kufikisha idadi ya maduka yaliyopo hapa Tanzania kuwa manne, mawili yakiwa Mjini Arusha na mengine mawili yako Dar es Salaam. Pia alisema kwamba maduka mawili mapya yatafunguliwa mjini Kampala na kuongeza idadi ya maduka ya Woolworths nchini humo kufikia matatu.

''Tunaamini katika uwekezaji wetu hapa Tanzania, tunafurahishwa pia na mweelekeo wa ukuaji wa biashara zetu.Imani yetu kwa Tanzania na mbia mwenzetu Ali Mufuruki imetuwezesha kufanya maamuzi ya kuwekeza katika upanuzi wa biashara na mauzo'' alisema Mkurugenzi wa Biashara wa Woolworths Bwana Glenn Gilzean.

Tunatarajia ukuaji, upanuzi zaidi wa biashara na mauzo ambayo yatatoa fursa za ajira na kuongeza ujuzi katika mauzo kwa siku zijazo.

Woolworths yenyewe makao yake makuu mjini Cape Town nchini Afrika Kusini ni kampuni ya Afrika kusini inaendesha biashara ya uuzaji wa nguo za mavazi, vifaa vya nyumbani na vyakula katika mfumo wa rejareja, imeorodheshwa kwenye Soko la hisa la Johannesburg (Johannesburg Securities Exchange - JSE).

Woolworths imejikita zaidi kwenye mitindo bora ya mavazi, chakula, bidhaa za nyumbani na huduma za kifedha wakishirikiana na ABSA Bank ya Afrika Kusini. Woolworths ina zaidi ya maduka 400 nchini Afrika ya KusiI na baadhi ya nchi za Afrika, Mashariki ya Kati, pia ni mbia mkubwa katika kampuni maarufu ya nguo iitwayo Country Road ya nchini Australia. Mapato yake ya jumla kwa mwaka wa fedha uliopita ilikuwa Randi billion 25.6 saws na doll za kimarekani 3.3 billion.


Woolworths inao mpango wa kufungua jumla ya maduka 16 katika nchi mbalimbali za Afrika mwaka huu na kufanya jumla ya maduka ya Woolworths barani Afrika bila kujumuisha Afrika Kusini kuwa 60. Nchi zenye maduka ya Woolworths ni pamoja na Tanzania, Botswana, Namibia, Lesotho, Swaziland, Msumbiji, Mauritius, Uganda, Kenya, Ghana, Zambia na Angola.

Nchini Tanzania Woolworths imeboresha huduma zake kwa wateja. Wateja sasa wanayo fursa kubwa ya kuchangua mitindo na bidhaa zinazokidhi mahitaji yao, hii ni pamoja na mavazi nadhifu, mavazi ya watoto, bidhaa za urembo, na mavazi ya kawaida ambayo yanaenda na wakati kwa wanaume, wanawake na watoto. Inajumuisha pia nembo maarufu za "Re:" na "Studio.w" ambazo zilizinduliwa hivi karibuni huko Afrika ya Kusini.

Mfumo wa usafirishaji wa bidhaa (supply chain) na mipango ya uendeshaji imeboreshwa ili kuwezesha Woolworths kumudu mahitaji ya wateja wake kwenye maduka yake nchini Tanzania na Uganda.

''Ninayo furaha kubwa kuwa mbia na kampuni kubwa ya kimataifa na yenye mafanikio kama Woolworths. Sasa tutaweza kujipanga kwa nguvu zaidi katika kukuza soko, nakuwapa wateja fursa ya kuchagua ubora ambao umeipatia Woolworths umaarufu duniani kote'', aplisema Mufuruki.

Aliongeza kusema kuwa kukamilika kwa makubaliano hayo ya kibiashara kupitishwa na kamisheni huru ya maridhiano Tanzania (Fair competition commission) na mfuko wa dhamana Johannesburg, Africa ya kusini.

Wadau wote wanayo imani kuwa makubaliano hayo yatapitishwa na kupatikana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ahsante woolies kwa kufungua duka lingine.ila pia muangalie swala la price ziwe fair ili watanzania wengi waweze kununua bidhaa zenu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...