Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mwantumu Mahiza akikata utepe wakati wa kuzindua magari mawili ya kubebea wagonjwa katika hospitali ya Tumbi mkoani pwani,magari hayo yametolewa na serekali ya Korea kupitia kwa Rotary Intenational club ya tanzania.Magari hayo yana thamani ya shilngi milioni miambili thelathini za kitanzania.kushoto ni mwakilishi kutoka Shirika la Kimaendeleo la Korea (KOICA),Jinyong Kim na kulia ni mwakilshi wa Rotary Club Tanzania,Bill Bali na nyuma yao ni Mganga Mkuu wa hosipitali ya tumbi,Dr Petar Datani na aliye nyosha mkono ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu Kibaha,Dr Cyprian Mpemba hafla hiyo ya makabidhiano imefanyikia leo katika hospitali ya Tumbi Mibaha.Picha na Chris Mfinanga
 
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mwantumu Mahiza akiwa ndani ya Gari hilo huku akipatiwa maelezo yahusuyo gari hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mwantumu Mahiza akiteremka kwenye gari hilo baada ya kulikagua.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Nalile gari(ambulance) lililo paki pale ofisini kwako RC-PWANI litoe likabebe Wagonjwa, Hospitali za wilaya, maana limekaa tu.

    ReplyDelete
  2. Msiishie kulala tu humo nyie madereva hamchelewi

    ReplyDelete
  3. tunaomba mara zinapo kuwa na mahitaji ziende mara moja sio uambiwa haina mafuta au ufunguo haonekani tunashukuru kwa msaada na mungu atawazidishia wawe na moyo huo huo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...