Wananchi wa kutoka maeneo mbalimbali wa jiji la Dar Es Salaam wakishuhudia bango lenye tangazo la bia ya Ndovu Special Malt lilivyofanikiwa kuwekwa katika teknolojia ya hali ya juu zaidi na ya Kwanza Nchini Tanzania ya 3D ambayo inamfanya mtu kuweza kuona picha zilizopo kwenye bango hilo kwa ukaribu mkubwa na ubora Zaidi.Bango hilo lipo eneo la Conner Bar Sinza jijini Dar es Salaam ambapo watu wanazidi kumiminika kushuhudia bango hilo linalodhihirisha ubora na usahihi mkubwa wa Bia ya Ndovu Special malt.Tangazo la Ndovu Special Malt la 3D…Ni la kwanza Tanzania na lipo katika kiwango tofauti sana kinachoweza kumfanya mtu na mpenzi wa bia hiyo kupata wasaaa wa kuona kile kinachoifanya bia hiyo kuwa tofauti na ya kimataifa zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Hii picha hapa bloguni ni Tangazo pia...Promo!!!!!

    ReplyDelete
  2. Sasa wafanyakazi wa hilo shirika la ndovu wanakaa na kugawa miwani za 3D kwa wapita njia ili waweze kuona hizo picha za 3D? Hiyo technologia haina faida kabisa kwa wanao tangaziwa kwa sababu hakuna mtu anaetembea na hizo miwani za 3D. 99.99% ya watu wataona hilo bango kama la kawaida.

    ReplyDelete
  3. then what? hivi tutaendelea kweli kwa kuendekeza, kutangaza na kusifia ulevi?

    ReplyDelete
  4. tangazo la aliyelipwa kutengeneza tangazo. inaboa.

    ReplyDelete
  5. Kumbe ni jamaa walipigwa posho kidogo, sasa hiyo 3D mpaka uvae miwani maalum.
    Ok,promo ya ulevi si mbaya.
    Mbegu

    ReplyDelete
  6. inamaanisha kila mpita njia ili aweze kuliona tangazo hilo na kulielewa inabidi apitie hapo bar au ofisini kuchukua miwani ya 3D ili aweze kuona hilo tangazo????

    au watu wanatoka sehemu mbalimbali za jiji kufika hapo kujionea hilo tangazo la kukanyaga kilevi kizazi bora cha badae???

    ankali pamoja kuwa unapata ulaji kupitia haya matangazo ya pombe lakini hutakiwi kusifia au kulipamba kwa maneno tangazo la kilevi kiasi hicho

    itakuwa vyema kama tukishiriki kuyapamba na kuyasifia matangazo ya kusaidia jamii kama mambo ya ELIMU HUDUMA ZA KIAFYA N.K

    hayo ni maoni yangu mdau wa santo domingo.

    ReplyDelete
  7. Je ni kila mpita njia atakuwa na hizi miwani?

    ReplyDelete
  8. Hapo nikopita wakaniofa miwani nikasema samahani mimi ni muislam, sisapoti pombe, tayari wataniita sijasoma.

    ReplyDelete
  9. Ukitaka kuona tangazo inabidi ununue ndovu na miwani ya 3D, tanzania wenzetu wanaenda mbele sii tunarudi nyuma, Mashaka

    ReplyDelete
  10. Juu pana tree D chini wana three Du.
    Si bora wangedhamini kivuko kwa walemavu kuvuka barabara chenye tangazo la kawaida tu .

    ReplyDelete
  11. kweli makampuni ya wazungu yanatupiga bao angalia hilo tangazo na hilo eneo lililowekwa hapo chini ni aibu kubwa watu wanajari biashara zao wakati mazingira yanatisha uuufff shame

    ReplyDelete
  12. ushamba tu umetuzidi.Kuweka bango la 3d lazima kuweko hizo miwani wakati wote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...