Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na wajumbe hao katika Manispaa ya Kinondoni kabla ya kuanza kwa ziara. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda.
Wajumbe wakiwasili Kata ya Mabwepande kukagua ujenzi wa Hospitali ya Mabwepande.
Mhandisi wa Majengo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi Brighton Kimaro akiwaongoza Meya wa Manispaa hiyo Yusuf Mwenda (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki na wajumbe hao kukagua jengo la hospitali ya Mabwepande.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida (kushoto kwake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki na wajumbe hao kuhusu maendeleo ya ujenzi wa soko la kisasa la wafanyabiashara ndogo lililopo ndani ya kituo kipya cha daladala cha Sinza.
Wajumbe wakiingia kukagua kituo cha kisasa cha polisi kilichofungwa CCTV Camera kilichopo ndani ya kituo cha daladala cha Sinza.
Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Ismail Mafita akitoa maelezo kwa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kituo cha daladala cha Sinza. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida (wa pili kulia) na Meya wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...