Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi Joyce Mapunjo na Naibu wake Dkt Shaaban Mwinjaka, wakimpokea Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda kutembelea Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara katika siku ya mwisho ya Maonesho ya miaka 50 ya Uhuru Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda katika Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Eline Sikazwe akimueleza Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda mafanikio mbali mbali yaliyofikiwa katika Idara yake.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bi Joyce Mapunjo akimpa maelezo Waziri Mkuu Mh Mizengo Pinda juu ya hatua mbali mbali za mafanikio zilizofikiwa na Wizara yake kwa kipindi cha miaka 50 ya Uhuru.
Piki piki ya miguu mitatu (Bajaj) iliyoongezewa ubunifu na kuifanya iweze kutoa huduma ya kusafirisha wagonjwa. Pichani ni mbunifu wa “Ambulance” hiyo Bwana Ally Dahally akionesha ubunifu wake.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Taasisi zilizo chini yake mara baada ya kufungwa kwa maonesho ya miaka 50 ya katika Viwanja vya Mwl J.K.Nyerere. Banda la Wizara ya Viwanda na Biashara limekuwa kivutio kikubwa kwa wageni kutokana na maandalizi mazuri na bidhaa mbali mbali zinazozalishwa na Viwanda vya Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. HIYO AMBULANCE YENYEWE CHINJA CHINJA. HEBU JAMENI TUWE SERIOUS. AU UNATAKA IKATUMIKE KWA BABU KULEEEEEEE ARUSHA. MAANA MJINI MGONJWA HATOFIKA APELKWAKO. KAMA HAIKUISHIA MTARONI, ITASHIA KWENYE MTI. DEREVA NA MGONJWA WATAPEKWA KWA TAKSI. UBUNIFU WAKO MJOMBA NI SAWA NA PROFESA, KIPEPE LODI LOFA WALOTENGENEZA BAJAJI INYOTUMIA UJI WA UNGA WA MHOGO. TEHE TEHTEHEHEEEE

    ReplyDelete
  2. Aibu kubwa sana, nchi ina umri wa miaka 50 halafu bajaji ndio ambulance!!!!

    ReplyDelete
  3. Ahsante kwa Ukombozi Ndugu Ally Dahally,,

    Mdau wa kwanza ambulance hii itafaa sana kwa hali ilivyo vijijini na sio mijini ambapo tutatumia Magari kwa ambualance na sio kufanya Ukombozi huu kama njia ya kubana matumizi mijini!

    Wabongo kwa kupenda nafuu bwana, mijini tutabaki na magari na hizi Bajaji ambulance itakuwa ni ukombozi sana kwa vijijini ambako hali ni ngumu na nzito yakikufika!!

    Utakuta mgonjwa anapelekwa Kilometa 30 au zaidi kwenye matibabu au mama mjazito kwenda kujifungua kwa kubebwa mgongoni au kwa machela au kwa baiskeli ya matairi mawili ambapo injini ni Uji wa muhogo au shibe ya mwendeshaji!

    Huku njia ikiwa ni ya mifugo hata gari inapita kwa tabu, labda mvua inanyesha, matope kibao, vichaka wanyama wakali, vilima na miteremko vikikusubiri mbele!

    SI BORA YA HIZI BAJAJI AMBULANCE VIJIJINI KULIKO HALI KAMA ILIVYO HAPO JUU ILIVYO HUKO SHAMBA?

    ReplyDelete
  4. huyu jamaa sio mbunifu ni muuaji kweli kabisa abiria wazima ambao wana umwezo wa kujisupport ni mashaka je kwa mgonjwa itakuaje na hao paramedics watakaa wapi acheni hizo yaani bila aibu mtu anajiita mbunifu wakati anahatarisha maisha ya watu kama ni amri yangu ningemfunga kwa mbali na ubunifu.

    ReplyDelete
  5. mdau hapo juu umeniua kwa kicheko. Dah lakini kweli huu sasa ni ujinga.

    ReplyDelete
  6. anony Tue Dec 13, 02:15:00 AM 2011 unajua sana kuponda lakini hauko tayari kuchangia mawazo yatakayopelekea suluhisho. Bw. Dahaly wala usikatishwe tamaa, taratibu hadi utapata suluhisho ni jinsi gani vibajaji vitabeba wagonjwa na kuwafikisha salama hospitali, zahanati au kwenye kituo cha matibabu.

    ReplyDelete
  7. HUYO KAKA ALIYESIMAMA KARIBU NA AMBULANCE ANAONEKANA MTU WA KINYWAJI SAWASAWA. CHAI KWAKE NI TATIZO KAMA POSHO ZA WABUNGE

    ReplyDelete
  8. Maoni haya saba 7 yametoka,

    Hebu tujaribu kutafakari hali halisi tuliyonayo sehemu zote:

    Ambulance za magari hata kwa mjini imekuwa ni mgogoro je kule mahala ambako kunaitwa 'MAHALA PASIPO NA DAKITARI' yaani Vijinini tutaweza?

    Hebu chukua taswira upo Kijijini huko Mibuyu Saba eneo la Sakasaka na unauguliwa na Mgonjwa na anatakiwa kufikishwa ktk kituo cha matibabu kilometa takribani 40 au zaidi itakuwaje?

    Hali yetu kuiwezo hasa Vijijini ni duni miundo mbinu hafifu barabara mgogoro sehemu zingine watu wanatumia njia za ngómbe hata magari kupita mgogoro hapo vipi?

    Mawazo ya Dallaly yasipuuzwe ila yaboreshwe zaidi na iwe ukombozi kamili kwetu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...