Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi katoni hamsini za maji na fulana 1,000 kutoka Vodacom kusaidia matembezi ya hisani yanayofanyika kesho Jumamosi 12 Oktoba, 2013 jijini Dar es salaam kuleta hamasa kwa wananchi kuchangia kampeni ya kumaliza uhaba wa madawati katika Manispaa ya Ilala. Kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Jerry Silaa aliyendaa matembezi hayo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kupokea katoni hamsini za maji na fulana 1,000 kutoka Vodacom kusaidia matembezi ya hisani yanayofanyika kesho (Jumamosi 12 Oktoba, 2013) jijini Dar es salaam kuibua hamasa kwa wananchi kuchangia kampeni ya kumaliza uhaba wa madawati katika Manispaa ya Ilala. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania,Bw. Salum Mwalim.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa pili kushoto) na Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim wakionesha kwa waandishi wa habari fulana zilizotolewa na Vodacom kusaidia matembezi ya hisani yanayofanyika kesho Jumamosi 12 Oktoba, 2013 kuibua hamasa kwa wananchi kuchangia kampeni ya kumaliza uhaba wa madawati katika Manispaa ya Ilala. Vodacom imetoa fulana 1,000 na maji katoni 50. Wengine pichani ni Zainabu Katimba na Halima Bulembo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam waliojitolea kusaidia usimamizi wa matembezi hayo.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa(wa pili kuhsoto) akipokea kutoka kwa Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim sehemu ya fulana 1,000 zilizotolewa na Vodacom kusaidia matembezi ya hisani ya kuhamasisha jamii kuchangia kampeni ya kumaliza uhaba wa madawati katika Manispaa ya Ilala. Wengine pichani ni Zainabu Katimba (kushoto) na Halima Bulembo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam waliojitolea kusaidia usimamizi wa matembezi hayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...