Watumiaji wa
simu za mkononi wameendelea kukua kadri siku zinavyo endelea na kumekua
na maswali mengi jinsi gani mtu anaweza kubaki salama atumiapo simu za mkononi.
Hapa
nitaangazia uhalifu mtandao unao ambatana na simu za mikononi na njia za matumizi salama
ya simu za mkononi. Nianze
kuangazia uhalifu unaoweza kusababishwa na simu za mkononi.
Swapping: Huu ni uhalifu
mtandao unao kua kwa kasi hivi sasa maeneo mbali mbali unaotoa fursa kwa
mhalifu mtandao kuwa na matumizi ya simu ya mtu bila ya mwenye simu kujua. Mara
nyingi wahalifu mtandao wana lenga kuiba pesa au kuwasiliana na watu wa karibu
wa mtumiaji halisi wa simu ya mkononi kwa sababu tofauti tofauti.
Hii inatokea
pale mhalifu mtandao anapo kua amepata namba yako ya simu na kusoma
ratiba yako hasa muda gani unakua hauna matumizi makubwa na simu – Baada
ya kujua hivyo kupitia programu zilizopo sasa zina mpa fursa kukutoa hewani na
kuanza kuitumia namba yako ya simu ambapo anaweza kufanya mengi baada ya
kua na umiliki huo ikiwa ni pamoja na kutoa au kuhamisha pesa zako na pia
kuitumia vibaya simu yako.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...