Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Ngosi Mwihava
(katikati) akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya lugha ya Kireno
Zahoro Athmani mmoja kati ya wanafunzi 15, waliohitimu mafunzo hayo,
ambapo 7 kati yao tayari wamepata ufadhili wa masomo ya Shahada za
Uzamili na Uzamivu katika fani za mafuta na gesi nchini Brazili. Kulia ni
Balozi wa Brazili nchini, Fransisco Carlos Luiz, akimpongeza mwanafunzi
huyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava,
akiongea na wanafunzi waliopata waliohitimu mafunzo katika lugha ya
Kireno ambapo saba kati ya 15 tayari wamepata ufadhili wa kujiunga
na vyuo vya mafuta na gesi nchini Brazili, Kushoto ni balozi wa Brazili
nchini Fransisco Carlos Luiz (kushoto), wengine katika picha ni baadhi ya
watumishi kutoka Kampuni ya kuchimba gesi ya PETRO Bras, Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Wizara ya Nishati na Madini.
Balozi wa Brazili nchini Fransisco Carlos Luiz (wa pili kulia) akiongea
jambo na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi
Mwihava (kushoto) baada ya kuwakabidhi vyeti wanafunzi 15 waliohitimu
mafunzo ya lugha ya kireno kabla ya kujiunga na masomo ya Shahada za
Uzamili na Uzamivu katika fani ya mafuta na gesi , saba kati yao.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava
(wa nne kulia) na Balozi wa Brazili nchini Fransisco Carlos Luiz (wa tatu
kulia) katika picha ya pamoja na Wanafunzi 15 walihitimu mafunzo
ya lugha ya Kireno. Wanafunzi 7 kati yao tayari wamepata ufadhili wa
kusoma masuala ya mafuta na gesi katika ngazi za Shahada ya Uzamili na
Uzamivu nchini Brazili mwezi Machi mwakani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...