Hello Michuzi.
Leo asubuhi mwenyeji wangu MTANZANIA kachukua barua toka box ya nyumbani (street adress) iliyopostiwa toka posta ya hapa johannesburg ikiwa na maandiko/onyo/tangazo/tahadhari hiyo ikiashiria vurugu kubwa.
Nina siku tatu tu hapa, nilikuwa Maputo kama mwezi hivi.
Nilishapata kuishi huku miaka mitano (1997-2002),nawajua hawa jamaa,hasira zao ni lazima wazipeleke sehemu hata kama haitakuwa jibu.
NAOMBA UITAHADHARISHE JUMIYA YA WATANZANIA WOTE KUPITIA BLOGU YAKO NA ILI WAWE MAKINI NA HILI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 53 mpaka sasa

  1. Brother michuzi you need not to post something like this. There are laws in every country and the consequences go to those who break the laws. Post like this just degrade this blog.

    ReplyDelete
  2. Hawa jamaa huwa wanafanya kweli na wala hawatanii.Wana sahau kama africa nzima ilikuwa inawalaani makaburu kwa kuwatetea wao.Sasa na sisi tuwafanyeje waliokuwepo huku?Na wao si wamekuja kuchukua kazi vilevile na wamepunguza nafasi za watanzani ktk ajira?Nibora nirudi kijijini kwetu kuliko kuishi huko maana roho yako unaiweka mikononi wakati wote.Unaishi ndani ya nyumba utafikiri jela na kumbe unailipia.Jamani watanzania rudini haraka.

    ReplyDelete
  3. Wapumbavu hao wamesahau walivyofurika hapa Tanzania wakati wa ubaguzi SA. Sasa wako huru ndio jeuri imepanda.Wahenga wamesema TENDA WEMA WENDE ZAKO.Kuwafadhili kote kule hayo ndo malipo yao.

    ReplyDelete
  4. Ni vigumu kumuelewa mwafrika, tunapigana na kuchukiana sisi kwa sisi hadi lini?
    Wasauzi wako kama vipofu, wamesahau adui wao ni white man, sasa wanataka kuua kaka na dada zao.
    Hivi wana aikili timamu? watakuja kujuta baadaye.

    ReplyDelete
  5. very sad, inaonyesha wazi mwandishi ana uelewa mdogo!!! God bring peace!

    ReplyDelete
  6. dah! hawa mbuzi wameshasahau kwamba tuliwafadhili hapa bongo, maisha yanawashinda wana singizia wageni. sawa sawa na hapa bongo wachina wanatanua sisi tunapiga kelele hatuna ajira

    ReplyDelete
  7. Duuh huu unaonekana kama mkwara mbuzi lakini kwa hao wazawa wa Sauzi inaonekana watalianzisha anytime kwahiyo kwa kifupi Wabongo inabidi wakae chonjo maana inaweza ikawa noma . Inabidi Ubalozi wa TZ ndani ya Sauzi ujue hili swala maana hao jamaa hawana la Mswalie Mtume. Be carefull you guyz .

    ReplyDelete
  8. NAONA UMELEZEA KUWA UMESAFIRI NCHI MBALIMBALI LAKINI UJUWO WA AKILI YAKO NI FINYU KUNA VYOMBO MBALIMBALI UNGEZA KUTUMIA KWA UFAIDA YA WATU WASIOTAKIWA KAMA KUPELEKA BARUA HII POLISI YAAHI KUREPORT AU KUHIPA TAHAFIFA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI SOUTH AFRICA MAANA KAMA UWEKA BARUA KAMA HIZI BILA USHAHIDI WOWOTE NI VIBAYA KWANZA UNATISHA RAIA WA TZ, PELEKA BARUA HII PILISI AU UBALOZINI.

    ReplyDelete
  9. hapo mbombo ngafu,wabongo jipangeni,hao jamaa ni noma,wamepinda ile mbaya,hapo hawatishii,yaani watafanya kweli,wapumbavu ile mbaya hao.

    ReplyDelete
  10. Hilo tatizo dogo tu. Hapa UK walianza miaka mingi iliyopita kuuwa wageni. Wageni walichofanya ni kujumuika pamoja na kuishi sehemu moja, kuweka vilabu vyao. Mzungu akijeruhi mweusi mmoja na weusi nao wanajeruhi mzungu mmoja. Mpaka polisi na serikali wakaingia na sasa wanaweka ulinzi mkali. Huwezi kumgusa tena "minority". Ndio maana wabongo tunajidai sasa.

    ReplyDelete
  11. Afrika Kusini ilipaswa kutawaliwa na makaburu hadi dunia ifike mwisho. Hawa ni watu waliozowea kutawaliwa na si watu wachapa kazi. Ukiangalia historia ya kutafuta uhuru kutoka kwa muingereza ni makaburu ndio waliopigana na kuuliwa wakati huo weusi hawana habari. Sasa wamepewa uhuru imekuwa nongwa. Haraka makaburu chukueni nchi na muwageuze watumwa wote hawa tuone kama watakimbilia wapi. Pumbav kubwa.

    ReplyDelete
  12. WAKIFANYA NA WAO SI WANA NDUGU ZAO BWANA WANAISHI BONGO. MBAYA MBAYONEKE.
    LUGHA HII CHAFU USINGETOA. KWA NINI USIZIBE HAYO MANENO YASIYOTOKA KWENYE MDOMO USOPIGA MSWAKI?

    HICHO KIKUNDI KINAJULIKANNA KWA HII BARUA ISIRIPOTIWE POLISI. INAWEZEKANA MLEVI ANAANZISHA HIYO WATU WATAUNGA BEHEWA NA KUANZISHA VAGI. MIE SIPO.

    ReplyDelete
  13. Fine enough, nawaambiaga watz wanaofikaga kwenye nchi za wenzetu na kujiona wamefika kwa kupata makaratasi wasijiamini sana mtu kwao. Huku Uk Watz wengi mliopata makaratasi mmejisahau, na sasa Cameroon hataki na haelewi. Kuweni makini. Poleni wenzangu ili pelekeni hii barua polisi kwani prevent is better than cure

    ReplyDelete
  14. Du hapo mbombo ngafu naloli

    ReplyDelete
  15. Wa sauzi wavivu na walevi tu hawana lolote,

    Wana wivu wa maendeleo wala msiondoke la muhimu ni kuwa makini tu ktk nyendo zenu huko.

    Hakuna dunia utakaa bila challenge, America walikuwepo Black Panthers,Black Liberation Army (BLA), na wengineo kibao.

    Cha muhimi ni kuwa na silaha za moto kwa kujihami!

    ReplyDelete
  16. hii ni kwa wale wote walioona kutolewa kwa hii msg mtandaoni ni kwenda kinyume na ustaarabu. nyie watanzania acheni kuficha mambo ya msingi, nampongeza aliyepost maana alitaka ujumbe ufike kama ulivyokusudiwa sasa afiche nini? Afiche maneno yanayomaanisha matusi sasa si ataficha barua nzima! Mie naona kila neno lililosemwa hapo ni tusi kwetu watanzania ukiangalia ni kiasi gani tumepoteza kwa kuwatetea, matusi sio lazima yale ya nguoni, ile maana ya maneno mtu anayokumaanisha ni tusi pia. Jamani tujifunze kuukubali ukweli wakati mwingine na muache mambo ya kuficha ficha vitu. hii barua inaashiria hatari jamani, watu wakianza kuuwawa ndio mtajua wanaamanisha nini na naungana mkono na wale wanaoshauri kuwa ipelekwe ubalozini na polisi

    ReplyDelete
  17. Bwana Issa hii post ni hatari kwa blog kwani haijachujwa ina matusi mkubwa ya nguoni natumaini blog hii ina heshima zake kwani inasomwa ulimwengu mzima, matusi na vitisho ni mazito hayakupaswa kuanikwa kwenye blog ya jamii na hayo matatizo ya SA hayajaanza leo kwani kuna watanzania wengi tayari wameshapoteza maisha yao au wamepotea hawajulikani walipo, kama unakumbuka walishamvamia na kuwajeruhi vibaya sana balozi wa tanzania na wageni wake walipokuwa wanafanya sherehe ya kuagwa kurudi nchini. Kwa utaalamu wa uandishi wa habari hukupaswa kuipost kama ilivyo, ninajua you are a very nice and humble man na unataka kumtidhisha kila mdau lakini wakati mwingine lazima uchukue taadhari. Kwa ujumbe wa message hii tungetumiana kwa kupitia email kuliko kuiweka kwenye blog yetu kwani inachafua hali ya hewa hili tatizo lipo na linaendelea SA na watanzania wote waishio kule wanajua nini kinachoendelea na wanachukua tahadhari kila siku.
    Asante ankal unaweza usiipost hii ni ushauri tu binafsi. Ndimi mdau USA

    ReplyDelete
  18. mmmmh nilikuwa nataka kwenda huko januari sasa basi. Hawa jamaa noma.

    ReplyDelete
  19. hapo ndo huwezi kuja kumwelewa mwafrika maisha,wasouth hawa hawa sasa wanannza kutafuta mchawi nani wakati ni wao wenyewe hawataki kufanya kazi zaidi ya kufanya crimes kila mahali.wamekabidhiwa nchi na makaburu wanashindwa kuiendesha wanaanza kushusha lawama huku kwa ndugu zao waliohamia.na walivyo mabwege hawa watafanya kweli nyie subirini muone.wakilianzisha na nyie lianzisheni huko bongo.

    ReplyDelete
  20. Ooops TZ tulijisifu kwelikweli kwamba tumesaidia our BROTHERS and SISTERS wa SA ili wajikomboe,tukatoa ardhi yetu ili wafanikiwe,lakini leo hii wanatuona TUNAWAZIBIA,kweli CHANGU CHAKO,CHAKO CHAKO,rudini nyumbani bana kwani kitu gani.

    ReplyDelete
  21. Well Well, this also has happened in US as Black Americans see African Americans (Africans from Africa) as a threat to their Jobs and Opportunities.

    Anyway be careful TZAns in RSA those people are really rude.

    ReplyDelete
  22. Ni muhimu barua hii ifikishwe polisi haraka iwezekanavyo. Na kwa haraka haraka hiki kiingerea na "attitude" ya aliyeandika, inanifanya nidhanie kwamba inawezekana kabisa barua hii imeandikwa na mzungu kaburu. Kuna alama za "ukaburu" kwenye hi barua.

    ReplyDelete
  23. Kaka Michuzi angalia lugha iliotumika. Sio ya kupost kwenye blog ambayo inatumika na watu wa rika zote! Watoto huingia humu kwenye blog yako...Uwe makini...

    ReplyDelete
  24. Hivi unawezaje kuishi South Africa kwa miaka 8,9,au 10 na bado ukaendelea kuwa mgeni? Mwafrika yoyote m-bantu anayeishi South Africa kwa miaka yote hiyo anatakiwa aweze kuzungumza lugha za South Africa katika lafidhi ya wenyeji. Lugha yoyote ya kibantu ni rahisi sana kwa m-bantu kujifunza, na utaweza kuizungumza kwa lafudhi ya wazawa. Ukizungumza ki-Xhosa, au Zulu, au Sesotho; utajulikana vipi kama wewe ni muhamiaji? Ni vigumu kuchanganyika na wazungu kwa waafrika walowezi wa ulaya na pengine hakuna sababu yoyote ya kutaka kuchanganyika na wazungu; lakini kama unaamia nchi nyingine ya Afrika na ukaendelea kujitenga kama mgeni basi haya ndiyo matokeo yake.
    Hapa Bongo wanakuja wazaire wanaongea "Ile bitu ya bukavu iko na kifukutho juu yangu, nasema eti mimi napenda fanya ile kitu, nayionyesha";.
    Wakishakaa hapa Bongo baada ya miaka mitano mtu yuleyule utamsikia akizungumza sentesi ile ile kama ifuatavyo "Achana na watu wa bukavu, eti wanasema kwamba mimi napenda kujionyesha".

    Huwezi tena kumjua yeye kama ni mzaramo au mkongoman.

    ReplyDelete
  25. KARIBU SANA SA KWA MARA NYINGINE TENA WEWE ULIOKUWA MAPUTO ILA ACHA KUTISHIA NYAU NA BARUA YAKO YA UONGO USITUDANGANYE NA WALA USIPOTOSHE WATU KATIKA NCHI ZILIZOORODHESHWA KATIKA BARUA YAKO NCHI KAMA KENYA,TANZANIA WASAUZI ASIMILIA KUBWA HAWAZITAMBUI KIASI KWAMBA WATAKUITA MNAIGERIA.BARUA INGEKUWA YA UKWELI NIGERIA LAZIMA INGEORODHESHWA IKIWEMO ZIMBABWE NA MSUMBIJI.

    ReplyDelete
  26. Hii story ni between 2people moja wamegombana may be ktk biashara au wanawake.kwanza wazimbabwe tu wapo 10 million hapa utawamalizaje wa popo wapo 1 million mozambique milioni pia huu mziki mkubwa hivi vitu tumevizoea kwanza walisema baada ya world cup mziki utaanza wapo wapi kama ndugu yangu umeishi miaka 5 hapa kweli ulikaa Sandton. hujatembea hata Brixton sisemi khu soweto nipo hapa SA since 1994 na vitisho kama hivi nisawa na kumpigi kuku gita hakuna mchawi anakuambia kesho nakuja kukuroga .kama kaamua anafanya tu hawa jamaa Shemeji zangu nimeishi nao Location na ktk suburn moja wanapenda kuongea sana hasa ukujua lugha yao ndo utawaelewa wageni wanao chukiwa sana hapa hawapo ktk hio list.kwa uzoefu wangu Wazimbabwe namba moja Wapopo na mbili Mozambique 3 wasomali 4 wake na wabongo wapo mbali ktk list wa Bngladesh na wachina wapo juu zaidi ya wabongo wageni wesha zaa sana na dada zao kwahio itafikia kila family ya sauz ina mtoto mgeni atamfukuza mtoto wa dadake pia wacha jamaa pia walalame tupo wengi sana hapa kupita kiasi.Mr Gugs

    ReplyDelete
  27. sidhani kama ni mtu mweusi ameandika hii,wazungu wanataka kutuchonganisha sisi kwa sisi tuuane,tuchukiane...huko kwao choka mbaya sasa hivi hawaelewani wenyewe kwa wenyewe na wameshaona kwetu tuna amani waanze chokochoko...mtaona hakuna lolote litakalotokea,hapa muafrika anatiwa moto a wazungu akianza mmoja ndio inaendelea lakini sidhani kama hii ni mwafrika.

    ReplyDelete
  28. Bora umeiweka hiyo barua watu wapate taarifa na wawe makini.

    ReplyDelete
  29. kaka nadhani si vizuri kupost kitu cha namna hii...lugha iliyo tumika ni mbaya sana ukizingatia kuwa hii ni blog ya jamii...next time recosider

    ReplyDelete
  30. Hili si la kupuuza,ukipewa taarifa unaifanyia kazi jamani...sisi wa-tz hatukuzoea vurugu ndio maana wakati mwingine hata ukitishwa ukiwa kwenu huogopi...lakini hili ni tishio la nje kwa wa-tz waliomo ndani,ni budi kulifanyia kazi kuanzia balozi zetu na kadhalika.Watu na tabia hutofautiana nchi na nchi,kwa hiyo ni bora kulifanyia kazi.

    ReplyDelete
  31. Hawa jamaa ni wavivu sana wanawaza tu kuendesha BMW na kunywa pombe hakuna kutafuta maendeleo. Wakifika watanzania au wakenya katika sehemu kama hii yenye opportunities nyingi wanagfanya kweli hawafanyi makosa ni kutengeneza tu pesaa sasa wao wivu sijui unatoka wapi.KWani kuna mtu anawazuia kutengeneza pesa? Adui yenu ni kaburu na wala sio mtu mweusi aliyekuja kutafuta maisha

    ReplyDelete
  32. Kaka Michuzi, Mimi sioni ubaya wa hili Tangazo kuwekwa hapa. Ndiyo taarifa rasmi. Na ni vema ikatoka kama ilivyotoka. kuna huyo anony anayeuliza ushaidi anataka ushahidi gani? yaani uweke picha ya maiti au? Nafikiri jamaa wameshajisahau; walipokuwa wanaonewa sisi tuliwakingia kifua leo wao wanatuona sisi magonjwa. Wao wanaweza kuwa tatizo kubwa kuliko wale weupe! Kwa lugha aliyoitumia anaoneka si Mtanzania, maana kiswahili chake kimepinda pinda sana. Anaweza kuwa ndiye yule wa mwanzo aliyeandika kwa kiingereza.

    Mdau HK

    ReplyDelete
  33. I am against the first comment, this is a very nice post, because this isa menase(threat) we need to know what they are thinking about us, for me it is very nice, keep it up, I wanted to go to south Africain recent days, now I cancel my travel to that crazy country for good.Is good to know who is the enermy and who is the friend don't hide things like these, Ok Michuzi.If you think law of countries enjoy killing, have your law and let's save our souls.

    ReplyDelete
  34. at the end of the day home is best ona sasa mambo gani haya ya kuabishana still dozens of somalians,ethiopians and elitrians are on the roads heading RSA Mh!

    ReplyDelete
  35. Jamani huwezi kupost maneno ya aina hii kwenye blog kama hii ya kijamii,kwa sababu unawafundisha nini watanzania sasa?kwani sheria si zipo?mi naona hapa tunafundishana kutukana kwenye blog.

    Naomba maadili ya wasomaji hasa ya kitanzania yazingatiwe wakati wa kupost issue zingine.

    ReplyDelete
  36. Nipo Johannesburg city center, haya mambo sisi hata siku moja hapa ndani ya jiji hayatupati. Sanasana sisi ni kuwasaidia tukipenda kwa kuwatoa hela kidogo2, maana wengi wanakula bangi na madawa mengine hawawezi hata kujimudu. Yaani hapa jijini hawafanyi lolote, ila wale manaokaa mbali na jiji msipokuwa makini wanaweza kuwaanzishia.

    Nijuavyo mimi wanaoharibu SA ni wanigeria kwa biashara zao haramu na sio wengine waliotajwa. Wametutaja sisi kwa sababu wanajua hawawawezi wanigeria ni watata watawakimbiza. Kwa hiyo unapoongelea xenophobia mie sijui hata harufu yake, ni sawa na watu wanachinjana Tarime halafu unanitahadharisha mie niko Dar, Masaki. Watawavamia huko mashambani sio hapa mjini, hata hivyo huo ni mkwara tu. Mikwara kama hiyo ndiyo inatuchangamsha vichwa tunachacharika zaidi.

    ReplyDelete
  37. we annos wa kwanza Tue Dec 13, 12:10:00 AM 2011,kama hauna cha kuchangia ni bora huwe unasoma maoni ya watu si lazima uchangie.pili icho kiinereza chako mbona ni cha kubabaisha umeandika kwamba(you need not to post something like this.
    nakutakia raheri.

    mdau,cologne.

    ReplyDelete
  38. Brother michuzi ...mimi kimtazamo natofautiana na mchangiaji wa kwanza anaesema umefanya makosa kuipost hii taarifa. eti kwamba sheria zipo zitachukua mkondo wake incase anything happen . mi nasema LA!! Haiwezekani kusubiri mtu adhurike / afe eti kwasababu unaamini akifanya hivyo sheria itachukua mkondo wake ...ni vyema kujihadhari kabla ya hatari. Kwa kuiona hii taarifa wahusika watachukua tahadhari au hata watu wenye ndugu RSA Pia watawataarifu ndugu zao wakae makini kuliko michuzi angekaa kimya ni hatari zaidi.
    na lingine tujifunze sasa watanzania tumezidi ukarimu unaotutokea puani ...wenzetu kwenye nchi zao wanatunyanyasa wakati sisi kwenye nchi yetu tunawaona babkubwa!!!! inatia hasira sometimes!!!

    ReplyDelete
  39. America magaidi wa kibaguzi zaidi ya Black Panthers na Black Liberation Army (BLA) walikuwepo ma racist kama KU KLUX KLAN walikuwa ni whites au Wazungu wakiwa na chuki dhidi ya blacks lakini watu waliishi hivyo hivyo tu!

    ReplyDelete
  40. Mdau wa kwanza kabisa Anonymous..Brothe Mihcuzi you need do not post this!.

    Mficha maradhi kilio humuumbua!
    Mwanaume ni muhimu kujua nini tatizo ili kutafuta na kupata ufumbuzi wake!

    Michuzi amefanya vizuri ku pos,,,sasa asipo post tungejuaje?

    Suluhisho la matatizo linakuja kwa kuyatambua na kuyashughulikia sio kwa kunywa pombe ili kupoteza mawazo!

    ReplyDelete
  41. SAWA SAWA SASA WABONGO TUJIFUNZE, HILO NI SOMO. KWANI KILA MTU ANAKIMBIA NCHI, OOOH SIJUI MAREKANI SIJUI DENMARK, UK JAPAN
    HAKUNA ANAEWAPENDA WAGENI HASA INAPOFIKIA WAKATI WA MASLAHI. NI SISI TU NDIO TUMEBAKI MDEBWEDO, MATAIFA YOTE NI WAKALI KWA WAGENI.LAZIMA TUJUE UCHUMI WA DUNIA NI CHINI HIVI SASA ,BADALA YA WAO KUPATA KAZI ZINACHUKULIWA NA WAGENI TENA, CHEAP LABOUR.(TUNAPOZIDI KUWAUDHI HAPO).NA SIS TUIGE MFANO HUO,MIMI NAWA SUPPORT KWA ASILIMIA KWA MIA.HAPA KWETU BONGO MIJITU IMEJAZANA HATA HATUJUI IMETOKA WAPI WALA MAKARATASI MUHIMU YA KUISHI TANZANIA HAWANA. NA SISI TUANZE KUPIGA WACHINA, WARUNDI, WAKONGO, MANIGERIA,MA CAMERRON, WAKENYA , WAGANDA WAZAMBIA WADOSI MAPAKISTAN, NA WAHINDI WASOMALI, WAENDE KWAO HAWA NDIO WANATULETEA MATATIZO KWETU HAPA BONGO. WIZI,UTAPELI,KUGHUSHI,NA DADA ZENU WANATOA NYETI BURE ETI KAMPATA MZAIRE AU MNIGERIA,YOTE HAYO NI MATATIZO .KARIAKOO SOKONI HIVI SASA KAZI ZA WALALA HOI,KUVUTA MIKOKOTENI, TAYARI MCHINA KISHA VAMIA NA SISI KULE KWAO HUTOSUBUTU KUCHUKUA KAZI YAO LA SIVYO NI KIFO UNAKITAFUTA. LAZIMA SASA TUAMKE . TUWEKEZE BONGO HUKO SOUTH ,USA.UK.CANADA,SIJUI UPUUZI WA SCANDINAVIA HAKUNA TENA! WAZUNGU WA SCANDINAVIA WANABAGUA MPAKA KICHEFUCHEFU., LAKINI UTAMKUTA MTZ BADO KAMA HAELEWI KITU VILE, SASA KAMA HUELEWI NDIO KICHAPO KINAANZA NA SEREKALI ZAO ZINA WASUPPORT HAO WABAGUZI.

    NA SISI BONGO TUANZE VITA ZAIDI YA WAGENI HASA HAWA MUSICIAN TOKA ZAIRE KINA NGWASUMA WANACHUKUA KIPATO CHA WANAMUZIKI WETU HAPA WAO WANALIPIWA MPAKA NYUMBA NA DADA ZETU KIASI AMBACHO KINAUMIZA SANA ROHO UKIANGALIA KASI YA MAISHA YA HIVI SASA. NI WAKATI VIJANA WETU WA BONGO FLAVA KUTENGENEZA LAKINI WANAKUWA WANAGAWANA NA HAO WAGENI WAKONGO WANAOISHI HAPA BILA KULIPA KODI YOYOTE, NA BONUS YA WANAWAKE WANAPATA. KWELI? MIMI MTANZANIA NINA UCHUNGU KAMA HAO JAMAA WA SOUTH AFRIKA, NA HAPA BONGO TUTANGAZE VITA VILEVILE.

    MDAU KINONDONI_DAR
    ,

    ReplyDelete
  42. Hawa na Mozambique ni watu wa aajabu sana. Afrika kusini hii haitokuwa mara ya mwanzo, kwa hiyo watafanya tu. Kwasababu vijana wa Tanzania si watu wa fujo, wao ndio watakao athirika, ni vyema wakatafuta sehemu nyengine za kuishi lakini si Afrika kusini. Lazima watambuwe, kama kuna nchi ilitumia pesa zake nyingi kwa ajili ya ukombozi wa nchi nyengine ikiwemo Afrika kusini, basi ni Tanzania.

    ReplyDelete
  43. Haturudi bongo ng'oo!!

    ReplyDelete
  44. Kifupi nasema chukua tahathari mapema. Big up mtoa habari

    ReplyDelete
  45. Watu wanaandika pumba hadi aibu,mnaoweka maoni yenu, basi kabla ya kupost soma tena kwa makini kama inafaa yasomwe na wengine.

    ReplyDelete
  46. Manyanyaso yapo hata huku India,tatizo wanashidwa kututofautisha wabongo na wanaijeria michuzi.kuna mbongo bangalore,India alikufa kwa utata sana na inasemekana waindi walimkata kichwa.je ni waindi wangapi wako hapo tanzania na hatuwafanyii huo unyama.Serikali Amkeni na sisi kama ni umaskini basi kila mtu haishi kwake.Wabongo mlioko South ondokeni haraka na wasauth walioko bongo nao waondoke.

    ReplyDelete
  47. Manyanyaso yapo hata huku India,tatizo wanashidwa kututofautisha wabongo na wanaijeria michuzi.kuna mbongo bangalore,India alikufa kwa utata sana na inasemekana waindi walimkata kichwa.je ni waindi wangapi wako hapo tanzania na hatuwafanyii huo unyama.Serikali Amkeni na sisi kama ni umaskini basi kila mtu haishi kwake.Wabongo mlioko South ondokeni haraka na wasauth walioko bongo nao waondoke.

    ReplyDelete
  48. Simplicity said...
    Nipo Johannesburg city center, haya mambo sisi hata siku moja hapa ndani ya jiji hayatupati. Sanasana sisi ni kuwasaidia tukipenda kwa kuwatoa hela kidogo2, maana wengi wanakula bangi na madawa mengine hawawezi hata kujimudu. Yaani hapa jijini hawafanyi lolote, ila wale manaokaa mbali na jiji msipokuwa makini wanaweza kuwaanzishia.

    Nijuavyo mimi wanaoharibu SA ni wanigeria kwa biashara zao haramu na sio wengine waliotajwa. Wametutaja sisi kwa sababu wanajua hawawawezi wanigeria ni watata watawakimbiza. Kwa hiyo unapoongelea xenophobia mie sijui hata harufu yake, ni sawa na watu wanachinjana Tarime halafu unanitahadharisha mie niko Dar, Masaki. Watawavamia huko mashambani sio hapa mjini, hata hivyo huo ni mkwara tu. Mikwara kama hiyo ndiyo inatuchangamsha vichwa tunachacharika zaidi.

    Tue Dec 13, 03:28:00 PM 2011

    Na huyu nae hamnazo!

    ReplyDelete
  49. WABONGO TULIOKO SOUTH HATUONDOKI NA HAKUNA CHOCHOTE KITAKACHOTOKEA

    ReplyDelete
  50. Mi naona ni vitisho vya wanadamu tu, Globalzation ni pamoja na watu wa nchi mbalimbali kuishi nchi zingine kwa sabubu za kielimu au kufanya kazi as long as umepatiwa kibali cha kukaa na hiyo serikali. Swala la kusema hao wabongo wa SA waondoke huo ni woga. Chuki kama hizo ziko kila mahali hata hapo nyumbani, cha muhimu ni kuwa imara katika kila unachikifanya ila zaidi ya yote mtangulize Mungu maana duniani hakuna mahali kwema kwa kuishi. Ila kwa ulizi wa Mungu utaishi hata IraQ na mtu hakugusi. Sie wanadamu hatupendani hata kidogo kwa ajili ya ubinafsi wa maslahi ndio mana nchi yetu iko masikini mpaka leo na vijana hawana ajira kwakua viongozi wetu wenyewe ni wabinafsi wanaangalia maslahi ya familia zao na si wananchi. So stand where you are keep your head up and pray hard, yoo will not find a safe place to live as long as you live in this crazy world. Hapo nyumbani watu wangapi wanauawa???....kibao..so?

    ReplyDelete
  51. Wasauzi tutakula nao sahani moja...wao husema UMKHONTO WE SIZWE...na sisi tutasema MKUKI WA UKOMBOZI!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...