LEO NI DIWALI, SIKUKUU YA WAHINDU INAYOSHEREHEKEWA MWANZO AMA MWISHO WA MWAKA KILA MWAKA. LAKINI KWA  NDUGU ZETU WANAOISHI MAOLENEO YA MBAGALA, HUSUSAN KARIBU NA KAMBI YA JESHI, IMEKUWA KERO NA TISHIO KWA MAISHA YAO. 

BAADA YA FATAKI NA FASHIFASHI KUANZA KURUSHWA ENEO HILO, WAKAAZI WENGI WAMEKIMBIA MAKAZI YAO WAKIJUA KWAMBA NI YALE YALEEEE...YAANI MABOMU YAMEANZA KULIPUKA TENA. UJUMBE KIBAO WA SMS UMEIFIKIA GLOBU YA JAMII KUELEZEA WAHAKA HUO NA KUBAINISHA KUWA UKWELI SIO MABOMU YA KIJESHI BALI NI SIKUKUU YA NDUGU ZETU WA-HINDU MAARUFU KAMA DIWALI. 

UJUMBE HUO UNASEMA CHA KUSHANGAZA NI KWA NINI ISINGETOLEWA MAPEMA TAARIFA KUWA KUNA MILIPUKO LEO??  NA KWAMBA HUKO MBAGALA WATU WANAKIMBIZANA OVYO, WAKIASHA FAMILIA ZAO HUKU VIBAKA WAKIJISEVIA BILA UPINZANI WOWOTE. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. siyo mabagala tu ankal, hata mwanza raia wanahaha kwa hizo fataki

    ReplyDelete
  2. Ni lazima wapewe adhabu kwa kudharau kutoa taatifa kwa wananchi ambao wanajua fika kuwa bado wana machungu ya kupotelewa na wapendwa wao na mali zao kutokana na milipuko ya mabomu. Kuwa sherehe haimaanishi iwe kero au tishio kwa wengine, ni lazima tushereheke kwa kuwajibika (celebrating responsibly) na kuwazingatia watu wengine.

    ReplyDelete
  3. serikali yetu ni ya kibaguzi, mbona huwa wanatukataza kusherekea kwa namna hii sikukuu ya mwaka mpya?? alafu kwa wahindi inawaachia tena bila hata kutoa angalizo kwa wananchi wake...?? wageni wanathaminiwa zaidi kuliko wenyeji...tutawalamba viatu mpaka lini hawa watu...??? its not fair

    ReplyDelete
  4. Si tabia nzuri kufanya kitu kama hicho bila taarifa. Tanzania ni ya watu wote si kwa rangi dini au hali..hawa na diwali zao wasirudie tena kufanya jambo kama hili bila taarifa. Hii inaonyesha ni jinsi gani baadhi ya watu hawatakii wenzao amani wa mwili na roho.

    ReplyDelete
  5. HUU SIYO UUNGWANA KABISA,WATU HATUKULALA, TUMEHANGAIKA ,TUMEPIGIANA SIMU,WENYE JAMAA ZETU JESHINI TUMEWAPIGIA KUULIZIA JAMBO HILI,WATU BADO TUNAMACHUNGU YA MABOMU YA MBAGALA NA GONGOLAMBOTO,WENGINE TUKAFIKIRI AL-SHABABU WAMEUFATA UBALOZI WA KENYA.KILA MTU ALIKUWA NA LAKE LA KUSEMA,TUMEPIGA SIMU MPAKA HERA ZIKAISHA,TUKAKOPA NAZO ZIKAISHA,ILI TUJUE KULIKONI.KUMBE WAHINDI WANAKULA TAMBUUUU! HUU SIYO UUNGWANA KABISA.KAMA HAWA WATU WALIKUWA NA KIBARI,BASI WAHUSIKA WALITAKIWA KUUELEZA UMMA JUU YA MILIPUKO HII,HAKUNA TAARIFA ZILIZOTOLEWA ,NAOMBA WAHUSIKA WAWAJIBIKE,NAOMBA WANANCHI TULIOPATA USUMBUFU HUU TULIVALIE NJUGA HILI.NAWASILISHA KWA UMMA(MSHIKAMANOO)

    ReplyDelete
  6. nilipata shida sana na watoto maana tupo peke yetu baba yao kasafiri, wananiuliza, mamaa tuambie ukweli, huna la kutuambia, sisi blasts tunazijua, tumeshuhudia za mbagala na g/mboto, kwa hiyo sisi ndani hatukai tunataka kujua ukweli au tuanze kukimbia? jamani, mwenzenu nilipata shida, nilipiga simu kwa zaidi ya watu 30, kila mmoja nasema hajui nikampigia mpaka boss wangu yuko kwao nrb, lakini naye akasema hajui maana nilidhani ni AL-SHABAB! LOL, jamani, najiuliza, hii nchi yetu imeuzwa kwa wahindi? kwa nini hawajali maisha ya watu wengine? mimi naamini kwa case ya jana, subirini kusikia idadi kubwa ya watu waliolazwa mahosptalini kwa ajili ya mshtuko. kwa kweli, hapa nimevua kofia kwa serikali, kumbeee, inabidi kila mtu ajijue kivyake, not fair hata kidogo

    ReplyDelete
  7. Tanzania zaidi uijuavyo,kwa kweli hili sio jambo la kiistarabu,watu wanaishi kwa wasiwasi bila kuwa na taarifa zinazoeleweka,Kama wahusika walijua hili kwa nini hawakutoa taarifa,bado watu wana machungu ya Mbagala na Gongo la Mboto,halafu leo hii unaambiwa ni watu walikua wanasherehekea,Naomba serikali iangalie jambo hili kwa undani sana,kumekua na watu wanatoa taarifa zisizo za ukweli,itakuja kutokea taarifa za kweli na watu wakazipuuza kukaja kuwa na maafa makubwa,Wahusika naomba wawe makini.

    ReplyDelete
  8. michuzi hii habari ,ni mhimu sana na ni kwa manufaa ya jamii,na hii blog ni maarufu kama blog ya jamii,naomba uilete tena front page watu tutoe maoni yetu,mpaka hatua mhimu zichukuliwe au serikali itoe tamko juu ya jambo hili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...