Meneja Huduma wa Airtel Tanzania, Hilda Nakajumo (kulia), pamoja na baadhi ya wateja wao wa makampuni, wakipakua chakula katika hafla ya futari waliyoiandaa kwa wateja wao, katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha jana. Kushoto ni Anne Gitarda na Evelyn James, wote kutoka katika ofisi za UN-ICTR jijini humo.
Meneja Huduma wa Airtel Tanzania, Hilda Nakajumo (wa tatu kushoto), akizungumza na baadhi ya wateja wao wa makampuni, katika hafla ya futari waliyoiandaa kwa wateja hao, katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.
Baadhi ya wateja wa makampuni wa Airtel Tanzania wa Mkoani Arusha wakichota uji katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Airtel Tanzania,katika Hoteli ya Naura Springs jijini Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. kwani wamefunga?

    ReplyDelete
  2. Wadau hiyo futari mbona haifuati utaratibu wa futari? Au fuutari fashion? Maana hao kina mama hawana shungi na sioni kama kuna dalili zozote kama kuna maadili yoyote ya ibada ya Swaumu hapo.
    samahani sana kwa kusema hivyo lakini imebidi niseme.

    ReplyDelete
  3. futari gani watu hawajajisitiri. hii inaharibu maana ama tuite dinner party.

    ReplyDelete
  4. Waseme airtel wamefanya chakula cha jioni, hapo hakuna mfungaji hapo.

    ReplyDelete
  5. Duh! kaazi kweli kweli, mbona hawajakaa kama wa kufuturu acheni kutuzuga nyie aairtel, kuna mfungaji kweli hapo , hata ushungi lol?!!1 semehi chakula cha usiku!

    ReplyDelete
  6. Hata mimi naona ni chakula cha usiku, maana swaumu au ftari ina staha zake, kujihifadhi ni vyema.
    Lakini waandaaji - airtel wameona wafanye dinner kwa kupakazia ftari.
    Kuna methali inasema ukikuta wamekunja miguu na wewe kunja... So mnakuwa sawa.
    Mdau wa Airtel

    ReplyDelete
  7. Hii ndiyo Arusha...International city ya Bongo....shungi wapi na wapi...nyie vipi!...shungi kwani ndio inakula? aah?...Angalie wenzenu wa Jordan..hi mambo yenu ya shungi hakuna kabisa....kwani Arsuah ni Jangwani?...kuna upepeo wenye mchanga?...Acheni ushamba huo!

    ReplyDelete
  8. Mm nasema Airtel Arusha ni wanafiki kwa sababu hawakufuturisha ila waliwapa dinner watu amanao hata hawahusiki na futar,kualika wti amabao wameshindwa hata kujistir na kuacha kuonesha picha za wahusika wa tukio,nasema huo ni unafki kwa Airtel Arusha hii waliamua kualika marafiki zao na kuwapa dinner,so discusting kwa kweli,na ni tabia mbaya kwawaandishi habari waliochukua tukio lote pamoja na waandaaji wa shughuli,so badilisha hilo jina lafutar na uandike Aitel Arusha waandaa dinner kwa marafiki zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...