Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla, akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kidudwe, Kata ya Mtibwa , Wilayani Mvomero kwenye Mkutano wa hadhara alioufanya kijijini hapo jana.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero,Mh. Amos Makalla ( kushoto) akimkabidhi Mpira kwa mmoja wa watoto wa Kijiji cha Kugenge, Kata ya Mtibwa aliyoinunua Mbunge huyo kwa ajili ya kuendeleza michezo kwenye timu ya watoto wa kijiji hicho.
Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( kulia) akimkabidhi Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kugenge, Kata ya Mtibwa ,Romanus Daniel ( kushoto), Jenereta moja kubwa aliyoinunua Mbunge huyo kwa ajili ya kusukuma maji safi na salama ili kuwaondolea kero wananchi wa Kijiji hicho.
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro , Yusuph Kingu ‘ Lule’ ( kulia mwenye shati la kijani) akiwatambulisha baadhi ya waliokuwa wanachama wa Chadema Kata ya Mtibwa ,ambao waliamua kurudisha kadi zao na kujiunga na CCM kwenye Kijiji cha Kidudwe wakati wa mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mbunge wa Jimbo la Mvomero ( CCM) Amos Makalla (hayupo pichani) .
Mmoja wa aliyekuwa mwanachama wa Chadema , Kata ya Mtibwa, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, akitoa ushuhuda wake kwa niaba ya wenzake waliokihama chama chao na kujiunga na CCM wakati wa mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla ( hayupo pichani) kwenye mkutano uliofanyika Kijiji cha Kidudwe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. sorry picha zote, zinaonekana. nilifunga na kufungua tena.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...