Meneja Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Karim Mattaka (katikati) akionyesha sehemu ya ujenzi wa Daraja hilo unaoendelea hivi sasa katika eneo la Kurasini mpaka Kigamboni wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia Maendeleo ya Jamii ilipofanya ziara ya kuona ujenzi wa Daraja hilo leo.Watano Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mh. Jenista Mhagama na Kulia ni Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudencia Kabaka. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau (kulia) akiuongoza ujumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia mambo ya Maendeleo ya Jamii,iliyofanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa Daraja la Kigamboni mapema leo.Wengine pichani toka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mh. Jenista Mhagama,Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka na Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtera,Mh. Livingston Lusinde.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia mambo ya Maendeleo ya Jamii wakiwa katika ziara ya kutembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigambini unaosimamiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),uliopo eneo la Kurasini Jijini Dar es Salaam leo.
Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia mambo ya Maendeleo ya Jamii ikipatiwa maelezo mbali mbali juu ya ujenzi wa Daraja hilo ambalo ujenzi wake utachukua takribani miezi 36 mpaka kukamilika kabisa.Daraja hilo lina urefu wa mita 680 na litakuwa na jumla ya barabara sita ambazo tatu zitakuwa zinakuja mjini na zingine za kuelekea Kigamboni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Tungepata watu kama watano tu kama Dr Dau basi Tungezungumza maneno mengine. Inakuaje kijinchi kama Rwanda kitushinde wakati imetoka ktk vita. Ktk vitu tunavyojisifu navyo ni pamoja na amani lakin tunashindwa kuelewa amani imetusaidia nini ktk kuutengeza maisha bora kwa kila mTanzania. Haya gas hiyo imegundulika basi pia kutakua na longo longo jingine. Tuweni serious

    ReplyDelete
  2. Mdau wa Kwanza hapo Anony wa Thu Oct 18, 11:08:00 PM 2012

    Nakuunga Mkono kabisa!

    Mfano wa Jamhuri ya Rwanda nchi ndogo ambayo Uchumi wake unategema Kilimo cha Chai, Kilimo cha Maua, na Utalii wa Manyani Mlima Ruhengeri wameweza kununua ndega Mpya 'brand new' Boeing 737 nne (4) na wanataka kutimiza ziwe 10 hapo 2014 huku sisi tukiwa na mali kuluki kama Gas,Almasi,Mafuta,Chuma,Dhahabu,Misiti,Madini mengine,Maliasili na mali zingine kibao tukiwa tumekodi ndege 2 tu tena mbovu!

    Hii yote inatoikana na kuwa na Wanasiasa wa aina ya Karata tatu kama akina ZK wanaouma huku na huku wakiuma na kupuliza,

    Ni Uamuzi wa busara Mhe. Prof. Mhongo Waziri wa Nishati na Madini kuipitia Mikataba yote 27 upya ili nchi iweze kuwa na maslahi na kupiga hatua kimaendeleo ikitumia nafasi ya Rasilimali zake kama tunayoyasema na kuyatarajia hapa.

    Haiwezekani ujenzi wa nchi na Mustakabali wake akaachiwa Raisi Jakaya Kikwete peke yake anahitaji awe na watu wenye nia njema na nchi yetu na wenye kuaminika kama akina Dr. Dau, Prof.Muhungo na wengineo!

    ReplyDelete
  3. Ili Tanzania yetu kupiga hatua na Raisi wetu Mpendwa Jakaya Mrisho Kikwete kupewa mazingira ili aweze kutimiza alichotuahiadi na sisi tusimwone muongo yanahitajika mambo haya:

    1.Tunatakiwa tujitoe muhanga kuhakikisha ya kuwa Maadui wapinga maendeleo ya nchi wasiozidi 45 ktk nchi ya watu Mil 45 tuwatoe kafara ili tuweze kusonga mbele!

    2.Tujenge mwenendo wa kuwajibishana na kuulizana hatua kwa hatua ktk mchakato wa kuendesha mambo yetu.

    3.Tuhakikishe Rasilimali zetu zote nchini sio kinadharia bali kivitendo zinashikiliwa na Wananchi walio wengi na sio maslahi yake yana hodhiwa na kundi dogo la watu hao hao wasiozidi 45 wa No. 1 hapo juu!

    Mara nyingi vitu kama Mikataba mibovu na maslahi ya rasilimali ni saccos au njia ya ulaji ya watu hao hao wasio zidi 45 nchini.

    Kama tutazingatia hayo matatu (3) hapo juu ni wazi Tanzania itapiga hatua kwa namna nyingi zaidi za maendeleo kama ya Ujenzi wa Daraja la Kigamboni!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...