Msemaji katika Hafla ya Women in Balance Kitchen Party Gala Mhadhiri Msaidizi wa Idara ya Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Chris Mauki akitoa somo la Saikolojia kwa wakinamama na wasichana waliohudhuria hafla hilo iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee VIP Hall jijini Dar.


Life Style Designer of Sex and Relationships kutoka Kenya Bi. Getrude Mungai akitoa somo la kuhusiana na masuala ya mahusiano ya kimapenzi kwa wenye ndoa na wasiokuwa na ndoa ambapo amesema vipo vitu vingi vinavyochangia kuboresha ama kuharibu mahusiano hayo ambapo wahusika wanatakiwa kuvifahamu na kuvitilia mkazo ili kudumisha mahusiano yao.


Mafunzo kwa vitendo yalihusika pia.
Msemaji wa mwisho alikuwa ni Mama Victor aliyewaacha hoi kwa vicheko wanawake waliohudhuria Kitchen Party Gala ambapo alizungumzia masuala ya uvumilivu katika ndoa sio tu kukosekana kwa kipato ndani ya nyumba bali hata mikimiki ya Unyumba kwa wanandoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hii inadhihirisha jinsi ambavyo wanawake tunatumika na kukubali kutumika kama sex-tool! Kulikoni hili Gala lisihusishe wanaume kwa pamoja kupata yaliyojiri? It takes two to tangle.

    ReplyDelete
  2. I SEE, HIVI WANAWAKE PEKEE NDO WANATAKIWA KUWA WAVUMILIVU KWENYE NDOA ZAO? KWAHIYO WANAUME WAFANYE MAMBO YAO HATA YA AJABU MWANAMKE UWE UVUMILIE TU.... KAZI KWELIKWELI!!

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza umenifurahisha kweli.

    Nyumba ni Mwanamke na Mwanamme, iweje hilo GALA liwe ni la wanawake tu?

    Mwanamke tu ndio ajue jinsi ya kuishi na mwenzie lakini mwanamme hatakiwi kujua jinsi ya kuishi na mwenzie?

    Binti wakati anaolewa ni sawa kufanyiwa Kitchen party, ndio anakwenda kuyaanza yale mambo, hayaelewi kiundani, wewe mama umeshakaa kwenye ndoa miaka kadhaa kwa nini usiende na mumeo nae akajue yanayojiri.

    Wanawake tubadilike

    ReplyDelete

  4. Hicho kitengo cha bwana Mauki hakuna akina mama?

    Kitchen party is for Ladies only.

    ReplyDelete
  5. Shangazi lake na bi. harusi siku hizi hawatumiki na familia kufunda walengwa kwa siri na staha uwani?

    ReplyDelete
  6. Na huyo bwana katikati ya wanawake anatafuta nini?

    ReplyDelete
  7. Hawa wawezeshaji wanaimarisha mfumo Dume ambao wengine sisi tunaupiga vita. Tutakomboka kweli Kifikra, Kijamii, Kiuchumi na kitaaluma? Kama mwanamke pekee ndiye abebe jukumu la kuhakikisha, kujenga na kuimarisha Nyumba na Unyumba, ustawi wa familia, afya kwa wagonjwa na wazee katika jamii yake na ya Mume! Kaaaaazi Kweli kweli.

    ReplyDelete
  8. Kwa nini wanawake wasio na haki ya ku starehe pamoja na wanawake wenzao? Siyo wanawake wote wana penda kushirikiana kwenye siasa au dini. Kila kheri,

    ReplyDelete
  9. Watu wanatafuta pa kupatia ulaji tu.Mama na mashangazi wanatosha kufunda mtu haya mambo ya kitchen party imekuwa watu kupata vyombo tuuuu mambo ya muhimu yanasahauliwa. Kubalance mambo ni kweli ingebidi watu wote wafundishwe si kina dada tu kwani wao ndo wanakosea peke yao wakaka hawakosei?

    ReplyDelete
  10. Kitchen Party Gala nauliza,

    Hivi wale Waume kwenye ndoa wanaokunywa na kulewa chakari wakirudi usiku wa manane bado Mwanamke avumilie tu?

    Mume hatoi kodi ya meza Mke avumilie tu, ilhali inajulikana Mume anatumia fedha nyingi kulewa na kwa Vimada?

    SOMO LILITAKIWA LIWAFIKIE JINSIA ZOTE WAKE KWA WAUME ILI KU BALANCE KAMA MNAVYOSEMA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...