Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Finland,Maria Kakkala wakati alipofika ofisini kwake vuga,visiwani Zanzibar.Bi. Maria akiongoza ujumbe wa watu sita yupo Zanzibar kuangalia hali ya mazingira katika maeneo mbali mbali.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Finland,Maria Kakkala akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,Balozi Seif Ali Iddi leo wakati alipomtembelea ofisini kwake leo.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea na hadhari na kutafuta mbinu mbadala za kuhakikisha matumizi mazuri ya ardhi na uhifadhi wa mazingira yanazingatiwa na jamii nzima.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameeleza hayo hapo Afisini kwake Vuga wakati akizungumza na Ujumbe wa watu sita wa Finland unaoongozwa na Waziri wa Mambo ya nchi za Nje wa Nchi hiyo Bibi Maria kukkala.

Balozi Seif amesema matumizi mabaya ya ardhi yasiyozingatia Sera wala taratibu yamepelekea Visiwa vya Zanzibar kuwa katika hatari ya uchafuzi wa Kimazingira.

Amesema maeneo mengi hasa yale ya Vijijini yanaendelea kuwa jangwa kutokana na baadhi ya watu kukata ovyo Misitu kwa ajili ya miradi ya Makaa ya Kupikia.

“ Utumiaji mkubwa wa Makaa katika masuala la mapishi majumbani hasa kwa wananchi wa kipato cha chini umepelekea ukatwaji mkubwa wa miti ikiwemo pia Mikarafuu ambayo ni uchumi wa Taifa ”. Alisema Balozi Seif Ali Iddi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ameipongeza Finland kwa Hatua yake ya kuendelea kusaidia Maendeleo ya Zanzibar.

Ameishauri Nchi hiyo kuangalia uwezekano wa kusaidia sekta ya Kilimo na Maji kwa Vile Wananchi walio wengi katika Visiwa vya Zanzibar wanaishi Vijijini.

Balozi Seif amesema Finland kwa kuwa imepia hatua kubwa kimaendeleo inaweza kusaidia Utaalamu kwa Kilimo pamoja na ile ya Mazingira.

Akizungumzia suala la Kisiasa Balozi Seif amesema Utulivu unaoendelea kuwepo Zanzibar umepelekea Viongozi na Wananchi kutekeleza majukumu yao kwa pamoja ndani ya mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ulioanza Bada ya Uchaguzi Mkuu uliopita.

Naye Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Finland Bibi Maria Kurikkala amesema hivi sasa ni wakati muwafaka kwa Zanzibar kujaribu kudhibiti hali ya uchafuzi wa Mazingira ambayo inaanza kuleta athari.

Bibi Maria amesema Finland inaangalia utaratibu wa namna inavyoweza kusaidia suala hilo kwa vile Zanzibar bado haijaathirika sana kimazingira ikilinganishwa na Mataifa mwengine Duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Gender wars. It is interesting to see how the delegates from Finland is represented by women and the Zanzibaris by all male team. Can we learn from this? I think so. Look at where they are and look at where Zanzibar is. Hmmmm!!

    ReplyDelete
  2. Napenda kusahihisha habari hiyo na huyo mwandishi aliyeituma; huyo bibie ni waziri wa maendeleo ya kimataifa anaitwa Heidi Hautala (sio Maria Kurikkala)kama ulivyotaka ifahamike. Waziri wa mambo ya nje ya Finland anaitwa Tuomioja na ni mwanaume sio mwanamke.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...