Kwa masikitiko makubwa tunawatangazia kifo cha Mzee wetu Robert Jaka wa Forest Hill- Morogoro (pichani), kilichotokea katika hospitali ya Regency mchana huu wa Jumapili ya tarehe 22/01/2012 Dar-es-salaam-Tanzania.

Marehemu katika uhai wake alifanya kazi katika vyuo vikuu vya Sokoine na baadae chuo kikuu cha Dar-es-salaam kabla ya kustaafu na kurejea Morogoro. Msiba upo Dar-es-salaam Mtoni-Kijichi (nyumba za maafisa wa Magereza)

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Morogoro siku ya Jumanne na Mazishi yanatarajiwa kufanyika Morogoro siku ya Jumatano tarehe 25.01.2012.

Kwa taarifa zaidi za msiba unaweza kuwasiliana na Kizito Jaka (+255 762 583740 begin_of_the_skype_highlighting            +255 762 583740      end_of_the_skype_highlighting) Paschal Kunambi (            +255 713 233843      ) au Exupelius Kunambi (+255 767 201098 begin_of_the_skype_highlighting            +255 767 201098      end_of_the_skype_highlighting)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. R.I.P mzee Jaka ulikuwa mtu wa aina yake ulipokuwa unafanya kazi UDSM mwenyezi mungu akurehemu .amen

    ReplyDelete
  2. Poleni sana akina Kizito. Mzee Jaka ni jirani yangu pale Forest Hill Morogoro. Ukapumzike kwa amani.

    ReplyDelete
  3. poleni sana wana familia,poleni sana wanamji kasoro bahari,mungu ailaze mahala pema peponi roho ya mzee jaka.

    ReplyDelete
  4. Mzee Jaka nimefanya kazi nae pale UDSM ni mtu mwema sana. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, amin.

    ReplyDelete
  5. expelius kunambiJanuary 23, 2012

    R.I.P my dear father.

    ReplyDelete
  6. Natoa pole sana kwa Familia ya Mzee Jaka. Nawaombea familia yake ipate faraja katika kipindi hiki kigumu.

    RIP Mzee Jaka

    ReplyDelete
  7. Mzee Jaka alikuwa jirani yetu pale Simba Road karibu kabisa na UDASA. Taifa limepoteza mmoja wa wazee ambao walikuwa mfano mkubwa kwa wasomi wa kizazi chetu.

    ReplyDelete
  8. Pole sana wapendwa wetu Jaka and Kunambi's family Mwenyezi Mungu awatie nguvu. RIP baba mpendwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...