TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

       Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Ignus Paul Kitusi kuwa Msajili Mkuu wa Mahakama (Chief Registrar) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.  Kabla ya kuteuliwa kushika wadhfa huo mpya, Bwana Kitusi alikuwa Msajili wa Mahakama Kuu.

       Katika uteuzi huo, vilevile Rais Kikwete amemteua aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Rufani la Kodi, Bwana Panterine Muliisa Kente kuwa Msajili wa Mahakama ya Rufani (Registrar of the Court of Appeal) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012. 

       Aidha, Mhe. Rais amemteua Bwana Benedict Bartholomew Mwingwa kuwa Msajili wa Mahakama Kuu (Registrar of the High Court) kuanzia tarehe 1 Julai, 2012.  Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mwingwa alikuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
6 Julai, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2012

    MBONA SIKU ZA KARIBUNI DR KIKWETE APPOINTMENT ZAKE NI WAKRISTU TU HIVI WAISLAMU HATUONI?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 09, 2012

    Heee!!makubwa,we mwananchi,tulia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...