Naibu Katibu Mkuu Mtendaji Ofisi ya Rais Kamisheni ya Tume ya Mipango, Bw. Clinfford K. Tandari, akifuatilia majadiliano yaliyohusu Utekelezaji wa Mpango wa Istanmbuli kwa nchi maskini maarufu kama LDGs. Mkutano huo ulifanyika nchini ya Kamati ya Pili ya Baraza Kuu la 67 la Umoja wa Mataifa.

 Alipopata nafasi ya kuchangia utekelezaji wa Mpango huo ( Istambul Plan of Action) Bw. Tandari pamoja na mambo mengine, alisema Tanzania imekwisha kuuingiza mpango huo katika Mpango wa Kitaifa wa Maendeleo wa Kila Miaka Mitano , lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba Tanzania inaondoka katika kundi la nchi maskini na kuingia katika kundi la nchi zenye uchumi wa kati ( Middle Income Countries), ikifikapo mwaka 2015.

Akabainisha kwamba ili kufikia hatua hiyo, Serikali imejiwekee vipaumbele kadhaa ambavyo vimeainishwa katika Mpango huo wa Miaka mitano. Akavitaja baadhi ya vipaumbele hivyo kuwa ni Kilimo na Usalama wa Chakula, uboreshaji wa huduma za Elimu, Afya na huduma za maji na usafi wa mazingira, maendeleo ya miundombinu ikiwamo ya barabara, reli, bandari na huduma za nishati. 

Akavitaja vipaumbele vingine kuwa ni usawa wa kijinsia na uwezeshashi pamoja na kujenga mazingira bora ya biashara na ushindaji wa kibiashara. Katika hatua nyingine Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Ofisi ya Rais Kimisheni ya Mipango alieleza kwamba Tanzania ingeweza kufikia lengo lake la kutoka katika kundi la nchi maskini na kuwa kundi la nchi ambazo uchumi wake ni wakati kabla hata ya mwaka 2015 ikiwa tu washirika wa maendeleo ya kichumi watatekeleza ahadi zao za kuisaidia Tanzania zikiwamo zile walizotoa miaka mingi ya nyuma na ambazo hazijatekelezwa hadi sasa. 

Hata hivyo akasema Tanzania imejidhatiti katika kuhakikisha kwamba inaboresha makufanso ya mapato yake ya ndani ikiwa ni pamoja na kupanua wigo wa kodi na kuibua vyazo vipya vya mapato ili kuziba pengo litokanalo wa wadau wa maendeleo kushindwa kutekeleza ahadi zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hatuwezi kamwe kuondoka kwenye kundi na nchi maskini huku tukiwa hatufanyi kazi na badala yake tunapigania dini badala ya UTAIFA wetu.

    Ikimbukwe nchi zilizoondoka kwenye umaskini, hawakuondoka kwa maneno kama wabongo tulivyozoea, walifanya kazi kwa bidii na kuweka mbele maslahi ya nchi zao. Je hapo sisi tuko wapi? Kuna yoyote anayejali maslahi ya nchi? Jibu ni hakuna, sasa kwenye umaskini tutaondoka je?

    Yako wapi madaraja waliosema watajenga? Wenzetu Kenya walitusikia tukizungumzia madaraja wakaanza kujenga, sisi tumebaki na maneno tu..mara nani kafanya nini, mara mamilioni yako USWISI, mara.....khah...inaumiza sana

    ReplyDelete
  2. Na ufisadi tutamuachia nani? Thubutuuuuuu

    ReplyDelete
  3. hahhhhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, this is the biggest crap I have ever heard in my life. It can't be and it is impossible. We are a second country in the World to depend on Aid, first being Afghanistani. Probably first in ufisade - uozo mtupu. Keep dreaming. Even my grand mother will not believe this though she is dead. Killed by mafisadi, wanaokula hela za kununua madawa ya hospitali. Wake up wabongo

    ReplyDelete
  4. Uongo mtupu huo, come 2015 we should look for this guy and have a long hard chat with him. What a joke!!!!!! Unadanganya nani??

    ReplyDelete
  5. Mwongo huyo, wala hana aibu!!!

    ReplyDelete
  6. kwakweli kuondoka kwenye umasikini ni ndoto kwetu sisi Tz kwani hata wanaotuongoza wamerizika na hali halisi ya nchi yetu tunatia haibu wajameni yani hapo ukifika na wageni unatamani ujifiche kwanzia angani ukiangalia unakokwena kutua nikituko fika sasa air port ndo kabisasaaa nenda sasa mitahani foleni zisizo na sababu nashangaa hawa viongozi wakifika nchi za watu hata awatamani awana wivu au kujifunza basi kama ubunifu awana jamani sii kwamba hatuwezi kuwakuta, ubinafsi umetuzidiiiii

    ReplyDelete


  7. Haha nacho penda kuhusu nchi yangu tunapenda sana kuota hvyo nadhani nivizuri kuendelea kuota,,,, Kwa elimu gani tunayo pewa tuondoke kwenye nchi masikini??

    Tena naona wanakosea kusema Tanzania ni 3rd world country me nadhani ilitakiwa iwe 5th world country

    ReplyDelete
  8. Ni kweli kabisa na naungana nawe mdau hapo juu, sisi wabongo tumebaki kusema tu bila ya kutenda na haya yote yametokana na viongozi wetu kuwa hodari sana wa kusema kuliko vitendo kwani muda wao mwingi wanautumia kutafuta ni wapi penye mwaya ili wakwapue na kuendelea kujilimbikizia mali kujali wananchi wako kwenye hali gani na taifa kwa ujumla wake. Tutamkumbuka sana baba wa taifa mwalimu Nyerere kwani aliwahi kusema kama yeye angetaka kujilimbikizia mali angekuwa nazo nyingi sana wakati ule, lakini hakutaka kwani alijali sana taifa hili pamoja na wananchi wake, lakini viongozi wengi wa sasa ni tofauti kabisa ahadi nyingi vitendo hakuna. Mimi nataka niwakumbushe kitu kimoja "haya yote yana mwisho na mwisho wake ni siku ile utakaporudi kwa Mwenyezi Mungu ili kujibu ni nini uliwafanyia wananchi waliokupa uongozi na ulionyesha image gani kwa huo huo uongozi aliokupa Mungu pia?"

    ReplyDelete
  9. Mafanikio nchini Tanzania tutayapata sio kwa ndoto ila kwa Maamuzi MAGUMU NA UJASIRI!

    SIO KAZI NGUMU, NI KIASI TU CHA KUWACHUKUA WALE WATU WASIOZIDI 45 (Mafisadi) NDANI YA IDADI YETU YA WATU 45 MILIONI TUKAFANYA HIVI:

    1.TUKAPIGA MAHESABU YA WIZI WALIOFANYA TUKAWACHIA WANACHOSTAHILI NA KUWAFILISI KWA KURUDISHA MALI ILIYOZIDI (YA WIZI) MIKONONI MWA SERIKALI.

    2.TUKAWEKA SHERIA MPYA KALI ZA USIMAMIZI WA MALI NA UTAFUTAJI WA FEDHA.

    3.TUKAWAACHIA HURU (wala hakuna sababu ya kuwaadhibu) KWA KUWA MALI WAMERUDISHA.

    (NI WAZI KASI YA WIZI NA UFISADI INAIZIDI KASI YA MAENDELEO NCHINI)

    BILA YA HIVYO TUTA CHOTA MAJI KWA PAKACHA NA HAYO MAENDELEO KUFIKIA HIYO 2015 ITAKUWA NI NDOTO ZA MCHANA!!!

    ReplyDelete
  10. Nchi yoyote inao promote mambo ya kudangnya wananchi utapele,ufasidi pamoja mambo ya utumwa huwezi kuondosha umaskini. Changamoto kwa viongozi hakuna heshima. Wana tegemea heshima kutoka nje siyo wananchi. Wananchi wana ishi kwa mpigao siyo ya serikali lakini system ya ubaguzi na ufisadi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...