Dear Colleagues,
 Naomba niwasimulie yaliyonipata jana ili na ninyi mchukue tahadhari mapema!
 Jioni baada ya kutoka kazini nilielekea nyumbani  Tabata Kinyerezi moja kwa moja na nilipitia njia zifuatazo.Nilipita Fire,Magomeni,Round about ya Kigogo,Tabata-Dampo, moja kwa moja hadi Tabata Segerea then Kinyerezi.Nilipofika njia ya kuingia kwangu,pembeni kuna Bar inaitwa Fantastic na ina Kigorofa,basi nikamkuta jamaa yangu mmoja nilyekuwa na mazungumzo naye then nikapark gari then nikashuka na kuongea naye nikiwa nimesimama umbali kidogo kama hatua kumi na tano na nilikopark gari langu-Noah!Baada ya mazumgumzo ya hardly dk 5 nikarudi kwenye gari ili niingie home,hamadi nikakuta tayari kioo cha gari cha kulia nyuma ya kiti cha dreva umeshavunjwa na wamechukua lap top yangu binafsi, iliyokuwa ndani ya begi na kulikuwa na documents nyingine nyingi na ziliakuwa original docs-vyeti vya shule na kadi za benki!
Ila upande wa pili wa barabara kulikuwa na waendesha pikipiki wenge tu sasa nikaanza kuwauliza je walimwona nani akiingia kwa gari langu,sikupata majibu hata kidogo!Katika kufutailialia na nikaenda polisi,walinieleza kuwa kuna wimbi la vijana ambao hutumia magari ya kifahari na pikipiki ambao kazi yao ndo hiyo tuu!na walijaribu kufutailia zaidi na ikaonekana kuwa hawa watu wanapenda kufuatilia watu nyuma na hata kama kuanzia mjini hadi katika vitongoji vyetu!Hii ni story ya kweli na imenitokea jana jioni ndugu zangu.
Sasa lengo la kuwasimulieni kisa chote hiki ili nanyi mchukue tahadhari!hata kama mtu unashuka kwenda kuchimba dawa,shuka na all your belongings especially your computer na vitu vyote muhimu ndugu zangu.Usipuuzie kwani yaliyonikuta jana sijalala hata kidogo maana Hasara niliyopata ni kubwa isiyopimika ndugu zangu.Katika kundelea na uchunguzi wamebaini kuwa maeneo ya tabata ni hatari sana kwa sasa na hawa wahuni wanatumia gari aina ya Rav 4 nyeusi,na wakati mwingine wanatembea na Toyota OPA.Ndugu zangu nawasihi sana ikiwezekana acha laptop nyumbani  beba external disc au flash disc maana kwenye gari sio tena shehemu nzuri ya kuhifadhia docs zako.
 Hayo ndo yaliyonipa jana na sina jinsi nabaki tu mdomo wazi! Samahanini kama nitakuwa nimewaboa but nawaokoa na ninyi ndugu zangu. Mtu yoyote atakayeona karatasi zime tupwa mahali tafadhali jaribu kuangalia maana na kama ni zangu nitashukuru nikizipata.Asante

Cayus

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Pole sana bwana Cayus kwa yaliyokupata. Ingekuwa vizuri ukataja jina lako kamili yaani yote mawili au hata matatu. Pia uweke namba yako ya simu ili kama tutapata clue yoyote au kuona hayo ma docs tuweze kukupatia. Kama hapa inavyoonekana, si rahisi kukupata hata kama tutakuwa na msaada kwako

    ReplyDelete
  2. Hakuna wizi wowote wa ajabu, ni wewe mwenyewe tu umekuwa mzembe. Utawachaje vitu ambavyo ni "valuables" kwenye gari ndugu yangu? Nani asiyejua wivu wa dezaini hapa Dar siku hizi?

    ReplyDelete
  3. Pole sana ndugu. Nami maeneo ya nyumbani ni huko huko, japo nipo nje kwa sasa, lakini naelewa fika unachozungumza. Mimi nililizwa laptop na mgeni niliyempa lift ambae alinipungia mkono kunisimamisha kama mtu anaenifahamu, akiwa na tabasamu kubwa akisimamisha kwa juhudi zote. Walikuwa wawili. Mmoja akaniambia anaomba lifti anafika hapo mbele tu. Very humble, Dress-code suti na tai, middle-aged, 50s hivi, huwezi kudhani kuwa anaweza kuwa mwizi wa kutupa. Kuwapa lifti ya kuwasogeza tu toka Tabata Muslim nilipowakuta, hadi junction ya Tabata/Mandela Rd ikawa kosa nililoli-regret hadi leo. Jamaa akaniibia lamptop yangu nikiwa nae kwenye gari nimekaa nae side to side, akaniachia begi la laptop tupu. Nikagundua baada ya kufika ofisini nanyanyua begi nitoke kwenye gari, naona begi tupu. Nakubaliana na ndugu yangu huyu na na-feel loss ya laptop yake, kwani sio li-mashine tu kwani lingine utanunua, ila nyaraka zilizokuwemo humo ndio hazina kubwa unayoisikitikia. Nilikuwa hapo. Nilipoteza thesis document yangu ya muhimu wiki chache tu kabla ya ku-defend shahada yangu. Ilibidi nianze kazi nikiwa na 3-quarters ya thesis. Unarudishwa nyuma kiasi gani namna hiyo? Fundisho nililipata, tangu siku hiyo katu sitoi lifti kwa mtu yeyote nisiyemfahamu hata anisimamishe mtaani jirani na kwangu.

    ReplyDelete
  4. ok pole sana ni tahadhari kwa wengine. ila mnapotumia lugha ya kiswahili mutumie kwa ufasaha haina haja kuingiza kimombo, TUKUZE LUGHA YETU.Kama unaijua sana englishi basi yote ungeandika englishi.

    ReplyDelete
  5. pole sana.Lakini pia nyie watu wa hapo nyumbani mmezidi kujionyesha mnatembea na simu tatu laptops kuwakogoa wenzenu.kwani ukiweka kwenye buti ya gari nani ataona?

    ReplyDelete
  6. pole sana kaka

    ReplyDelete
  7. Pole mdau, siku hizi usiacha kitu ndani ya gari kama mwenyewe humo. Je uliweka bima ya "Comprehensive"?

    ReplyDelete
  8. Pole sana mambo kama haya yana tokea mara nyingi kwenye mjiji mengi duniani.Iko wapi tekenologia?Hakuna security camera?

    ReplyDelete
  9. Pole sana kwa yaliyokupata! Asante sana kwa taarifa hiyo! Inachoshangaza kumbe Polisi wanajua habari zote hizi! Lakini kwa sababu wanapokea sana rushwa kutoka kwa wezi hao wanaona ni sawa tu! Kama kweli wanawapenda wananchi wao wasipatwe na majanga kama yako wangeshafanya mitego mingi sana na wahusika wote wangepewa adhabu zinazostahili kutokana na makosa yao! Polisi yetu imeathirika vibaya sana kwa kuweka pesa mbele kuliko kazi! Pole sana ndugu yangu.

    ReplyDelete
  10. Sasa wewe nduguyangu hukujuwa pakuweka laptop ila display,!!!.kwanini huja chukuwa hadhari ya kuweka nyuma ya buti,eee.nduguyangu pole sana mimi sio mkaazi wahapo bongo naishi europ huku vilevile kuna wizi kama huuo na watu wanapewa tahadhari ya kuweka vitu nya thamani nyuma ya butikama satnav,laptop,Reyband,WALLETnk. hata kama unamfuko umetia nyanya basi uweke nyuma au weka wazi kuwa hizi nyanya usiifunge,na yote olosema kweli ila hujasisitiza kuwa watu waweke vituvyao vya thamani nyuma ya gari zaoo,aaa ,pole sana mdaw

    ReplyDelete
  11. pole sana, ndomana nasema kila siku mtu yoyote ataemuonea huruma mwizi akiwa anachomwa moto au kupigwa basi na huyo nae achanganywe....

    ReplyDelete
  12. Wizi huo hupo sehemu zote dunia. Vitu thamani weka kwenye boot, lakini huyu anasema alikuwa na Toyota Nohah, sasa boot itoke wapi? Siku ilikuwa imefika.

    ReplyDelete
  13. Nakushangaa mpaka leo hujajua aina hiyo ya wizi, sisi tunaujua yapita miaka minne sasa. Pole.

    ReplyDelete
  14. Jamani hii dunia sijui tunaenda wapi? Wizi umezidi hasa wa laptop, juzi nilikuwa napita maeneo ya Tegeta darajani majira ya mchana nikaona dada anakabwa katoa macho kwenye yale machuma ya darajani nika park bahati nzuri kuna wakaka waarabu walishuhudia ilo tukio nao walipark na kwenda kumpa kichapo yule kaka kumbe alikuwa kibaka anampora simu. Kaka alikuwa kavaa smart kachomekea huwezi kumdhania kama ni kibaka. Cathy Dsm

    ReplyDelete
  15. Nakubaliana na anonymous hapo juu kabla ya kuanza safari yoyote vitu vya thamani weka ndani ya buti ya gari.

    Hata huku ulaya huwezi kuona mtu anapaki gari na kugunga vioo huku ameacha vitu vya thamani ktk sehemu ya abiria au siti za gari. Si laptop tu hata makoti na kadhalika vyote ulaya wanaweka ktk buti la gari ili kuondosha viwewe vya vibaka kuvunja kioo wakifikiria labda jacketi, koti n.k limetumika kuficha vitu vya gharama.

    Tufanye ulinzi shirikishi kwa sisi wenyewe kuwa waangalifu kuhifadhi vitu ktk buti za gari, buti ya gari si kwa ajili ya kubebea kiroba cha mkaa wa kuokea nyama choma.
    Mdau
    Jijini London

    ReplyDelete
  16. Pole sana ndugu.Nyie mnaosema 'BUTI',Noah ina 'buti' lipi?.Na hapo usiseme umelizwa Laptop tu na docuents andaa na Tsh150,000 hivi kununua kioo kingine.Wana kera sana

    David V

    ReplyDelete


  17. Mbona huo wizi huko nyumbani tuu uko kila mahali hata huku Canada upo tena i think hata ule wa kuibiwa na maderaca pikipiki nasikia umeingia bongo hivi karibuni wakati huku ulikuwepo tokea nimefika huku last 9 years

    ReplyDelete
  18. Fantastic, kijiwe hatari hicho ati

    ReplyDelete
  19. Ndugu Cayus pole sana hiyo ndio changamoto ya Ugumu wa Maisha.

    Isipokuwa wengine wanakuwa na njia mbaya ya kuyafikia malengo ya maisha kama aina hiyo ya wizi!

    ReplyDelete
  20. Hakuna jipya hapo, wizi huu upo dar es salaam muda mrefu. hata kwenye buti msiweke siku hizi wanatemebea na censors, ambazo zina-sensi vitu vya electronics vyote vilivyo kwenye gari. So msiweke kwenye buti

    ReplyDelete
  21. Hakuna jipya hapo, wizi huu upo dar es salaam muda mrefu. hata kwenye buti msiweke siku hizi wanatemebea na censors, ambazo zina-sensi vitu vya electronics vyote vilivyo kwenye gari. So msiweke kwenye buti

    ReplyDelete
  22. Pole sana kwa yaliyokupata, chakushangaza hiyo gari Rav four police wanaijua, kuna mtu aliibiwa maeneo ya TCRA police wakatoa taadhali juu ya hiyo gari kuwa ni Rav 4 nyeusi na hao vijana ni chotara wa kiarabu, sasa kama wanawajua kwa nini wasiwakamate, ndio maana watu hawana imani na jeshi la police, tena walivyo wa ajabu wanakutajia kabisa mwizi nani, hao vijana wanajulikana wanazunguka mji mzima kazi yao ni hiyo tu wakiona gari imepark wanaenda kupark gari karibu sana ili mtu anayepita asione wanapochomoa vitu.

    ReplyDelete
  23. Mdau aliyelizwa ameshaambiwa kua wezi hao siku hizi wanakufuatilia kuanzia ulipotoka na Noah haina buti sasa sijui mnaomwambia amekua mzembe mlitaka afanye vipi? Labda angeshuka na mzigo wake. hata hivyo pia huwezi kujua labda wangeshuka kwenye gari lao na kumkwapua ambayo ingekua na madhara zaidi kwakua hujui na wao wana silaha gani za kujiami pindi plan zao zikiwaendea visivyo.

    ReplyDelete
  24. POLENI SANA NA WOTE WALIOIBIWA KOKOTE KULE. SABABU KUBWA NI KUWA WATU WENGI NI WAVIVU HAWATAKI KUFANYA KAZI YA KUTUMIA NGUVU ILA KUPORAPORA MALI ZA WALIOZIHANGAIKIA. TUWE MACHO/MAKINI KWANI HATA TUNAOTEMBEA KWA MIGUU KUNA MADEREVA WA MAGARI NA PIKIPIKI WANAPITA KARIBU YAKO NA KUKUPORA MZIGO WOWOTE ULIONAO, HII IPO SEHEMU NYINGI NA INAFANYIKA MUDA WOTE HIVYO TUJIHADHARI KWA HIYO MALI ITAPOTEA NA UTATAFUTA TENA LAKINI UNAVYONYANG'ANYWA AU KUPORWA UNAWEZA KUANGUKA NA KUBURUZWA UKAUMIA AU HATA KUPOTEZA MAISHA.

    ReplyDelete
  25. Unajua wezi wa aina hiyo huwa hawakrupuki.....huwa wanakuwa wanajua tabia na nyenendo zako za kila siku....kuwa ukitoka job unaendaga home moja kwa moja au unapitia mahali.....sasa, hapo mahali ndio zoezi hufanyikia.

    My take ni kuwa, kama una tabia ya kupitia mahali ukitoka kazini...basi jamaa walikuotea....lakini, kama unatabia ya kutoka kazini na kwenda nyumbani moja kwa moja, basi yule jamaa yako ulieongea naye hizo dk 5, anahusika katika mchoro.

    Akusimamishe kwakua anakujua, tena akuongeleshe hadi jamaa wampe signal kuwa kazi imefanyika ndio akuruhusu uondoke.

    Tunapoendesha magari tuhakikishe kuwa:-

    1. Tumelock milango na tumepandisha vioo kiasi kuwa ni vigumu kwa mtu kupenyeza mkono kufungua.

    2. Tuwe na tabia ya kuangalia at least gari tatu nyuma, ni ipi inakufuatilia kila unapokunja.

    3.Tusiwe na utaratibu unaofanana, sio kila siku njia hiyo hiyo, bar hiyo hiyo, parking hiyo hiyo.

    4. Ukipak gari mahali, mkabidhi hata muuza duka au mtu yeyote katika eneo ulilomkuta ili uje umtoe...atalilinda.

    5. Usimpe mtu funguo wako, akauminya kwenye sabuni akawa na nakala yake.

    6. Usiache hata begi lenye nyanya kwenye gari, ili kutowatamanisha wezi wasivnje kioo chako.

    7. Kama una wasiwasi na eneo utakalo paki gari....lipaki gari,tokomea gafla then rudi baada ya dakika 2 au 3 hivi....!

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  26. Hakuna kipya siyo Dar peke yake. Miji mikubwa yoyote yana changamoto mbona wakenya pia wanazungumza mambo kama haya huko Nairobi, pia Afrika kusini. Changamoto kila mahali. Mbona WaTanzania wegeneo waajabu wana kuja kulalamika kwenye blog waki uzembe wao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...