Mzee wa Libeneke - Naomba uipost hii thread, wadau waipitie please,

Nimetoka zangu ofisini, naingia kwenye daladala natafuta mahali pa kukaa, kwa bahati nakaa jirani kabisa na dereva. 

Daladala hili linafanya safari zake Masaki – Gongo la Mboto. Baada ya muda kidogo mjadala wa vurugu zilizotokea eneo la Kariakoo tar 19.10.2012 unachanganyia sana, hapo ni baada ya kutoka kituo cha Morocco, dereva wa daladala anasema “vita vya dini ni ujinga kwani mtu huwezi kupigania dini yako” anajenga hoja yake kwamba suala la imani ni gumu kiasi kwamba halina mashiko kuwagawa watu ambao wameishi kwa kuheshimiana na kuvumiliana kwa kipindi kirefu huku kila mmoja akiwa na uhuru wa kuabudu atakacho. 

Nateremka kituo cha Banana na hapo ninaanza safari yangu nyingine kuelekea Machimbo, napita eneo moja nasikia mjadala huo huo, wachangiaji wamehamasika sana. Mmoja anasema “wanaopigana kwa ajili ya dini ni wapumbavu kwani hakuna mtu ambae amewahi kuwa mshindi hata katika mijadala ya dini achilia mbali kupigana ~ mijadala tu haijawahi kutoa mshindi” anaenda mbali zaidi anasema “Mimi nitapigania Utaifa na si Dini”. 

Nashindwa kujizuia nageuka kumwangalia, kumbe ni fundi seremala kwani ameshika ubao wake na randa na pembeni yake kuna kitanda kilichotengenezwa tayari. Naanza kufikiri ~ huyu ni seremala amekuwa na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo, wako wapi hao wanaojiita wanazuoni wa dini na watu wengine ambao tungedhani kwa elimu zao wanaweza kuwapa elimu waumini wao ili kuepuka machafuko yasiyo ya lazima. Nimemheshimu yule kijana hasa ukizingatia kwamba elimu yake ni ya wastani,

“Kupigania Dini ni Ujinga - Nitapigania Utaifa”

EKN - DSM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. wewe na yeye bado mko nyuma pia.

    unatakiwa upiganie haki bila kujali dini wala taifa.

    ndo maana tanzania ilipigania kupinga ukaburu hali si raia wetu.

    ndo maana USA ilipigania uhuru wa bosnia na hali marekani ni 99% wakristo.

    unakiwa uhakikishe wantu wanapata haki hata kama wanaisema dini yako vibaya. hapo wataona dini yako nzuri. lakini kama wewe unaongoza kuminya haki, wanaweza kupigania haki katika kivuli cha dini.

    ReplyDelete
  2. swala zaidi ni kupigania haki.

    dini inaingia tuu kwani ni rahisi kukusanya raia kiimaini kuliko kikabila au kimkoa. halafu waambie unapigania haki, hakuna dini haitopigania haki isipokuwa iliyo feki.

    na dini itayorudi nyuma na kuacha kudai upatikanaji wa haki basi dini hiyo si ya kweli. haijali anayepata haki ni nani.

    ReplyDelete

  3. kila raia ana haki ya kulinda maisha yake kwa gharama zoote bila kujali imani yake.

    ReplyDelete
  4. Mtazamo wako na wa seremala uliendana, na wote mnaona watu wanapigania dini. Ukweli (au mawazo yangu) ni kwamba watu wanapigania haki dhidi ya dhuluma. Ni katika vyama vya siasa pia, unadahani watu wanapigania vyama?

    ReplyDelete
  5. Mdau EKN,

    Makala yako ni nzuri, la muhimu ni kuwa Hakuna Dini inayoelekeza kuwatendea Ubaya watu wa Imani zingine, pamoja na viumbe wote pia.

    Kuwa Muumini mzuri kigezo kimojawapo ni kuwa Mstaarabu, kutokuwa na pupa wala Jazba ktk kuyafikia mambo.

    Sasa unapomkuta Mtu akiwa na Dini inayosisitiza Ubaya dhidi ya watu wengine inawezekana hajaelewa vizuri Masomo ya Dini aliyopewa na Wanazuoni.

    ReplyDelete
  6. Kupigania kitu unachokiamini si Ujinga. Ujinga ni kupigania kitu usichokiamini na kisichokuwa na tija kwako!

    ReplyDelete
  7. MDau wacha unafiki.Hujamsikia yeyote kusema maneno hayo,haya ni maoni yako tu yakipuuzi.Hapaumewalenga waislam bcoz ndio waliopigwa K.Koo.Ila wale wanaotumia nyadhifa zao ktk maofisi,mashule na mahospitali kuwabagua wenzao wao sio wadini si ndio?
    Tatizo lenu nyie mnajifanya mna akili nyingi na wengine wote ni wapumbavu.Lkn huko ni kujidanganya wenyewe na kelele za mpita njia hazimshughulishi mkazi wa nyumba.

    ReplyDelete
  8. Anonymous nina kubali mpita njia hazimshugulishi makazi wa nyumba.Wengeno tuna piga kelelele hata kama hakuna mabadiliko tuna taka kuhakikisha kelelele zetu ziwe ushahidi mambo yana tokea nchi ni. Hasa kwa wale tulio tumiwa na kuendelea kudangaya tusio na uhuru, au haki ya kurundi nyumbani.

    ReplyDelete
  9. Tatizo la hapa ni kwamba hii nchi ina makundi mawili ya wananchi wake,
    kundi moja ni lile ambalo halina haja ya kufanya kitu wao wakisema tu serikali inatekeleza na kundi la pili ni lile ambalo limekuwa likisema serikali inapinga au haifanyi kitu.
    Sasa kama kawaida ya mnyonge hufika wakati hata yeye huchoka na akichoka matokeo yake ndio hizi challenges tunazoziona.
    Hakuna seremala wala dereva wa daladala ukifika wakati wa basi huwa basi unafiki wa kusema nitagombania utaifa kuliko dini ni unafiki wa kuridhisha wachache.
    Hakuna atakaekubali kutukaniwa dini yake lililopo hapa ni kundi moja lina sikio la serikali na jingine serikali imezoe kuliburuza na sasa limechoka
    na kwa mtindo huu wa serikali kujifanya viziwi na vipofu haya hayatakwisha, na yule aliyesema USA in 99% wakristo hizo data umezitoa wapi mpaka 2010 walikuwa 72% usilolijua uliza....

    ReplyDelete
  10. Kwa mungu hakuna dini, ndio maana jua na mwezi havijagawanywa kidini, usiku na mchana haukugawanywa kidini. Mengine mtamalizia wadau

    ReplyDelete
  11. Mimi mtanzania nipo america, haki gani hiyo ambayo ilikuwa inapiganiwa kwenye machafuko kariakoo, acheni ujinga kila mtu alikuwa mtoto ama anawatoto, au mtoto, ukifanya mambo yote ambayo watoto wanafanya utakuwa mjinga, ni mtoto, kama kweli unataka haki yako atuna maji ya uhakika, umeme na watu wanalipwa milioni of dollars kisa viongozi na unasema haki haki gani?kima cha chini tanzania ni shillingi ngapi? acheni ujinga wa watoto kwa watoto, kama haki msiweke udini.

    ReplyDelete
  12. Naomba ninukuu maoni ya mdau Anonymous:
    MDau wacha unafiki.Hujamsikia yeyote kusema maneno hayo,haya ni maoni yako tu yakipuuzi.Hapaumewalenga waislam bcoz ndio waliopigwa K.Koo.Ila wale wanaotumia nyadhifa zao ktk maofisi,mashule na mahospitali kuwabagua wenzao wao sio wadini si ndio?
    Tatizo lenu nyie mnajifanya mna akili nyingi na wengine wote ni wapumbavu.Lkn huko ni kujidanganya wenyewe na kelele za mpita njia hazimshughulishi mkazi wa nyumba.

    Mon Oct 22, 01:24:00 PM 2012

    Halafu naomba nimkumbushe kwamba Mwajiri Mkuu wa Serikali ni Jakaya Mrisho Kikwete. Makamu wake ni Dk Gharib Bilal. Rais wa Zanzibar ni Dk Mohamed Shein. Anonymous anataka kusema kwamba watu hao wanabagua wenzao katika nyadhifa zao?????

    Niwakumbushe pia wadau kwamba hii nchi haina Wakristo na Waislamu tu. Kuna watu wana imani nyingine wapo nchini na wana imani nzuri tu. Kuna Wabuda, watu wenye imani za jadi nk kati yetu. Wote wanahubiri upendo.

    Hao walioleta vurugu kwa muda mrefu nilikuwa naamini ni kikundi kidogo cha wahuni. Nashangaa kuna watu wanataka kuwahusisha na imani ya dini. Kuna dini inahubiri kuvunja sheria halali kama vile kutoharibu mali ya mwenzio, kutovamia ardhi ya mwenzio nk???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...