Kwa niaba ya familia ya Dr.Balandya, Kaijage na Mgimba, ningependa kutoa shukrani za dhati kwa msaada mkubwa wa hali na mali mlioutoa kwa siku zote za msiba wa mama yetu mpendwa aliyefariki Ijumaa 05-Oct-2012 na kuzikwa Jumatatu 08-Oct-2012. 

Tunashukuru sana na tumeguswa sana kwa faraja mliotupa na kwa kutoa muda wenu kwa kuwa pamoja na sisi kwenye kipindi chote hiki kigumu cha majonzi ya msiba huu. Mmeonyesha moyo wa kujali na upendo wa hali ya juu sana kwetu. Tunaomba muendelee na moyo huo huo. 

Tumejifunza mengi sana kutokana na wema wenu. Shukrani za pekee ziwafikie pia wale walioweza kufika kwao nyumbani (Kimara Kilungule) na mazishini (Mbezi Kibanda cha Mkaa) ambako ni maeneo yaliyo nje sana ya mji na ukichukulia kwamba mazishi yalifanyika siku ya kazi. 

Sio rahisi kutoa shukrani kwa mtu mmoja mmoja. Tunaomba wote mzipokee shukrani zetu za ujumla. Mungu awabariki sana na awarudishie mara nyingi zaidi pale ambapo mtakuwa mmepungukiwa. Bwana ametoa, bwana ametwaa. 

Jina la mwenyezi Mungu lihimidiwe. Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un. Roho ya marehemu apate rehema kwa Mungu apumzike kwa Amani. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina. Misa ya shukrani itafanyika Jumapili tarehe 14-Oct-2012 saa 1:30 asubuhi katika Kanisa la RC la Mtakatifu Monica Kimara Kilungule. 

Asanteni sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Poleni sana Kaijage na familia nzima.. Mungu amlaze Mama mahali pema peponi... Amina... Ignas!

    ReplyDelete
  2. Thanks Ignas Chilewa. Tupo pamoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...