Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amefanya uteuzi wa viongozi katika Taasisi mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kama ifuatavyo:-

MKUU WA KIKOSI CHA VALANTIA

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 9(1) cha sheria ya Kikosi cha Valentia,Zanzibar No.5 ya mwaka 2004,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amemteua LT. COL. Mohammed Mwinjuma Kombo kuwa Mkuu wa Kikosi cha Valentia,Zanzibar.

KATIBU WA BARAZA LA WAWAKILISHI

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 76(1) cha Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984, Rais wa Zanziabar na Mwenyekiti wa Barza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amemteua Yahya Khamis Hamad kuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi,Zanzibar

MWENYEKITI WA BODI YA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 6(1) (a) cha Sheria ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege vya Zanzibar No.8 ya mwaka 2011, Rais wa Zanziabar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amemteua Abdulghan Himid Msoma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamalaka ya Viwanja vya Ndege, Zanzibar.

MWENYEKITI WA BARAZA LA ELIMU, ZANZIBAR.

Kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 5(1) cha Sheria ya elimu No.6 ya mwaka 1982 kama kilivyorekebishwa na kifungu cha 6 cha sheria No. 4 ya Mwaka 1993 Rais wa Zanziabar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein amemteua Saada Thani Fakih kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Elimu,Zanzibar.

Uteuzi huo umeanza 25 Machi 2012

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...