ZAIDI ya watu 200 wamefanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho bila malipo yoyote katika mkoa wa Iringa wakati wa kampeni ya upasuaji wa macho iliyofanyika kwa siku mbili mkoani hapa.

Wagonjwa hao wenye matatizo ya kutokuona mbali na karibu na wenye upofu walijitokeza kwa wingi katika  hospitali ya misheni ifunda na hospital ya halmashauri ya wilaya ya kilolo iliyopo ilula ili kupata huduma hiyo.

Kutokana na upofu kuwa tatizo la kidunia Shirika la Sightseves kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la kusaidia jamii la nchini Uturuki (IHH) limeendesha kampeni hiyo ya upasuaji wa macho ili kupambana na tatizo la upofu mkoani hapa.

Akizungumza na Mwandishi wakati wa kampeni hiyo Mratibu wa macho mkoa wa Iringa, Dokta George Kabona alibainisha kuwa Iringa  upofu upo kwa kiasi kikubwa ambapo zaidi ya watu 9,412 wanakabiliwa na tatizo hilo.

Kwa upande wao mmoja wa wagonjwa Martini Msasa ambaye alifanyiwa upasuaji katika hospitali teule ya Ilula alisema kuwa anawashukuru sana madaktari pamoja na mradi wa IHH kwa kuwakumbuka kwani umewafanya kuweza kuona na hivyo wataweza kwenda kufanya kazi mashambani na biashara ili kujikimu kiuchumi tofauti na mwanzo walikata tamaa na kuwa watu wa kukaa ndani na kuhudumiwa kwa kila kitu.

Huduma hiyo ya upasuaji hutolewa bila malipo yeyote na hivyo watu wenye upofu na matatizo ya macho walijitokeza kwa wingi kupima katika vituo hivyo vya afya na kupata huduma wengi wao wakiwa ni wazee.

Sambamba na hayo pia wameshauri kuwatumia wenyeviti wa mtaa kufikisha taarifa za huduma kama hiziili taarifa ziwafikie walengwa wote mara zinapojitokeza vijijini ili watu wengi waweze kujitokeza zaidi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...